DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sasa MD2 na hoja yake vinaingilianaje..?
Kwanza mental issues zamani tulikuwa tunasoma MD4 wengine MD5 sijui kwa sasa. Anyways, kubali kutokukubaliana bila kuvunjiana heshima.
Yeye ni kama anaongelea bioethics, huja soma comments zake za nyumba ni kama anataka kuprove kua anajua ethics
 
Yeye ni kama anaongelea bioethics, huja soma comments zake za nyumba ni kama anataka kuprove kua anajua ethics
Nadhani ni vyema mnge focus na swala la kwamba huyo dada ni kweli huu ndo msaada wa kweli aliostahili kuupata kutoka kwa huyo jamaa na mke wake au hii pia haijakaa sawa. Na kama haijakaa sawa, tuunganishe nguvu na mawazo ya namna bora ya kumsaidia. I am sure the thread writer is flexible to learn and help better.
 
Umejuaje ana matatizo ya akili?

Kama anadhani ana matatizo ya akili kwanini asipige simu ‘mental health unit’ wamchukue bure kwa matibabu aihitaji kudhalilishwa.

Hii ndio shida yetu watanzania mtu akianza na leading statement we automatically take that viewpoint as undisputed fact, wakati mleta mada hajui ata jina la ubini wa huyo dada wala background story yake zaidi ya kutengeneza narrative yake based on is own interpretation of her situation.
Nanukuu::
"Umejuaje ana matatizo ya akili?"
Mkuu; kama sikosei (samahani lakini)swali kama hili mara nyingi huwa ni swali la ki-Polisi. (Maafisa-polisi mliopo hapa pia naomba samahani)
Lakini katika hali ya kawaida, hata huku kijijini mtu akipatwa na Tatizo la akili haihitajiki kutafuta jibu la swali eti Umejuaje ana matatizo ya akili?. Watu wanakijiji kwa busara zao (common sense) humtambua wanachukua hatua ya humdhibiti kwanza kwa kumfunga kamba ili asijidhuru mwenyewe au asidhuru wengine na mali zilizopo. Ww mkuu, unaulizaje swali kama hilo nukuu hapo juu?? Ina maana hata ikatokea mmoja wapo ktk familia yako akipatwa na tatizo kama hilo kweli hutajua? Sasa wewe mbona unamwuliza mtoa dokezo kwamba Umejuaje ana matatizo ya akili? Wahenga walisema "Mwenye macho haambiwi tazama"
Hapo umetuwekea utaratibu wa kufuatwa ili anayedhaniwa ni mgonjwa wa akili apatiwe huduma.
Ina maana Ubolozi wetu haufahamu utaratibu huo? Lakini pia ukizingatia kwamba mtoa dokezo kuna shughuli ilompeleka hapo Marekani na sio kazi ya kufuatilia waTz wengine hapo USA esp. Afya zao. Hilo kalifanya on Charity basis tu.
Kazi ya kujaza hiyo Fomu na kutoa Location ya alipo mgonjwa ni 100% mojawapo ya kazi ya Ofisi ya Ubalozi wa Tz uliopo hapo Marekani.
Labda Ofisi ya Ubalozi ikatae kwamba hilo halimo kati ya majukumu yake au iseme haimjui mtu huyo au waseme huyo dada wanamfahamu ila sio mgonjwa wa Akili.
 
Wazungu wana msemo «Charity starts at home». Jee, hakuna umoja wa Watanzania huko Houston ambao wapo karibu zaidi naye wakafuatilia hadi kujua huyo dada ni nani na wakaweza kumsaidia? Unakimbilia ubalozini wkt mji mkubwa kama Houston kutakuwa na umoja wa Watanzania? Unajifanya unahangaika kumsaidia lkn hakuna lolote la maana unalofanya. Pumbaavu kabisa.
 
Hayo ndio matatizo ya kureua mabalizi bila kufata vigezzo, tayari umeshafanya msaada mkubwa.
Kwa sababu aliingia kihalali ni wazi kwenye passport Kuna sehemu ya ndugu au mtu wake wa karibu hii ni kufanya mawasiliano kupitia immigration ya huku pia kwa kutumia jumhiya ya watanzania waishio nje mnaweza kujipanga muwasaidie

Tunahitaji kuwaona upendo wao badala ya kupiga kelele wapewe haki ya uraia umefanya makubwa Mungy akybariki.
Kwanini tusitumia kigezo cha huyu dada kumfukuza kazi huyo balozi wa Tz nchini Marekani. Hawajali kabisa watanzania
 
Labda hawa wanaoenda ulaya siku hizi zama zetu tuko wachache ilikuwa mambo yakienda mrama utatia akili, kulała park ishawakuta watu wengi sana au kukaa ghetto watu wanapishana vitanda kwa kufanya kazi day and night shifts.

