DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu umeongea kwa uchungu. lkn bongo hamnaga watu kuna sanamu tupu. Yani namaanisha kuna mifano ya watu hawana maarifa wala roho za kistaarabu
Yaani mtu hatoi pesa mfukoni ni swala la kumfatilia na kumrudisha Tanzania ndugu watapatikana tu ila sasa kwa roho za hao jamaa nao ndio kwanza wanasoma hizi taarifa kama wapo China...
 
Mtu anakwambia sitaki niache kwanini ulazimishe kumrekodi na kumpa msaada ambao hana shida nao?

Halafu unatoka hapo unaenda rusha maudhui mitandaoni na kumwita chizi? Hakuna tafsiri nyingine ya hiyo act zaidi ya udhalilishaji.

Give a dog a bad name and hang him. Ndio nilichokiona hapo.
Watanzania wanapikuwa nje ya nchi ni ndugu tofauti na makabila mengine kama wasauz, ukimkuta ndugu yako kavua nguo anakataa kuvaa huwezi mwacha utatafuta watu wakusaidie kumsitiri ndo alichofanya ndugu yetu, we msaidie hata kwa mawazo tu.
 
Balozi za kwetu ni za kipumbavu sana. Hazina msaada hata chembe kwa watanzania wenzao wenye shida. Mtu katoa taarifa na ameelekezwa jimbo alipo. Wanashindwa kutrack hadi wampate na kumrjesha nyumbani. Hawa watu ni qumer sijawahi kuona.
Mambo kama haya ndio ya kuandamana mpaka Bunge liongee
 
Yeye huyo aliyekaa nae hapo bustanini Texas kwann asimuhifadhi. Huku akisubiri msaada zaidi kwa ndugu husika? Au hujui nn namaanisha?
Siyo kama amekosa sehemu ya kukaa. Ni kichaa. Nadhani unajua changamoto za watu wenye ugonjwa wa akili. Wengi wanakimbia nyumbani. BTW kuishi na mtu mwenye ugonjwa wa akili kunahitaji uangalizi wa 24/7. Nani atafanya hiyo kazi wakati majuu unatoka asubuhi na kurudi jioni? Ukikuta amechoma nyumba moto? Au amejinyonga?
 
Tunaobakia Tanzania na kupambana na Hali zetu ( Shida ) huku tukisoma katika Vyuo Vikuu vyetu na Kula Maharage, Tembele na Dagaa huwa tunachekwa na kudharaulika mno na wale ambao huona Ulaya / Marekani ndiyo Pepo na Suluhu yao ya Maisha na Taaluma. Kudadadeki apambane na hali yake kama nasi tunavyopambana na hali zetu huku Madongo Kuinama Afrika.
Wewe ni mpumbavu sana. Ndiyo maana utaozea hapo Bongo kwa sababu mawazo yako ni kijinga. Unaonea wivu mpaka vichaa kwa sababu tu alisafari nje ya nchi? Unataka kila mtu akae Tanzania una kazi za kuwapa? Idiot!
 
Nikisema kuhusu balozi za Watanzania mnabisha hapo ni swala la siku moja tu hilo huyo dada yupo Tanzania ila Watanzania wakipata tu vyeo ni makatili kupita kiasi niliwahi kuambiwa na bwana mdogo mmoja Mnigeria kuhusu huyo dada sikuamini maana hakuna na picha aliniambia kuwa pana dada Mtanzania anapata tabu huko mtaani ninyi hamna msaada wowote...mkuu ukiweza wasiliana na Agent afanye hiyo kazi utapata dhawabu za kutosha sana inaumiza sana hasa kwa sisi wasafiri hatujui kesho yetu ipoje...
Kuna jinga moja linaitwa GENTAMYCINE linachekelea eti ni kwa nini alienda nje ya nchi. Hebu fikiri jitu kama hili likipewa madaraka litakuwaje!
 




Kitendo cha ku-post hiyo video, tena mwenyewe anamwambia niache sitaki; ame-violate kanuni kadhaa za afya na human rights naweza kukujazia uzi nikitaja zote.

Mambo mengine yanataka uelewa na experience ya maisha hayo mambo ni kawaida hata kwa wazungu wenyewe huko kwao kulała rough kipindi ambacho unashida na huna msaada.
Ficha upumbavu wako. Narudia: ficha upumbavu wako.
 
Kuna jamaa kipindi fulani huko majuu alichanganyikiwa hivyo hivyo kwa stress tu, akaonekana chizi watu tujiunge tumsaidie kumrudisha home. Huyu jamaa alikuwa 'kajilipua'/. Ebanee akaenda kusema kwa mamlaka kuna watu wanataka wamrudishe nyumbani kwa nguvu akauawe! Kuna watu walihama nyumba. Haya mambo sio rahisi kihivyo huko nje, kumrudisha mtu bila ridhaa yake sio kazi rahisi na ukisema ana matatizo ya akili kwa mujibu wa nani?
 
Siyo kama amekosa sehemu ya kukaa. Ni kichaa. Nadhani unajua changamoto za watu wenye ugonjwa wa akili. Wengi wanakimbia nyumbani. BTW kuishi na mtu mwenye ugonjwa wa akili kunahitaji uangalizi wa 24/7. Nani atafanya hiyo kazi wakati majuu unatoka asubuhi na kurudi jioni? Ukikuta amechoma nyumba moto? Au amejinyonga?
Huyo amesema hana Pa kuishi, na anaishi darajani au msituni.
Sasa wee hapo Pa kukaa aliponapo na unapajua ni wapiii?
 
