DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Unajiita Dokta Alafu hujui Taarifa whitney ..yule ni hujuma zilifanyika Kwake na mtoto wake pia..Sina mida wa kuelezea Sana ..ila aliuwawa.
Sasa hapo kuna issue nyingi, miaka 10 Marekani huna makaratasi ni uzembe.

Halafu usikute aliingia kwenye drug abuse.

Ujuwe yule Whitney Houston alikuwa demu smart sana lakini alipokutana na Bob Brown ndio alimfundisha kubwia unga hadi kifo chake.
 
Mleta mada alijuaje kama ni Mtz!? Hata kama aliongea naye kiswahili....bado haitoshi kusema yeye Mtz ....
 
Nikisema kuhusu balozi za Watanzania mnabisha hapo ni swala la siku moja tu hilo huyo dada yupo Tanzania ila Watanzania wakipata tu vyeo ni makatili kupita kiasi niliwahi kuambiwa na bwana mdogo mmoja Mnigeria kuhusu huyo dada sikuamini maana hakuna na picha aliniambia kuwa pana dada Mtanzania anapata tabu huko mtaani ninyi hamna msaada wowote...mkuu ukiweza wasiliana na Agent afanye hiyo kazi utapata dhawabu za kutosha sana inaumiza sana hasa kwa sisi wasafiri hatujui kesho yetu ipoje...
 
Sasa si ndo wee umsaidie hapo kwa kumuhifadhi na nk, huku ukisubiri ndugu zake wajitokezee.

Kumuacha ahangaike na huku unamtangaza, si unamchoresha tyuu.
Unafikili kumhifadhi mtu mwenye tatizo la akili ni jambo dogo?
 
Unatakiwa kuelewa mipaka yako na kuheshimu privacy ya mtu.

Kwanza umeenda kumrekodi bila ya ridhaa yake, unalazimisha kumpa msaada wa hela ambao auhitaji; halafu unamposti mitandaoni huo ni udhalilishaji.

Pili unalazimisha msaada kwa mtu ambae ajakuomba na hataki hiyo ni kuingilia rights zake. Dada anaonekana ni mzima maana unakiri umewahi kuongea nae na hata hapo kwenye video inaonekana anajielewa huo uchizi unampa wewe.

Tatu hujui changamoto zake za maisha hadi kua homeless, ungeanzia kudadisi hapo kimetokea nini kwenye maisha yake hadi kufikia alipofika.

Nne kama lengo ni kutaka ndugu zake wapate habari ungeweza anzisha mada kwa title yoyote na ku-crop sura yake tu na kuomba msaada kama kuna mtu anamfahamu huyo dada wakupe details za ndugu zake uwape taarifa, wao ndio wana mamlaka ya kwenda serikalini na kuomba msaada arudishwe.

Umemkosea sana huyo dada na kumdhalilisha.
Naungana na wewe mkuu ila ni wachache sana watakao kuelewa hasa hili la kumrekodi na kupost mtandaoni,
Nashauri Moderator waiondoe hiyo picha pamoja na hiyo vdo clip.
 
Mimi ni Mtanzania ninayeishi Marekani, kuna Mtanzania mwenzetu mbaye alikuja kama Mwanafunzi hapa, sijui vizuri kuhusu historia yake huko nyuma.

Miaka kadhaa iliyopita alipata changamoto ya Afya ya Akili, sijui nini kiliendelea baada ya hapo kati lakini kilichofuata amekuwa chizi na analala barabarani, amekuwa akifanyiwa ukatili wa kingono na Wanaume mara nyingi bila kuwa na msaada.

Nilienda Ubalozini mara kadha pia kuripoti ili ikiwezekana huyu Mtanzania asaidiwe lakini kinachoonekana wao (Ubalozi) ndio wanataka nianze kufanya kazi yao.

Wanataka kufuatilie na kujua details zaidi kuhusu huyo Mtanzania na mambo mengine kama hayo, mimi siwezi kuingilia hayo masuala ya wao, wenyewe ndio wataalam, mimi nikiwapa taarifa wanatakiwa kujua nini cha kufanya baada ya hapo.