Sasa hivi ukiwaona hao watu wanapiga picha na ma-Range na mijengo yao Africa. Huyo hana support ya watanzania wenzake tu huko halipo Iła sio chizi.

Mpaka leo kuna waafrica na wahamiaji kibao wanalala nje kisa hawana makaratasi na awana ndugu.

Hakuna ushahidi wa huyo dada kuwa chizi zaidi ya kufanyiwa humiliation tu na huyo jamaa.

Yes alipofikia kama aiwezekani ana sababu ya kuwataarifu ndugu zake Jane anataabika kama wana namna ya kumshauri harudi nyumbani ningeelewa, lakini sio kwenda ku-record watu whilst condescending them on your video unataka kuwapa hela halafu unakwenda kurusha video mitandaoni that’s just humiliating her tena bila ya ridhaa yake, mwenyewe anakwambia sitaki niache uelewi.

Very bad
Me nakuelewa sana mkuu, tatizo ni kwamba naona enzi zetu sisi tukiwa tunabeba boksi Texas ni tofauti na enzi za hawa waliopo huko saivi. Wanashindwa kuelewa Dignity unayoiongelea.
 
Nadhani unafikiri ukionekana unachangia mambo ya Nje ya nchi utaonekana unajua kwanza toa maoni kiswahili tu kingereza ni lugha tu sio elimu hili neno privacy nadhani hata hujui maana yake au jinsi ya kulitumia nikujulishe Tena na watanzania kwa ujumla huyu dada Ana ugonjwa wa akili sisi Ndio tunamuona hakuna mgonjwa wa akili Unaweza kusema anamaamuzi pia usidhani wagojwa wa akili ni waiopo maporini tu kuna wengine humu kina privacy nao wanahitaji msaada 😂
Ukishakua na shida ambayo iko nje ya uwezo wako neno privacy halina maana tena

Neno privacy linamaana kama shida bado iko ndani ya uwezo wako
Kama unashida usione aibu kusema kwa watu ndo maisha
 
Ukishakua na shida ambayo iko nje ya uwezo wako neno privacy halina maana tena

Neno privacy linamaana kama shida bado iko ndani ya uwezo wako
Kama unashida usione aibu kusema kwa watu ndo maisha
Mngekuwa mnaletewa picha za ndugu zenu wakiwa ulaya pale wanapokutana na maswahibu, server za JF zisingetosha. The streets are very rough and hard especially kwa ambao hawana papers na hawana kazi.
 
Mngekuwa mnaletewa picha za ndugu zenu wakiwa ulaya pale wanapokutana na maswahibu, server za JF zisingetosha. The streets are very rough and hard especially kwa ambao hawana papers na hawana kazi.
Kama wanashida na wameletwa huku jf sio vibaya watakua wametusaidia sana kama ndugu

kwani hata sahivi kuna nyuzi nyingi tu zisizokua na kichwa wala miguu huku jf
 
Nanukuu::
"Umejuaje ana matatizo ya akili?"
Mkuu; kama sikosei (samahani lakini)swali kama hili mara nyingi huwa ni swali la ki-Polisi. (Maafisa-polisi mliopo hapa pia naomba samahani)
Lakini katika hali ya kawaida, hata huku kijijini mtu akipatwa na Tatizo la akili haihitajiki kutafuta jibu la swali eti Umejuaje ana matatizo ya akili?. Watu wanakijiji kwa busara zao (common sense) humtambua wanachukua hatua ya humdhibiti kwanza kwa kumfunga kamba ili asijidhuru mwenyewe au asidhuru wengine na mali zilizopo. Ww mkuu, unaulizaje swali kama hilo nukuu hapo juu?? Ina maana hata ikatokea mmoja wapo ktk familia yako akipatwa na tatizo kama hilo kweli hutajua? Sasa wewe mbona unamwuliza mtoa dokezo kwamba Umejuaje ana matatizo ya akili? Wahenga walisema "Mwenye macho haambiwi tazama"
Hapo umetuwekea utaratibu wa kufuatwa ili anayedhaniwa ni mgonjwa wa akili apatiwe huduma.
Ina maana Ubolozi wetu haufahamu utaratibu huo? Lakini pia ukizingatia kwamba mtoa dokezo kuna shughuli ilompeleka hapo Marekani na sio kazi ya kufuatilia waTz wengine hapo USA esp. Afya zao. Hilo kalifanya on Charity basis tu.
Kazi ya kujaza hiyo Fomu na kutoa Location ya alipo mgonjwa ni 100% mojawapo ya kazi ya Ofisi ya Ubalozi wa Tz uliopo hapo Marekani.
Labda Ofisi ya Ubalozi ikatae kwamba hilo halimo kati ya majukumu yake au iseme haimjui mtu huyo au waseme huyo dada wanamfahamu ila sio mgonjwa wa Akili.
Kinachoonekana hapo huyo dada ni homeless nothing else.

