Mtanzania: Dr. Slaa atajwa kumtuma Ben Saanane kummaliza Zitto

Status
Not open for further replies.

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
*Yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini
*Mwenyewe akanusha, asema ni siasa chafu


TISHIO la kuuawa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, sasa limechukua sura mpya, baada ya kuibuika kwa madai mapya kuwa Bosi wake, Dk. Willbrod Slaa, alipanga njama za kumuangamiza, MTANZANIA Jumatano linaripoti.

Duru za habari zinaeleza kuwa Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni, anadaiwa alitaka kuuawa kwa sumu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Slaa, ambaye alimtumia kada na Mjumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Ben Saanane, kutekeleza mpango huo.

Habari zinadai kuwa tukio hilo lilipangwa kutekelezwa Mei mwaka jana, katika Hoteli ya Lunch Time, iliyoko Mabibo External, jijini Dar es Salaam.

Kwamba Zitto alilengwa kuuawa kwa kuwekewa sumu kwenye kinywaji chake wakati akiwa kwenye mazungumzo na baadhi ya makada vijana wa chama hicho katika Hoteli ya Lunch Time.

Mmoja wa watu waliokuwa katika tukio hilo amelieleza MTANZANIA Jumatano kuwa Zitto alinusurika baada ya aliyetumwa kumuwekea sumu hiyo kuidondosha na hivyo kuonekana kwa watu waliokuwa eneo hilo.

Anamtaja mtu aliyetumwa kumuua Zitto kuwa ni Ben Saanane, ambaye aliangusha karatasi ya nailoni iliyokuwa na ungaunga unaosadikiwa kuwa sumu na kuonekana kwa watu waliokuwa eneo hilo, akiwemo Zitto mwenyewe pamoja na aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano, Shonza alikiri kutokea kwa tukio hilo kwa kueleza kuwa yeye na Mwampamba walihoji kilichokuwa ndani ya nailoni ile, ambacho kilionekana wazi kuwa ni unga unga ni nini, ambapo Saanane alikiri kuwa ilikuwa sumu ambayo alipewa na Dk. Slaa, ili amuwekee Zitto.

Shonza alidai kuwa siku ya tukio, yeye na Zitto walikuwa wamekaa meza moja na Saanane ambaye mkono wake wa kushoto ulikuwa umefungwa bandeji aliyowaeleza kuwa aliifunga kutokana na maumivu ya mkono.

Alisema wakiwa katika maongezi, huku Saanane akionyesha kuzidiwa na kilevi alichokuwa amekunywa, alitoa bahasha ya kaki yenye fedha ili alipie gharama za vinywaji vya wote ambayo ilidondoka na ndani yake ikatoka karatasi ndogo ya nailoni ikiwa na unga mwekundu.

Kwa mujibu wa Shonza, Saanane alipobanwa aeleze unga ule ulikuwa nini, awali alidai ni kilevi aina ya kuberi, huku akiwataka wasiifungue nailoni hiyo, jambo ambalo Mwampamba alilikataa na kulazimisha ifunguliwe pale pale.

"Kwa hasira Ben alitaka arudishiwe ile karatasi, lakini, Mwampamba aliondoka nayo, usiku huo huo Saanane alimtafuta Mwampamba hadi nyumbani kwake akidai apewe mzigo wake.

"Mwampamba alimwambia atampa mzigo wake kwa sharti moja tu la kusema ukweli kuhusu kilichomo ndani ya nailoni hiyo na hapo ndipo Ben alipokiri kuwa alipewa mzigo huo ambao una unga unga wenye sumu na Dk. Slaa, ili amuwekee Zitto kwa sababu amekuwa akimsakama ndani ya vikao vya chama.

"Huo ndiyo ukweli ambao nitausema popote, sasa kama Ben alitudanganya kwa kumsingizia Dk. Slaa hiyo ni juu yao wenyewe," alisema Shonza.

Shonza alisema hali hiyo iliwaogofya na kuanza kuwa makini katika mapito yao na kuongeza kuwa Zitto bado yuko CHADEMA kwa sababu ana roho ngumu, mvumilivu na mkomavu wa kisiasa, anayeweza kukabiliana na mambo ya hatari.

Dk. Slaa alipoulizwa na MTANZANIA Jumatano kuhusu madai hayo, alisema hilo ni kosa la jinai, ambalo kama anatuhumiwa kulifanya anapaswa kushtakiwa kwenye vyombo vya dola badala ya tarifa hizo kupelekwa katika vyombo vya habari.

"Usipende kutumiwa na watu, lakini aliyekutuma anajua amekutuma kwa sababu gani. Sasa nitakujibu, hivi suala la kuua si ni jinai? Sasa suala la jinai linapelekwa kwenye vyombo vya dola au kwenye vyombo vya habari? Huyo aliyesema yuko CHADEMA au yuko wapi? Aliyesema hakwenda polisi? Aliyetaka kuuawa hakwenda pia? Sasa ninyi media mmekuwa nani?

"Wa kumuuliza suala hili ni Saanane mwenyewe au Shonza, wangekuwa na nia njema wangekwenda polisi au Zitto mwenyewe angekwenda polisi kushitaki kwa kutaka kuuawa," alisema Dk. Slaa.

Naye Saanane ambaye amefanya mahojiano na MTANZANIA Jumatano kuhusiana na mambo mbalimbali mabaya ambayo yamekuwa yakielekezwa kwake, akizungumzia madai hayo alisema madai hayo hayana ukweli wowote, bali yanaibuliwa sasa na mahasimu wake kisiasa kwa lengo la kutaka kumshusha baada ya majaribio mengi dhidi yake kushindwa.

"Kwanza siku ambayo wanasema tulikuwa wote mimi sikuwa huko, nashangaa na haiingii akilini kwamba mimi niende hadi Temeke (kwa Mwampamba) tena usiku wa manane kwa ajili ya kufuata sumu ya kuulia panya.

"Hizi ndizo siasa halisi za maji taka, kuliko nipange njama za kuua mtu kwa malengo ya kisiasa, ni bora niache siasa. Ni mwendawazimu pekee atakayeweza kuamini tetesi hizi za ovyo kabisa zinazofanywa na vijana walioshindwa kujenga hoja za maana kwenye majukwaa," alisema Saanane.

Aliwaonya watu wanaohasimiana naye kisiasa kuacha kumchafua Dk. Slaa kwa kutumia jina lake katika mambo wanayomtuhumu, kwa kile alichoeleza kuwa ni dhambi kubwa kutunga uongo na kuusambaza ili kutafuta huruma ya umma wa Watanzania.

"Nadhani lengo lao hapa ni kumchafua Dk. Slaa kwa tuhuma hizi za uongo zilizotolewa kwa mara ya kwanza na vijana waliotimuliwa Chadema kwa kukisaliti chama na baadaye kuhongwa na makada na viongozi wa CCM ambao wamejiunga nao sasa.

"Sasa kwa tuhuma hizo, kwanini wasiripoti polisi, inaingiaje akilini mtu kupanga njama kubwa kiasi hicho halafu ukae kimya tu," alisema Saanane.


CHANZO: MTANZANIA

MY TAKE:
GAZETI HILI LINATUMIWA KUIHUJUMU CHADEMA?

HIVI WAANDISHI WA HABARI SIO KWELI WANANUNULIWA?
 
Dr. Slaa apange kumuua Zitto kwa faida ya nani? By ze way kumbe chanzo ni Mtanzania ..........................
 
Mkuu Ben Saanane wameanza huku.....nakumbuka hili


 
hii singo ilishachuja mda and only masalia can do that.
 
Kumbe habari yenye chanzo ni masalia, nasikitika kupoteza muda kusoma upuuzi huu ambao uliishapitwa na wakati siku nyingi
 
Dr. Slaa apange kumuua Zitto kwa faida ya nani? By ze way kumbe chanzo ni Mtanzania ..........................

