DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna binamu yangu naye ni binti alipiga six fresh kwa ufaulu mzuri pale msalato girls miaka ya 97, akakacha kwenda chuo, akaenda Marekani, alikaa huko zaidi ya miaka 10 hakuna mafanikio yoyote ukizingatia wenzake waliamua kupambana hapa Bongo wengi wapo kwenye position na maisha mazuri , so ndugu zake wameamuakumrudisha Bongo baada ya kupata Sonoma na kurun mental health, siku hizi anafungiwa tu ndani maskini, kumuona na urembo wake utasikitika sana.
Sad
 
Kama ni rahisi hivyo, fanya ndio umeipata hii habari, unamsaidia vipi huyo dada maana mleta mada kashindwa kaishia tu "KUMCHORESHA"? Au na wewe msaada wako umeishia kwenye kufyonza?
Mie niko mbali na huyo dada, yeye ndie yuko karibu nae, aanze yeye huku akisubiri msaada kutoka kwangu.
 
Inawezekana kuna mengi sana huyu balozi wetu ameyakalia kimya kuhusu hao watu wetu, Rais Samia afanye kitu hapa. Hakuna balozi pale afanye mishe nyengine tu aachishwe hiyo kazi ina wenyewe.
Hii taarifa ikisambaa zaidi kwenye media itamharibia rais wetu kwa mtu mmoja tu asiyewajibika huko.
 
Inasikitisha sana ,hapo kuna mambo kama matatu nahisi:-

1. Sonona ,Msongo wa mawazo, frustration zimemvuruga na kumsababishia mental health.

2. Inawezekana watu wamempiga kitu(Uswahili) maana naona ni PC ya kwenda.

3. Either ametoswa na Mupenzi au Rafiki aliyemleta huko ikapelekea kumvuruga akili.
She is beautiful
 
Akaita tu police akapelekwa kwa nguvu
Nashangaaa na huko texas watz ni wengi sana
Watanzania wachawi sana, ingekuwa ni Mkenya wangemstiri mwenzao.

Imagine hapo Texas kuna community za Watanzania, mnashindwa vipi kuita Ambulace tu huyo akapelekwa hospitali kupata matibabu?

Federal government inawalipa some health agencies kuwatunza watu kama hao, nadhani ndio kazi zenye malipo makubwa tena kama Australia sasa hivi wameshusha kodi kwenye mishahara unalipwa mpaka laki 4 za Kitanzania kwa siku.
 
Unatakiwa kuelewa mipaka yako na kuheshimu privacy ya mtu.

Kwanza umeenda kumrekodi bila ya ridhaa yake, unalazimisha kumpa msaada wa hela ambao auhitaji; halafu unamposti mitandaoni huo ni udhalilishaji.

Pili unalazimisha msaada kwa mtu ambae ajakuomba na hataki hiyo ni kuingilia rights zake. Dada anaonekana ni mzima maana unakiri umewahi kuongea nae na hata hapo kwenye video inaonekana anajielewa huo uchizi unampa wewe.

Tatu hujui changamoto zake za maisha hadi kua homeless, ungeanzia kudadisi hapo kimetokea nini kwenye maisha yake hadi kufikia alipofika.

Nne kama lengo ni kutaka ndugu zake wapate habari ungeweza anzisha mada kwa title yoyote na ku-crop sura yake tu na kuomba msaada kama kuna mtu anamfahamu huyo dada wakupe details za ndugu zake uwape taarifa, wao ndio wana mamlaka ya kwenda serikalini na kuomba msaada arudishwe.

Umemkosea sana huyo dada na kumdhalilisha.
Mimi naona mtoa mada yupo sahihi, angeanzisha mada bila picha au video ungedai picha na hata video. Amefanya hivyo ili ndugu, rafiki, jamaa, majirani na waliosoma pamoja wamtambue ili msaada uwe rahisi kupatikana.
 
Nasimama na mtoa mada, hao wengine waliopinga kisa sijui human right and privecy sijui nini hawa ndiyo aina ya watu wanaondekeza issue za ushoga ni wapiga kelele tu.
Sasa ushoga hapa unahusu nn? Umevurugwa na ushoga eeeh?
Poleeee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom