Mtanzania ataka kuinunua LIVERPOOL!

Mtanzania ataka kuinunua LIVERPOOL!

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Posts
16,508
Reaction score
11,897
Mtanzania Suleiman Nassoro ametangaza nia yake ya kuinunua klabu maarufu ya liverpool.SWALI Je ni kweli huyu bwana mfanyabiashara ana uwezo wa fedha za kuinunua hiyo klabu au ni kutaka umaarufu?ni kiwaza wazazi mwananyamala hospital wanalala watatu kitanda kimoja siamini kama kuna mtanzania wa kununua klabu UK.source TBC1
 
na mimi nimemuona ITV lakini ni njaa anataka kutafuta jina na umaarufu hakuna kitu pale
 
Wakuu kwa nini hamuamini kwamba kuna Watanzania wenye uwezo huo? Wapo Watanzania kadhaa (wengi kuliko uzaniavyo) ambao ni matajiri wakubwa (tena siyo mafisadi). Ni kwamba tu kwa nchi kama za kwetu kujua income ya mfanyabiashara au kampuni fulani ni vigumu sana. Ila matajiri wapo sema kama haupo ndani ya circle za watu hao ni vigumu kujua.
 
Miafrika ndivyo tulivyo,tu mijitu ya hovyo,jitu linaaga nyumbani kwake eti linaenda kwenye kituo cha televisheni kutangaza nia ya kununua klabu cha uingereza ,hiyo tv haionekani hata kyela sembuse uk,
 
Mtanzania Suleiman Nassoro ametangaza nia yake ya kuinunua klabu maarufu ya liverpool.SWALI Je ni kweli huyu bwana mfanyabiashara ana uwezo wa fedha za kuinunua hiyo klabu au ni kutaka umaarufu?ni kiwaza wazazi mwananyamala hospital wanalala watatu kitanda kimoja siamini kama kuna mtanzania wa kununua klabu UK.source TBC1

This is why we elect fools to lead us. The average Tanzanian will believe any rubbish even though it makes no sense whatsoever.
 
Lofa yeyote anaweza kutengeneza business plan, kukopa hela benki na kununua club. Hata Gillett and Tom Hicks ni malofa tu. Walikopa
 
Nadhani inawezekana ujue watz individually wana pesa bwana, mwacheni apeleke maombi linawezekana hilo!
 
This is why we elect fools to lead us. The average Tanzanian will believe any rubbish even though it makes no sense whatsoever.

Unachokikasirikia nini kwani amekupa bank statement yake ukaona haiwezekani?
 
Wakuu leo asubuhi nilikuwa natazama TBC1 kipindi cha jambo Tanzania,kipindi cha michezo TBC 1 walimhoji mtanzania mwenye asili ya kiarabu alikuwa anadai ametuma washauri wake UK kuangalia uwezekano wa kununua Liverpool.Bahati mbaya sikulishika jina lake lakini alikuwa akijitapa ana uwezo mkubwa fedha haijawahi kuwa tatizo kwake.

WaJF wa Dar mnamjua huyo jamaa ua ni manjonjo ya wazee wa mujini ?.
 
Anauza sura tu yule jamaa. Kwa mimi ndio kwanza naumuona
 
Anauza sura tu yule jamaa. Kwa mimi ndio kwanza naumuona

Unajua hata mimi nilibaki nashangaa kidogo sijawahi kumsikia akichangia hata Twiga stars nikahisi anatufunga kamba.
 
Jamani huyu ataifanya tanzania ikose misaada kwa hawa wazungu ! Si angesaidia kujenga zahanati na kutuletea vifaa vya kisasa mahospitalini?
 
Jamani huyu ataifanya tanzania ikose misaada kwa hawa wazungu ! Si angesaidia kujenga zahanati na kutuletea vifaa vya kisasa mahospitalini?

Umeniacha hoi mbavu sina.Mkuu vipi wewe ni mshauri wa Muungwana kwasababu anashindwa kulinda rasilimali zetu anatembeza bakuli kwa wazungu !!!!!!
 
Kweli yule bwana nilipomwona asubuh nikajiuliza maswali mengi pasipo majibu....Yaani dhairi anataka umaarufu tu..sasa akinunua liverpool tanzania itafaidika na nn?.Ila mdau hapo juu ni kweli usemayo kawaida charity starts at om sasa hata kuonesha mapenzi yake kwenye soka la bongo hatujamsikia..au ndo one of the friends of simba?!
 
Si mshauri wake but napata wasiwasi kwa utegemezi wa tz usio na kikomo TUKISUSIWA kwa kununa team za mpira si wa tz hawataona hata kidonge kimoja kwa hospiatal
 
wabongo title kubwa lakini hawana kitu,kweli hizi ni nyeti
 
Jamani imetamkwa kuwa ni mtanzania mwenye asili ya arabuni hivyo inawezekana uwezo anao na anataka kuwekeza kwenye timu hiyo kwa kuwa yeye ni mfanya biashara na ameona hiyo ndio nafasi yake katika biashara zake hivyo sioni kama kuna tatizo.
Tujiulize,ni watu wangapi matajiri hapa Tanzania hutoa misaada kwa jamii?Inawezekana kabisa kuwa anatoa misaada ila haitangazwi katika vyombo vya habari na ndio maana kuonekana katika luninga imekuwa ni jambo la kushangaza kwa kuwa tumezoea kuona watu ambao tunadhani ni matajiri wakitangazwa kufanya hili na lile.
Tusubiri tuone matokeo yake,Tanzania pesa ipo.
 
Wabongo bwana kwa kuzarauliana!!, mko juuuuu mno. Kama angekuwa mchina au mkenya ndo anataka kuinunua liverpool wala msingechonga. Kweli nabii hakubaliki kwao!!!, nimeamini sasa. Badala ya kupongeza mnaanza kuingiza siasa, ndo hatuendelei.
 
Back
Top Bottom