TANZIA Mtanzania auliwa kwa kupigwa risasi Marekani, anaitwa RODGERS KYARUZI, alipata maluweluwe

Discrimination ipo sana USA kwenye mighahawa ikiwa wewe sio mzungu Kuna sehemu ukienda unaweza ambiwa all table has been reserved yaani inauma sana kisa wewe ni black, coloured au Asian #Americawillfall

Mimi napenda sana watu wabaguzi, Wazungu ni lazima wajilinde dhidi ya inferior cultures kama zetu, wasipofanya hivyo watakuja kuongozwa na akina Nape au Makamba.

Nchi kama Japan wakiruhusu inferior cultures wamekwisha, Japan ni tajiri sababu no immigration from third World!
 
Dah, sijawahi kusikia nchi za Kiarabu wanawaua watu kwa kuomba omba, tena ndio wanapenda kweli kusaidia waombao.
🙆🏿‍♂️🙆🏿‍♂️ Husika malalamiko ya dada wa kiafrika Mateso wanafanyiwa huko kwa waarabu ?
 
Naona ajenda ya mleta mada ilikuwa haijaeleweka.
Mkaenda kule asipotarajia.

Nilitaka kushangaa 'huyu Mtu' leo kuonea huruma 'marehemu wa race' yetu tena asiye wa itikadi yake na mbaya zaidi tukio lifanywe kwa hao Wazungu kwenye hilo Taifa kubwa!
 
Kifo huwa ni cha kijinga kweli,iki kiweze kuchomoka na wewe lazima kikutafutie sababu tu.
 
Anaandika MC Baraka Galiatano From Face Book Nime Copy na Ku Paste Kama Ilivyo

[emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484]

TANZIA :Wandugu wanajumuiya wa Tanzanite Community of Georgia, TCG.

Kwa taarifa zinazoendelea kwenye mitandao ya jamii hasa pia kwenye vyombo vya habari na vyombo vya dola, tunasikitika kutoa taarifa hizi za Mtanzania mwenzetu Ndugu Rogers kututoka gafla!!

Uongozi wetu umepata fursa ya kuongea na Mama mzazi wa Rogers, Mama Rose Yorke.
Kama jumuiya, Tunasikitika kuwatangazia kifo cha mwenzetu Rogers Kyaruzi Mtanzania mwenzetu na maisha yake kwa ufupi aliyoyaishi hapa Georgia USA:

~ Rogers alikuwa mtoto pekee wa kiume akiwa na umri 30, kati ya watoto watano kwenye familia yao, ameacha dada, Myra na wadogo zake wakike watatu (Agness, Maya, na Miya).

~ Rogers na mama yake walikuja hapa USA mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 10, waliishi Warner Robins GA.

~ Baada ya masomo yake ya juu; (major in Computer Networking) alifanikiwa kuoa Bi. Niteecha, ambapo walipata mtoto mmoja wa kiume (Raja, 5 yrs). Huku wakiishi Ellenwood GA na familia yake.

~Rogers alikuwa mjasiliamali ambapo alikuwa mtu wa maendeleo, aliwekeza kwenye biashara mbalimbali ikiwa pamoja na kumiliki mtandao (website) binafsi na kupata mafanikio makubwa.

~ Rogers alikuwa na rafiki yake wa karibu tokea utotoni alipofika hapa USA, huyu rafiki nae mwezi uliopita alitangulia mbele za haki jambo ambalo lilimuacha na huzuni kubwa.

~ Jumatatu ya tarehe 2 May hadi asubuhi ya Jumatano 4 May mwaka huu, Rogers alikuwa kwa mama yake Warner Robins GA, ambapo alikwenda kumtembelea.

~ Siku ya tukio, Rogers alikuwa ana appointment Apple store, Lenox Mall, karibu na eneo la tukio. Muda mfupi kabla ya tukio Rogers aliongea na mama yake na kusema, “Mama kila nikiingia kwenye gari namuona rafiki yangu aliyefariki amekaa pembeni yangu Mama, Mama naogopa, pls njoo unifate
Mama kwa kuwa anakaa mbali na Buckhead akampigia mke wa Rogers ili awahi aende kumchukua.

~ Mke wa Rogers kufika kwenye tukio, alikuta Paramedic wanatoa huduma ya kwanza, ambapo Rogers aliweza kumuangalia mkewe machoni ingawa hawakumruhusu, baadae hospitalini aliripotiwa kaaga dunia!!!!

~ Kwa habari za vyombo vya dola na Mama mzazi, ni kuwa uchunguzi unafanyika na majibu yatatolewa ndani ya siku tano!!

~ Wakati familia ikisubiria taarifa rasmi ya kitengo cha upelekezi hapa Jimboni Georgia, GBI. Familia imepanga mazishi kufanyika hapa GA, Warner Robins.
Taarifa kamili juu ya Safari ya mwisho Kwa mpendwa wetu itatolewa baadae!

~ Kama watanzania, tunaomba tuendelee kuiweka kwenye maombi yetu ya kila siku familia hii hasa kwenye kipindi hiki kigumu wanayopitia.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.[emoji1374][emoji1374][emoji1374][emoji1374][emoji1374]

Peter Okungu, TCG - President.
 
Mbona jamaa yupo active?
Oyaaa DIBAJI acha itikadi za Ugumu wangu
 
Sasa mambo gani ya kujidhalilisha hayo kwenda kuombaomba watu huko kwenye hoteli? Mtu unasikia fulani yupo marekani kumbe ndio maisha yao hayo.duuh poleni mnaopenda kwenda kuishi huko.

Kwani huku hawauliwi??

Poli-ccm wanaua raia kila siku
 
Hawa jamaa weusi wenzetu wa US hivi kwa nini polisi akiwasimamisha, wanakimbia? Wengine wanapigana mieleka na polisi! Wengine wananyang'anyana bunduki na polisi! Hivi kwa nini? Nashangaa kwa nini huwa wataki kwenda kituoni ama mahakamani na kujitetea huko?
 
Vijana wa kihaya huwa bia haiwakubali, wakinywa huchanganyikiwa, ndivyo walivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…