Mtanzania apeperusha vema bendera ya Taifa kwenye Boston Marathon. Ashika nafasi ya 2

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mtanzania Gabriel Geay, ameweka historia kwa kushika nafasi ya pili katika mbio za Boston (Boston Marathon) zilizofanyika kwa mara ya 127 mwaka huu huko Boston, Marekani

Geay alifanikiwa kumaliza mbio baada ya saa 2:06:04 akimaliza nyuma ya kinara, Evans Chebet kutoka Kenya aliyekimbia mbio hizo kwa saa 2:05:54

Evan amefanikiwa kutetea taji hilo mbele ya Eliud Kipchoge (KEN) anayeshikilia rekodi ya dunia katika riadha. Kipchonge ameshika nafasi ya sita katika mbio hizo

AC33B553-B847-4BF5-A99D-54DA2445DC91.jpeg

5259C644-6BB7-4D96-A29A-1E46C60E5F9D.jpeg

Na hizi ndio zawadi wanazopatiwa Washindi katika mbio hizo
8AA72E85-75A5-4AFD-8540-38CF5E7736E6.jpeg
 
Mwaka Jana alikuwa kwenye Mimi Bora na mwaka huu amefanya maajabu... hongera Sana kwake
 
Sio mbaya ujermani alipiga milioni karibu 300 , na sasa marekani kagonga milioni karibu 170 amefanya makubwa kwa kuitangaza nchi yetu
 
ni zaid ya fedha iyo m200 kabisa
 
Tunamshukuru Mama Samia kwa huu ushindi wa mwanariadha Geay. CCM iliahidi sasa inatenda.
Tatizo la hii nchi ni kubwa sana na kiongozi akipatikana wa kuyarekebisha anaitwa dikteta. Haiwezekani nchi hii watu milioni 60 awepo Geay mmoja pekee. Ukiangalia katika wakimbiaji 10 bora, 5 ni wakenya. Kwanini? Shida ipo kichwani mwa waTanzania na viongozi wao.

Tunalalamika ajira, wakati ajira hizp hapo. Kwanini serikali isiwekeze na kuhamasisha maendeleo endelevu ya michezo yote ambayo ni ajira tosha kwa vijana wetu. Serikali iwe na shule za michezo, au pengine iwape unafuu wawekezaji katika eneo la michezo wawekeze bila mikodi kwa kipindi maalumu.

Hapo Gaey atakaporudi, hizo pesa lazima serikali ikate kodi. Hebu fikiri kwenye mbio tu tungekuwa na akina Gaey 100 na bado michezo mingine, serikali wangekusanya kodi kiasi gani?

Wizara ya Michezo hebu amkeni bana msaidieni Rais wetu mpendwa kutunga sera nzuri kuendeleza michezo badala ya kumpa sifa zisizo na tija muonekane mnafanya kazi. Achaneni na maneno, mama mama kaahidi. Tungeni sera na mzisimamie tupate wanamichezo wengi walio bora, hebu ona sasa waKenya wamepata 5 kati ya 10 wakati sisi ni 1 kati ya 10. Huoni kuna shida mahali? Kuna shida katika sera tangu enzi na enzi za uongozi kwa hiyo kipindi cha mama, sasa kwa vile ameonesha utashi kuinua michezo lishughulikiwe na wizara husika.

Rais Samia limulike hili la sera ya michezo, najua unautashi kuona tunapiga hatua. Ni fursa na ajira kwa vijana wengi
 
Punguza siasa. Riadha ni kipaji na sio utasema kwamba kwasababu tuko 60m ndo tutapata wanariadha kirahisi. Ingekuwa rahisi kwenye hizo mbio ungeona USA wametawala kwasababu hela wanazo na pia idadi ya watu ni wengi. Au ungeona hata Nigeria wametawala hapo. Mashindano kama ya Boston Marathon yanahusisha vile vipaji vya hali ya juu kabisa kwenye riadha yaani ile top layer kabisa. Hapo world record holder Kipchoge alikuwa wa 6. Kimsingi hapo ni vipaji vitupu. Kwa rekodi alizoweka Geay inaweza kuchukua hata miaka 40 kutokea mtanzania mwingine wa kuzifikia.
 
Mtanzania Gabriel Geay, ameweka historia kwa kushika nafasi ya pili katika mbio za Boston (Boston Marathon) zilizofanyika kwa mara ya 127 mwaka huu huko Boston, Marekani

Geay alifanikiwa kumaliza mbio baada ya saa 2:06:04 akimaliza nyuma ya kinara, Evans Chebet kutoka Kenya aliyekimbia mbio hizo kwa saa 2:05:54

Evan amefanikiwa kutetea taji hilo mbele ya Eliud Kipchoge (KEN) anayeshikilia rekodi ya dunia katika riadha. Kipchonge ameshika nafasi ya sita katika mbio hizo

View attachment 2591321

View attachment 2591311

Na hizi ndio zawadi wanazopatiwa Washindi katika mbio hizo
View attachment 2591312
Wakenya wameshaanza nye nye nye huko[emoji1]

Wanasema huyu ni Mkikuyu aliyezamia TZ....
 
Safi sana,tunataka kuona watu,wanamichezo aina hii
Wanaoitangaza nchi...
Achana na wale wakata mauno

Ova
 
Bora umemjibu huyo jamaa maana anajua kabisa kuwa nimekosea Ila ni vile Tu ujuaji mwingi
Ntajuaje kuwa umekosea? Unahisi kila mtu anajua kila kitu? Huoni hata aliyenijibu kaandika kuwa anahisi?
 
Back
Top Bottom