Nipo kwenye makutano ya barabara ya Samora na Mkwepu hapa posta, kuna wauza magazeti wawili wako opposite. Nimekuta gazeti la Mtanzania linanunuliwa lakini kila anayeulizia na kulinunua anahusisha hiyo habari na vita ya Bavicha pamoja na jinsi Ben Saanane alivyowasambaratisha wanafiq wa Bavicha
 
Last edited by a moderator:
Nishahisi kwa nini Kibanda kafanyiwa umafia.
1. "Walimuiba" Tanzania Daima kwa hela nono.
2. Alipokuwa Mtanzania, Gazeti hilo lilibadilika ghafla likawa linaandika habari ambazo ni "sumu" kwa CCM na serikali.
3. Haikuchukua muda wamemmafia na sasa habari kama hizi za masalia zinapewa coverage.
4. Zitto stuka, kwa nini CCM waonekane wanakupenda kwa kiwango hicho ilhali wewe ni mpinzani??
 
Hakuna cha gazeti la Mtanzania kuwa linatumiwa, huo ndio ukweli wenyewe. Hata huyo mchumba wa Slaa kuna thread alichangia kuhusu Zitto na Saanane, nadhani waliofikiri zaidi kwenye ile post walimuelewa alimaanisha nini.
 
Siasa za bongo bana!
CHADEMA ni Chama Makini sio magamba haya CCM mnalengo la kutumia umri mdogo wa Zito na Ukongwe wa Slaa kuwamaliza Chadema tehe tehe tehe...Sifa kubwa za Zitto ni ukomavu wake wa kisiasa unaowafanya Magamba watake kumwangamiza kwa kumtoa baharini ili afie nchi kavu, kimsingi Kisiasa zito ni Mkongwe kuliko kina Jakaya Kikwete,Membe na wengine wote CCM..Slaa ni Mti Mkavu usiotikisika kwa hila zozote kuanzia kidini kisiasa na kikabila..Anastahimili hayo ambayo JK na wengine CCM hawana uwezo huo
 
Napendekeza kichwa kingekuwa "Masalia Waendelea kuiota chadema" Gazeti lingeuza zaidi. Hawa sasa ni makada wa magamba, mbona kila kukicha wanaiota cdm? au ni kweli walitumwa????
 
Kama habari hii ni kweli, saa 8 akamatwe kwa "attempted murder" ushahidi unatosha maana amekiri mwenyewe.
 
tumeshachoka na hii kitu, kila siku zitto zitto.
 
Hii habari ni zilipendwa humu inakuwaje habari leo? Huyu muandishi ndio wale wale alafu baadae atakuja humu kutafuta huruma mambo yakienda kombo! Watu mna familia zenu tena maskini alafu mnatumika kijinga jinga badala ya kuheshimu taaluma yenu.

Hivi kweli hata uwe kichaa mtu kama Ben Saanane bila kuteswa wala kubanwa na Polisi au basi kuhongwa akubali huu unga nimepewa na Dr Slaa nikamuue Zitto? Alafu uzushi uzushi unavyozidi kuwa mwingi kuna watu na akili zao wanaanza kuaminiamini baadhi ya mambo dhidi ya Dr Slaa!!!

Dr Slaa binafsi natambua changamoto unazozikabili kwa nia yako njema ya kutetea wanyonge,pamoja na mapungufu kama binadamu lakini umejaribu kufanya mengi yaliyowashinda wengine kwa miaka mingi hadi kuifikisha CCM ilipo pamoja na msaada wa wapiganaji kibao lakini wewe ukitangulia kama ngao na ndio maana risasi zote za maadui lazima ianze na wewe!!

Bado tunaamini dhamira yako safi pamoja na kusakamwa kila kukicha!
 
Kweli Mtanzania ni Gazeti Uchwara ! Habari hii si ilishafungwa humu zaidi ya miezi mitatu iliyopita ?
 
Hii biashara ya kuibua story fake ili kuuza magazeti mengi Tanzania sasa naona inavuka mipaka. Gazeti linawalipa watu ili kutengeneza story ambayo itauza magazeti kwa wingi kabla watu hawajaishtukia. Ila hawajui kutengeneza tuhuma zinazofanana na za watu walioenda shule kidogo, hizi ni za watu ambao hawajasoma kabisa. Hata bibi yangu hapa kijijini amewacheka sana.
 
Huyu Juliana Shonza toka arudi CCM hana lingine bali kujaribu kuinanga CHADEMA....nadhani hata katiba, manifesto na nyaraka nyingine za CCM hata hajajipa muda kuzisoma
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…