Huko sio Tanzania ukifikia hali hiyo ndugu mnatafutana kuokoa jahazi kwa kuogopa jamii itawasema mnashindwa kumsaidia ndugu yenu hana pakukaa.

Hizo nchi walipo diaspora ukikosea step unalo hilo ama uende ubalozini urudi mwenyewe, uende immigration zao uombe msaada wa kurudishwa kwenu au upambane unavyojua kitaa kama huna family and friend support network kama Jane.

Alipofikia Jane sio pazuri hilo halina ubishi but it none of everyone else business zaidi ya ndugu zake. Habari ingeweza letwa kwa njia nyingine bila ya kudhalilishana kuomba msaada wa kuwapata ndugu zake.
 
Kinachoonekana hapo huyo dada ni homeless.

Huko sio Tanzania ukifikia hali hiyo ndugu mnatafutana kumuokoa kwa kuogopa jamii itawasema mnashindwa kumsaidia ndugu yenu hana pakukaa.

Hizo nchi walipo diaspora ukikosea step unalo hilo ama uende ubalozini urudi mwenyewe au upambane unavyojua kitaa kama huna family and friend support network.

Alipofikia Jane sio pazuri hilo halina ubishi but it none of everyone else business zaidi ya ndugu zake. Habari ingeweza letwa kwa njia nyingine bila ya kudhalilishana.
Unafikiri kila mtu ana roho mbaya yako
Nyie ndo wale unamuona mwenzako anashida haumsaidii kwa kigezo cha unaheshimu privacy yake

Huna moyo wa kusaidia watu
 
Nikisema kuhusu balozi za Watanzania mnabisha hapo ni swala la siku moja tu hilo huyo dada yupo Tanzania ila Watanzania wakipata tu vyeo ni makatili kupita kiasi niliwahi kuambiwa na bwana mdogo mmoja Mnigeria kuhusu huyo dada sikuamini maana hakuna na picha aliniambia kuwa pana dada Mtanzania anapata tabu huko mtaani ninyi hamna msaada wowote...mkuu ukiweza wasiliana na Agent afanye hiyo kazi utapata dhawabu za kutosha sana inaumiza sana hasa kwa sisi wasafiri hatujui kesho yetu ipoje...
Mkuu umeongea kwa uchungu. lkn bongo hamnaga watu kuna sanamu tupu. Yani namaanisha kuna mifano ya watu hawana maarifa wala roho za kistaarabu
 
Mimi ni Mtanzania ninayeishi Marekani, kuna Mtanzania mwenzetu mbaye alikuja kama Mwanafunzi hapa, sijui vizuri kuhusu historia yake huko nyuma.

Miaka kadhaa iliyopita alipata changamoto ya Afya ya Akili, sijui nini kiliendelea baada ya hapo kati lakini kilichofuata amekuwa chizi na analala barabarani, amekuwa akifanyiwa ukatili wa kingono na Wanaume mara nyingi bila kuwa na msaada.

Nilienda Ubalozini mara kadha pia kuripoti ili ikiwezekana huyu Mtanzania asaidiwe lakini kinachoonekana wao (Ubalozi) ndio wanataka nianze kufanya kazi yao.

Wanataka kufuatilie na kujua details zaidi kuhusu huyo Mtanzania na mambo mengine kama hayo, mimi siwezi kuingilia hayo masuala ya wao, wenyewe ndio wataalam, mimi nikiwapa taarifa wanatakiwa kujua nini cha kufanya baada ya hapo.

Huyu mtanzania ninamfahamu kwa jina moja tu anaitwa Jane, mitaa ya Houston ndani ya Texas.

Maisha yake ni chini ya Daraja, amekuwa hivyohivyo akiishi chini ya Daraja.
View attachment 2995304
View attachment 2995860
Barua niliyowahi kuituma Ubalozini siku za nyuma​

Nilivyoanza kumjua
Kuna siku nikiwa na mke wangu kwenye bustani flani akasikia tunazungumza Kiswahili, akajumuika nasi na kuanza kuzungumza na kisha kujitambulisha.

Tukazungumza naye kwa Kiswahili na akajieleza naye anatoka Ukanda wa Kaskazini kama nilivyo mimi hapo nyumbani Tanzania.

Bahati mbaya nimesahau jina lake la pili na hata sas aukisema umuulie huwezi kupata jibu hilo.

Nimeshatoa picha zake mara kadhaa sehemu tofauti ili anayemjua iwe ni ndugu zake, jamaa au marafiki wamsaidie lakini sijafanikiwa katika hilo, ndio maana nimeona nitumie JamiiForums kufikisha ujumbe huu nadhani utawafikia wahusika na wanaweza kumsaidia.

Nipo tayari kuto ushirikiano kwa ambaye anaweza kuhitaji kumsaidia huyu au kama anawez kumtambua, nimewasilisha mawasiliano yangu kwa JamiiForums kwa mtu ambaye atahitaji kuwasiliana nami.
My village peole won it again.

#Hilinalomkalitizame.
 
Labda hawa wanaoenda ulaya siku hizi zama zetu tuko wachache ilikuwa mambo yakienda mrama utatia akili, kulała park ishawakuta watu wengi sana au kukaa ghetto watu wanapishana vitanda kwa kufanya kazi day and night shifts.

Sasa hivi ukiwaona hao watu wanapiga picha na ma-Range na mijengo yao Africa. Huyo hana support ya watanzania wenzake tu huko halipo Iła sio chizi.

Mpaka leo kuna waafrica na wahamiaji kibao wanalala nje kisa hawana makaratasi na awana ndugu.

Hakuna ushahidi wa huyo dada kuwa chizi zaidi ya kufanyiwa humiliation tu na huyo jamaa.

Yes alipofikia kama aiwezekani ana sababu ya kuwataarifu ndugu zake Jane anataabika kama wana namna ya kumshauri harudi nyumbani ningeelewa, lakini sio kwenda ku-record watu whilst condescending them on your video unataka kuwapa hela halafu unakwenda kurusha video mitandaoni that’s just humiliating her tena bila ya ridhaa yake, mwenyewe anakwambia sitaki niache uelewi.

Very bad
Mkuu; Niwajuavyo watanzania kwa kawaida wawapo nje ya nchi yetu(nina experiance ya 1yr in Denmark) wanaushirikiano sana. Sasa iweje huyo dada ameachwa bila msaada?
Mtoa dokezo amefanya (kama kweli unadhani ni udhalilishaji) kwa nia njema kabisa. Iko hv; yan kama mtu amekuwepo katika hali hiyo ya Ugonjwa (uchizi)kwa muda mrefu na hakuna anayejali ukizingatia Taratibu nyingi - rigorous and tedious activity in filling the Required Forms, angelifanyaje na roho inamuuma kwamba yan mTz mwenzangu anaendelea kutaabika kana kwamba hakuna waTz huku na hakuna anayemwona? Kama wapo na wanamwona ina maana wameridhika?
Mkuu kumbuka maradhi ya Akili huwa yana complications nyingi. Huku bongo tunasemaga mwezi mchanga, mwezi mpevu n.k. Ni mojawapo ya matatizo ya Akili na yanahusishwa na mambo mengi pia Biological na non biological.
Ni hoja ndefu tuache nafasi pia na wenzetu waweze kuchangia.
 
Kama wanashida na wameletwa huku jf sio vibaya watakua wametusaidia sana kama ndugu

kwani hata sahivi kuna nyuzi nyingi tu zisizokua na kichwa wala miguu huku jf
Hakuna utafutaji ambao hauna shida. Kila mtu anafurukuta mpaka anatoka kwenye hizo shida.
 
Back
Top Bottom