Mtanzania ataka kuinunua LIVERPOOL!

Mtanzania ataka kuinunua LIVERPOOL!

Liverpool imeshanunuliwa mstake kuchekesha watu hapa..na mnunuzi wa ukweli hafanyikazi kwenye magazeti au kwene tv..he simply goes for it..acheni komedi zenu ..mtachekwa.
 
Mods, hii thread ishaletwa hapa jamvini jana, ziunganisheni!
 
Wakati mwingine huwa nashindwa kujua kwa nini watanzania wana 'wivu wa kike' (Mkapa)!! Jamaa kajieleza vizuri kwamba yeye na wanafamilia wenzake wameamua kuingia katika mchakato wa kuinunua club ya Liverpool. Na kaeleza biashara anazofanya yeye na familia yake ambapo sehemu ya biashara hizo ni visima vya mafuta vilivyopo uarabuni vinavyoendeshwa na familia yake.

Tatizo lenu ni nini? Huyu ni mfanyabiashara na anaongozwa na kitu kinaitwa NPV (net present value) katika maamuzi ya kibiashara. Kwani wapi imeandikwa kwamba ukiwa tajiri au mfanyabiashara mkubwa uwe unachangia Taifa stars au Twiga stars? Kwani ni lazima ugombee ubunge au uwe treasurer wa CCM?

Acheni hizo jamani, hizo ni fikra za kimasikini na kukatishana tamaa ambako hakuna mantiki. Angalieni jinsi Bilionea wa kirusi anavyoendesha mambo yake pale Chersea........mbona yeye ana prefer zaidi kutoonekana ovyo ovyo kwenye ma TV?

Nakumbuka miaka ya 60 wakati Nyerere akiwa Rais....aliwahi kuambiwa katika moja ya safari zake za Uk, kwamba afikie kwenye Hotel inayomilikiwa na Mtanzania (Ndesamburo). Kuna mijitu ikaongea hivi hivi.....kwamba oohh hio utakuwa mgahawa na si hotel!!

Watanzania acheni wivu wa kike....kama wewe huna hela au ni masikini usifikiri watanzania wote ni masikini!!

Disclaimer: To all women, samahani kwa kutumia neno "wivu wa kike" no offence is intendend.
 
Kweli yule bwana nilipomwona asubuh nikajiuliza maswali mengi pasipo majibu....Yaani dhairi anataka umaarufu tu..sasa akinunua liverpool tanzania itafaidika na nn?.Ila mdau hapo juu ni kweli usemayo kawaida charity starts at om sasa hata kuonesha mapenzi yake kwenye soka la bongo hatujamsikia..au ndo one of the friends of simba?!

Hivi kumbe Yule aliyenunua man u Naye alianza kusaidia time za Kwao marekani eeeh
 
nimefikiria kwa undani kuhusu suala hili lakini nikasema pengine atanunua timu tusimdharau,wakati mwingine nilidhani labda anatafuta umaarufu lakin sina uhakika sasa nimeamua kuacha then nione mwisho wake atanunua au atarudi na jibu gani? yangu macho
 
Wabongo bwana kwa kuzarauliana!!, mko juuuuu mno. Kama angekuwa mchina au mkenya ndo anataka kuinunua liverpool wala msingechonga. Kweli nabii hakubaliki kwao!!!, nimeamini sasa. Badala ya kupongeza mnaanza kuingiza siasa, ndo hatuendelei.
hapana sio wote tunaomdharau,la!,ila napenda niseme hivi,kwanini asingejitolea hata kusaidia watanzania maskini hususan kule vijijini wasio na uhakika wa hata mlo 1kwa siku,madawa hospitalini,huduma za jamii kwa kufikia walengwa moja kwa moja kwa hela hizo anazotaka kununua liverpool kwanza kabla ya yote?hata Abramovich anasaidia sana ktk kuinua uchumi wa Russia uliosambaratika hasa baada ya kuvunjiva kwa muungano wa nchi za kisovieti,aanzie kwanza nyumbani akionyesha uzalendo,au la sivyo hakuwa na haja ya kujitangaza yeye ni mtz ile hali hasaidii ktk kutaka kuinua tz
 