Kuna jamaa kipindi fulani huko majuu alichanganyikiwa hivyo hivyo kwa stress tu, akaonekana chizi watu tujiunge tumsaidie kumrudisha home. Huyu jamaa alikuwa 'kajilipua'/. Ebanee akaenda kusema kwa mamlaka kuna watu wanataka wamrudishe nyumbani kwa nguvu akauawe! Kuna watu walihama nyumba. Haya ma mbo sio rahisi kihivyo huko nje, kumrudisha mtu bila ridhaa yake sio kazi rahisi na ukisema ana matatizo ya akili kwa mujibu wa nani?
Ubalozi au ndugu zake wanaweza kusikilizwa kuliko mtu baki tu. Ila kuna watu wanamshambulia mlete ''alert'' eti alitakiwa amchue aishi naye. Watu wanadhani mambo yanaenda kienyeji tu. Nakumbuka huko huko USA mama mmoja na mumewe walikuta na homeless mmoja wakaamua kumchukuwa na kumpa chumba cha kuishi kwenye makazi yao. Yaani alikuwa anapata kila kitu free kama mtoto wao. Pamoja na ukarimu wote akawavizia siku moja na kuwaua wote.
 
Mimi ni Mtanzania ninayeishi Marekani, kuna Mtanzania mwenzetu mbaye alikuja kama Mwanafunzi hapa, sijui vizuri kuhusu historia yake huko nyuma.

Miaka kadhaa iliyopita alipata changamoto ya Afya ya Akili, sijui nini kiliendelea baada ya hapo kati lakini kilichofuata amekuwa chizi na analala barabarani, amekuwa akifanyiwa ukatili wa kingono na Wanaume mara nyingi bila kuwa na msaada.

Nilienda Ubalozini mara kadha pia kuripoti ili ikiwezekana huyu Mtanzania asaidiwe lakini kinachoonekana wao (Ubalozi) ndio wanataka nianze kufanya kazi yao.

Wanataka kufuatilie na kujua details zaidi kuhusu huyo Mtanzania na mambo mengine kama hayo, mimi siwezi kuingilia hayo masuala ya wao, wenyewe ndio wataalam, mimi nikiwapa taarifa wanatakiwa kujua nini cha kufanya baada ya hapo.

Huyu mtanzania ninamfahamu kwa jina moja tu anaitwa Jane, mitaa ya Houston ndani ya Texas.

Maisha yake ni chini ya Daraja, amekuwa hivyohivyo akiishi chini ya Daraja.
View attachment 2995304
View attachment 2995860
Barua niliyowahi kuituma Ubalozini siku za nyuma​

Nilivyoanza kumjua
Kuna siku nikiwa na mke wangu kwenye bustani flani akasikia tunazungumza Kiswahili, akajumuika nasi na kuanza kuzungumza na kisha kujitambulisha.

Tukazungumza naye kwa Kiswahili na akajieleza naye anatoka Ukanda wa Kaskazini kama nilivyo mimi hapo nyumbani Tanzania.

Bahati mbaya nimesahau jina lake la pili na hata sas aukisema umuulie huwezi kupata jibu hilo.

Nimeshatoa picha zake mara kadhaa sehemu tofauti ili anayemjua iwe ni ndugu zake, jamaa au marafiki wamsaidie lakini sijafanikiwa katika hilo, ndio maana nimeona nitumie JamiiForums kufikisha ujumbe huu nadhani utawafikia wahusika na wanaweza kumsaidia.

Nipo tayari kuto ushirikiano kwa ambaye anaweza kuhitaji kumsaidia huyu au kama anawez kumtambua, nimewasilisha mawasiliano yangu kwa JamiiForums kwa mtu ambaye atahitaji kuwasiliana nami.
Hii stori inawea kuwa ni ya kutunga, si halisi
Vinginevyo kana ni ya kweli, utakuwa unafanya makosa makubwa sana
Watu wa aina hii wapo wengi tu Marekani na si lazima wawe wametoka Tanzania. Wewe uanchotakiwa kufanya ni kupata details za familia yao huku Tanzania, ili Ubalozi watakapoingia kazini, wawe na uhakika kuwa mtu huyu kweli ni Mtanzania
Naamini Ubalozi wanayo pia register ya wanafunzi watanzania wanaosoma huko, na possibly kati ya walio kwenye orodha yao, huyo siyo mmoja wao

Wewe unatakiwa uwa-provie ubalozi kuwa huyu mtu kweli ni Mtanzania, halafu baada ya hapo ndiyo uweze kuwalaumu
Wewe kwa details zote ulizozitoa hapa, unashindwa nini kupata taarifa za kule alikotoka? Wenzake aliokuwa anasoma nao, je?
Isisje ikawa ulitamani tu kuweka picha za watu wakiwa nusu uchi humu kwa visingizio
Taarifa yako hii inaweza kuwa ni crap, inaweza ikawa ni ya kutunga
 
Kama makada wa ccm wanaokotwa huko na kupewa ubalozi unategemea nini
Mtu kama polepole ana mastress yake yote unampa Ubalozi unategemea atasaidia kwetu

Sababu kapewa ubalozi kama adhabu nchi hii ina safari ndefu sana
Kuna balozi alitumwa nchi flani alipofika airport hajui hadhi yake akafuatana na wasafiri wa kawaida
Anaulizwa passport anatoa ya diplomatic
Akaambiwa ilibidi uende VIP lounge yaani hata kutoka tu hawajui itakuwa kazi zao

Wengine utafikiri walikuwa wanaishi na kuku tu
 
Back
Top Bottom