Huyu mtanzania ninamfahamu kwa jina moja tu anaitwa Jane, mitaa ya Houston ndani ya Texas.

Maisha yake ni chini ya Daraja, amekuwa hivyohivyo akiishi chini ya Daraja.

Nilivyoanza kumjua
Kuna siku nikiwa na mke wangu kwenye bustani flani akasikia tunazungumza Kiswahili, akajumuika nasi na kuanza kuzungumza na kisha kujitambulisha.

Tukazungumza naye kwa Kiswahili na akajieleza naye anatoka Ukanda wa Kaskazini kama nilivyo mimi hapo nyumbani Tanzania.

Bahati mbaya nimesahau jina lake la pili na hata sas aukisema umuulie huwezi kupata jibu hilo.

Nimeshatoa picha zake mara kadhaa sehemu tofauti ili anayemjua iwe ni ndugu zake, jamaa au marafiki wamsaidie lakini sijafanikiwa katika hilo, ndio maana nimeona nitumie JamiiForums kufikisha ujumbe huu nadhani utawafikia wahusika na wanaweza kumsaidia.

Nipo tayari kuto ushirikiano kwa ambaye anaweza kuhitaji kumsaidia huyu au kama anawez kumtambua, nimewasilisha mawasiliano yangu kwa JamiiForums kwa mtu ambaye atahitaji kuwasiliana nami.
Mkuu asante kwa taarifa nadhani ndugu zake wanaeza kupata habari!ila huko US si kuna vituo vya kutunza hawa watu!i think ni busara ukampeleka huko ktk vituo ili apate matibabu huku ndugu wakisubiriwa!si serikali ya US ndo inawatunza au hali ikoje huko.
 
Ukienda nje kitu pekee kitakachokusaidia zingatia sana kwenda sehem za ibada .kama Ww ni mkristo Nenda kanisani na kama Ww ni muislam Nenda msiktini ,huko ndipo utakutana na watu sahihi .yani jichanganye maeneo ya ibada yako,tatizo sisi tukienda nje tunajiona tumefika yani tumeyamaliza mpaka unasahau ibada mwisho wa siku unajichanganya mtaani unasahau kilichokupeleka .ndugu zangu duniani kuna wema.sehem za ibadani kuna connection kubwa sana
 
Unatakiwa kuelewa mipaka yako na kuheshimu privacy ya mtu.

Kwanza umeenda kumrekodi bila ya ridhaa yake, unalazimisha kumpa msaada wa hela ambao auhitaji; halafu unamposti mitandaoni huo ni udhalilishaji.

Pili unalazimisha msaada kwa mtu ambae ajakuomba na hataki hiyo ni kuingilia rights zake. Dada anaonekana ni mzima maana unakiri umewahi kuongea nae na hata hapo kwenye video inaonekana anajielewa huo uchizi unampa wewe.

Tatu hujui changamoto zake za maisha hadi kua homeless, ungeanzia kudadisi hapo kimetokea nini kwenye maisha yake hadi kufikia alipofika.

Nne kama lengo ni kutaka ndugu zake wapate habari ungeweza anzisha mada kwa title yoyote na ku-crop sura yake tu na kuomba msaada kama kuna mtu anamfahamu huyo dada wakupe details za ndugu zake uwape taarifa, wao ndio wana mamlaka ya kwenda serikalini na kuomba msaada arudishwe.

Umemkosea sana huyo dada na kumdhalilisha.
Kwamba ilimradi na wewe uonekane umetoa maoni jamii forum sio!?🐒
 
Acha kabisa, nakumbuka rafiki yangu naye alikutwa na hili, jamaa alikuwa very smart darasani bahati mbaya mwisho mwisho na kumaliza chuo akachizika aisee, mbinu zote za kitaalamu zimetumika lakini wapi Hadi Leo hii ana mawenge japo ana afadhali, maisha haya unaweza kusoma vizuri ukapata A's Kila somo kama mshikaji wangu lakini ukaishia vibaya.
 
Kwahiyo mtu alie changanyikiwa aombwe ridhaa ya kurekodiwa Ili asaidiwe?
Haya mambo ya sheria na haki za binadam yamevamiwa
Medical ethics
1. Beneficence
2. Non-małeficence
3. Autonomy
4. Justice

Uwezi kwenda kujifanyia mambo tu bila ya ridhaa ya wahusika ata kama unadhani ni wagonjwa hasa pale wanaposema awataki kwa hizo kanuni au kufanya mambo yanayoshusha utu wao.

Kingine huyo mtu sio mgonjwa kama mnavyokadhana kisa mleta mada kasema. Angekuwa hana akili timamu huko sio Tanzania mamlaka zimuangalie mental patient (vulnerable individual) anadhurura bila ya wao kuchukua hatua, kichaa akifanya jinai hizo nchi hata akiuwa uwezi mshitaki kisheria. Sasa kwanini wamuache mtaani.

Ni homeless tu mwenye akili zake timamu, sema mtu kaanzisha mada na kumpa label yake basi kila mtu anaamini ivyo.

Yeye kajuaje ni kichaa ana medical records zake, mtu ata jina lake kamili alijui au anasababu gani nyingine ya kusema kachanganyikiwa other than her sleeping rough. Mtu ata hiyo community yao ya wotanzania wavHouston hawamjui wala changamoto zake hadi kufikia hapo halafu unamwita mtu chizi tu.

Ni mzima huyo vinginevyo angekuwa mental health unit kama kweli mgonjwa.
 
Akimsaidia kwa kumuhifadhi baadae watajitokeza wakosoaji wenye akili kama yako kisha watamsingizia kwamba amemuhifadhi ili kumtumia kwa manufaa yake kisha atapewa kesi nzito hata ya kubaka,hili jambo umelifikiria?
Alichofanya ni sahihi kabisa amefuata sheria na kanuni zinavyotaka kwa kuripoti kwa mamlaka husika,mamlaka ikashindwa kutekeleza wajibu wake akaona atumie njia mbadala ya kupost social media ili wanaomtambua wafanye ufuatiliaji wizarani na kuwapush ubalozini,jamaa nampongeza kwa kutumia muda wake kulifuatilia hili jambo.
 
Nimesikitika sana kwa jibu la balozi zetu. Sasa wapo huko nje ubalozini kwa kazi gani kama wanashindwa saidia watu wetu? Nimeumia kwa kweli, bora tuendelee kula ugali na dagaa nchini kwetu kuliko kwenda nje huko kudharirika bila msaada. Kwa namna huyo binti alivyo, hata usingesema anadharirishwa kingono nilijua hilo lipo


Very painful. Vipi nyie diaspora mnafanyaje kumsaidia kwa kumkamata na kuishi naye (Kumuhifadhi sehemu salama) huku mkifanya utaratibu wa kumrudisha nyumbani?
Makamba pia linamuhusu hili kama ubalozi umeshindwa , tujitahidi kupushi hata X kule limfikie .
 
Kwamba ilimradi na wewe uonekane umetoa maoni jamii forum sio!?🐒
Kwenye nchi isiyofuata utaratibu wa medical intervention unaweza ona kilichofanywa sawa.

Huko anakoishi huyo dada akipata hizi habari na kum-report polisi jamaa anaweza kuwa na shida ni violation of her rights and privacy, pamoja na kumuondelea dignity and respect. Mambo ambayo uruhusiwi kufanya kwa mgonjwa, let alone kwa mtu mwenye akili zake timamu kama huyo dada.
 
Kuna binamu yangu naye ni binti alipiga six fresh kwa ufaulu mzuri pale msalato girls miaka ya 97, akakacha kwenda chuo, akaenda Marekani, alikaa huko zaidi ya miaka 10 hakuna mafanikio yoyote ukizingatia wenzake waliamua kupambana hapa Bongo wengi wapo kwenye position na maisha mazuri , so ndugu zake wameamua kumrudisha Bongo baada ya kupata Sonoma na kurun mental health, siku hizi anafungiwa tu ndani maskini, kumuona na urembo wake utasikitika sana.
😳
 
Back
Top Bottom