Miafrika ndivyo tulivyo,tu mijitu ya hovyo,jitu linaaga nyumbani kwake eti linaenda kwenye kituo cha televisheni kutangaza nia ya kununua klabu cha uingereza ,hiyo tv haionekani hata kyela sembuse uk,
Mkuu you have made my day

ni kichekesho kikubwa aisee, hata kama kweli alikua na nia ndio aende TBC1... kitendo cha TBC kumpa airtime tu ni ishara tosha ya nini tunacho pale TBC... huyo jamaa si angeanza kusaidia maskini hapa bongo??

ameshamaliza kuwachangia akina JK na CCM pesa ya mabango?
 
Ningependa kujua habari za tajiri mbongo anayewazia kuichukua Liverpool. nani ana details kidogo juu ya jambo hilo kama kweli lipo na huyo mtu kweli yupo!
 
thread hii ipo, na imeanzishwa leoleo na MwanaArusha namba MOJA, na mwana TLP wa Ukweli, anayekwenda kwa jina la NGONGO!..tafuta uone!
 
Anaweza kuwa ni mtanzania kwa maana anayo pass ya kusafiria ya TZ na huku akiwa ni Mturuki au Mjordan,hili lipo. Na anaweza pia kuwa ni Mtanzania halisi mwenye asili ya Asia na ni tajiri haswa kwa fweza na rasilimali,na kutokana na kutokuwa wawazi ktk biashara zetu, na wengi wa matajiri wakubwa ndo wakwepa kodi wakubwa,basi huyu jamaa anaweza kuwa na uwezo wa kuinunua Liverpool na tusidharau wala kushangaa.

Kwamba hajawahi kuchangia Twiga stars au huduma ya jamii,hiyo siyo ishu kwa vile kila mtu anafanya jambo kwa interest zake,hivyo tusubiri tuone japo kuna habari kuwa timu imeshanunuliwa tayari.
 
Tatizo ni yeye kwenda TBC nadhani ingekuwa poa zaidi kama habari hii angeitolea kwenye TV stations kubwa duniani maana Liverpool sio Kagera Sugar au Manyema....
 
Hata angekuwa tajiri wa kwanza dunia bado wasingemuuzia,hizo ndio hathari za kutoka nchi maskini.
 
alikuwa anasubiri inunuliwe kwanza............is it
 
Lofa yeyote anaweza kutengeneza business plan, kukopa hela benki na kununua club. Hata Gillett and Tom Hicks ni malofa tu. Walikopa
Tom Hicks ana worth $ 1 billion kwa mujibu wa Forbes Magazine ya 2009, na mwenzake Gillett ana biashara kadhaa na shares kwenye kampuni kadhaa zinazomuingizia million kadhaa.

Hivi kumbe Yule aliyenunua man u Naye alianza kusaidia time za Kwao marekani eeeh
Owner wa Man Utd ana miliki Tampa Bay Buccaneers.

Huyo jamaa alikuwa wapi siku zote kubid amesubiri mpaka wamejitokeza wanunuzi waliopitishwa na board ndio anajitokeza. anataka limelight tu hakuwa serious.
 
Huyo jamaa alikuwa wapi siku zote kubid amesubiri mpaka wamejitokeza wanunuzi waliopitishwa na board ndio anajitokeza. anataka limelight tu hakuwa serious.

Spot on.
Nina mashaka pia na elimu yake na kama anafuatilia mambo ..
 
Walio angalia Habari,

je Huyo Nassoro ni Nassoro wa SuperDoll au ni mwingine ?

B.P (2010)
 
Kama Tanzania **** matajiri kama hao, itakuwa vigumu kwa mh kwenda kuomba msaada. Naona anatka kuaribu deal za viongozi kwenda kuoba misaada nchi za nje!
 
Back
Top Bottom