DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mimi ni Mtanzania ninayeishi Marekani, kuna Mtanzania mwenzetu mbaye alikuja kama Mwanafunzi hapa, sijui vizuri kuhusu historia yake huko nyuma.

Miaka kadhaa iliyopita alipata changamoto ya Afya ya Akili, sijui nini kiliendelea baada ya hapo kati lakini kilichofuata amekuwa chizi na analala barabarani, amekuwa akifanyiwa ukatili wa kingono na Wanaume mara nyingi bila kuwa na msaada.

Nilienda Ubalozini mara kadha pia kuripoti ili ikiwezekana huyu Mtanzania asaidiwe lakini kinachoonekana wao (Ubalozi) ndio wanataka nianze kufanya kazi yao.

Wanataka kufuatilie na kujua details zaidi kuhusu huyo Mtanzania na mambo mengine kama hayo, mimi siwezi kuingilia hayo masuala ya wao, wenyewe ndio wataalam, mimi nikiwapa taarifa wanatakiwa kujua nini cha kufanya baada ya hapo.

Huyu mtanzania ninamfahamu kwa jina moja tu anaitwa Jane, mitaa ya Houston ndani ya Texas.

Maisha yake ni chini ya Daraja, amekuwa hivyohivyo akiishi chini ya Daraja.
View attachment 2995304
View attachment 2995860
Barua niliyowahi kuituma Ubalozini siku za nyuma​

Nilivyoanza kumjua
Kuna siku nikiwa na mke wangu kwenye bustani flani akasikia tunazungumza Kiswahili, akajumuika nasi na kuanza kuzungumza na kisha kujitambulisha.

Tukazungumza naye kwa Kiswahili na akajieleza naye anatoka Ukanda wa Kaskazini kama nilivyo mimi hapo nyumbani Tanzania.

Bahati mbaya nimesahau jina lake la pili na hata sas aukisema umuulie huwezi kupata jibu hilo.

Nimeshatoa picha zake mara kadhaa sehemu tofauti ili anayemjua iwe ni ndugu zake, jamaa au marafiki wamsaidie lakini sijafanikiwa katika hilo, ndio maana nimeona nitumie JamiiForums kufikisha ujumbe huu nadhani utawafikia wahusika na wanaweza kumsaidia.

Nipo tayari kuto ushirikiano kwa ambaye anaweza kuhitaji kumsaidia huyu au kama anawez kumtambua, nimewasilisha mawasiliano yangu kwa JamiiForums kwa mtu ambaye atahitaji kuwasiliana nami.
Yuko state gani; hebu ni-PM details zaidi.
 
Mbona barua imeandikwa na Masilingi na tarehe ni 2018 huko??? Saivi yuko bi Kanza, ni nini sijaelewa hapo?
 
Mpumbavu hujulikana kwa maneno na matendo anayotenda na siyo kwa kutukanwa! Wewe ndiyo umeonyesha upumbavu wako kwa kufurahia huyo mateso anayopata huyo mgonjwa kisa tu umekosa connection ya kusafiri kama yeye. Dunia ya leo imekuwa kama kijiji na binadamu wanakuwa encouraged kusafiri na kuishi nchi nyingine ili wajifunze vitu vipya wewe unakuja na ulimbukeni wa kufurahia janga linalompata binadamu mwenzako eti kwa sababu tu amekwenda nchi nyingine. Kama siyo wivu na roho ya kichawi ni nini. Umefungiwa hapo Bongo? Jitahidi na wewe utembee uone dunia na siyo kuwa na roho ya kichawi ya kutaka waliokuzidi waangamie. Hizi ni chuki na wivu uliopitiliza na inaonekana wewe unaishi kwenye maisha ya shida na yenye frustration sana. Watu walio nje ya nchi wakirudi kukaa Bongo ndiyo watamaliza shida zako?
Nakazia mkuu
 
Back
Top Bottom