DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Maisha haya daa
Halafu balozi zetu huwa hazina msaada kabisa sijui kwanini

Kuna mataifa hata mtu wao akifungwa au kuhukumiwa kufa watamtoa.

Sasa masikini huyo tena mwanamke wanashindwa hata kumpeleka hospitali
Nchi nyingi za kiafrika huwa hazina msaada kwa raia wake!! Halafu utayasikia eti watu hatuna uzalendo!! Ndio maana wazungu wanakuwa wazalendo sana kwa nchi zao kwani hata wakipata matatizo huwa zinawasidia sana!!
 
Kuna mdada mwingine Belinda Ringo aliajiriwa na TPDC mwaka 2007 kama Lawyer. Baada ya mwaka mmoja TPDC wakampeleka UK kusoma Masters. Kufika huko akawehuka kabisa akakataa kurudi Tanzania. TPDC wakamfukuza kazi akiwa hukohuko. Jitihada za Familia yao zikafanikiwa wakamrudisha Tanzania lakini mpaka leo yupo TU nyumbani kwao Sinza karibu na Meeda akili haziko sawa
Jaman too sad
 
Mimi ni Mtanzania ninayeishi Marekani, kuna Mtanzania mwenzetu mbaye alikuja kama Mwanafunzi hapa, sijui vizuri kuhusu historia yake huko nyuma.

Miaka kadhaa iliyopita alipata changamoto ya Afya ya Akili, sijui nini kiliendelea baada ya hapo kati lakini kilichofuata amekuwa chizi na analala barabarani, amekuwa akifanyiwa ukatili wa kingono na Wanaume mara nyingi bila kuwa na msaada.

Nilienda Ubalozini mara kadha pia kuripoti ili ikiwezekana huyu Mtanzania asaidiwe lakini kinachoonekana wao (Ubalozi) ndio wanataka nianze kufanya kazi yao.

Wanataka kufuatilie na kujua details zaidi kuhusu huyo Mtanzania na mambo mengine kama hayo, mimi siwezi kuingilia hayo masuala ya wao, wenyewe ndio wataalam, mimi nikiwapa taarifa wanatakiwa kujua nini cha kufanya baada ya hapo.

Huyu mtanzania ninamfahamu kwa jina moja tu anaitwa Jane, mitaa ya Houston ndani ya Texas.

Maisha yake ni chini ya Daraja, amekuwa hivyohivyo akiishi chini ya Daraja.

Nilivyoanza kumjua
Kuna siku nikiwa na mke wangu kwenye bustani flani akasikia tunazungumza Kiswahili, akajumuika nasi na kuanza kuzungumza na kisha kujitambulisha.

Tukazungumza naye kwa Kiswahili na akajieleza naye anatoka Ukanda wa Kaskazini kama nilivyo mimi hapo nyumbani Tanzania.

Bahati mbaya nimesahau jina lake la pili na hata sas aukisema umuulie huwezi kupata jibu hilo.

Nimeshatoa picha zake mara kadhaa sehemu tofauti ili anayemjua iwe ni ndugu zake, jamaa au marafiki wamsaidie lakini sijafanikiwa katika hilo, ndio maana nimeona nitumie JamiiForums kufikisha ujumbe huu nadhani utawafikia wahusika na wanaweza kumsaidia.

Nipo tayari kuto ushirikiano kwa ambaye anaweza kuhitaji kumsaidia huyu au kama anawez kumtambua, nimewasilisha mawasiliano yangu kwa JamiiForums kwa mtu ambaye atahitaji kuwasiliana nami.
Hayo ndio matatizo ya kureua mabalizi bila kufata vigezzo, tayari umeshafanya msaada mkubwa.
Kwa sababu aliingia kihalali ni wazi kwenye passport Kuna sehemu ya ndugu au mtu wake wa karibu hii ni kufanya mawasiliano kupitia immigration ya huku pia kwa kutumia jumhiya ya watanzania waishio nje mnaweza kujipanga muwasaidie

Tunahitaji kuwaona upendo wao badala ya kupiga kelele wapewe haki ya uraia umefanya makubwa Mungy akybariki.
 
Wengine watasema heri kuwa kichaa kwenye nchi za watu kama huko USA kuliko kuwa mzima wa akili huku bongo!

Yote ya yote wakati utafika atapata msaada na wakati ndio huu , asante sana mleta mada, umefanya wema mkubwa sana na Mungu akaufanyia wema nawe pia.
 
Masikini dada wa watu isije kuwa watu wa kijijini kwao wamemroga.

Mungu amfanyie wepesi.
Kuna kijana alipata ufadhili wa kwenda kusoma nje na kwa kuwa wazazi wake walikuwa mkoa ikabidi akawaage ikiwa pamoja na kupata baraka pia, siku aliyoamka kurudi dar kwa ajili ya maandalizi alianza kuongea kauli tata na akavurugukiwa kabisa hata safari haikuwepo tena.
 
Maisha haya daa
Halafu balozi zetu huwa hazina msaada kabisa sijui kwanini

Kuna mataifa hata mtu wao akifungwa au kuhukumiwa kufa watamtoa.

Sasa masikini huyo tena mwanamke wanashindwa hata kumpeleka hospitali
Nchi ya kishetani sana hii, unafikiri wanatuona sisi wengine ni watu? Mungu amsaidie tu huyu jamaa alietoa taarifa
 
Maisha haya daa
Halafu balozi zetu huwa hazina msaada kabisa sijui kwanini

Kuna mataifa hata mtu wao akifungwa au kuhukumiwa kufa watamtoa.

Sasa masikini huyo tena mwanamke wanashindwa hata kumpeleka hospitali
Nimesikitika sana kwa jibu la balozi zetu. Sasa wapo huko nje ubalozini kwa kazi gani kama wanashindwa saidia watu wetu? Nimeumia kwa kweli, bora tuendelee kula ugali na dagaa nchini kwetu kuliko kwenda nje huko kudharirika bila msaada. Kwa namna huyo binti alivyo, hata usingesema anadharirishwa kingono nilijua hilo lipo

Very painful. Vipi nyie diaspora mnafanyaje kumsaidia kwa kumkamata na kuishi naye (Kumuhifadhi sehemu salama) huku mkifanya utaratibu wa kumrudisha nyumbani?
 
Mimi ni Mtanzania ninayeishi Marekani, kuna Mtanzania mwenzetu mbaye alikuja kama Mwanafunzi hapa, sijui vizuri kuhusu historia yake huko nyuma.

Miaka kadhaa iliyopita alipata changamoto ya Afya ya Akili, sijui nini kiliendelea baada ya hapo kati lakini kilichofuata amekuwa chizi na analala barabarani, amekuwa akifanyiwa ukatili wa kingono na Wanaume mara nyingi bila kuwa na msaada.

Nilienda Ubalozini mara kadha pia kuripoti ili ikiwezekana huyu Mtanzania asaidiwe lakini kinachoonekana wao (Ubalozi) ndio wanataka nianze kufanya kazi yao.

Wanataka kufuatilie na kujua details zaidi kuhusu huyo Mtanzania na mambo mengine kama hayo, mimi siwezi kuingilia hayo masuala ya wao, wenyewe ndio wataalam, mimi nikiwapa taarifa wanatakiwa kujua nini cha kufanya baada ya hapo.

Huyu mtanzania ninamfahamu kwa jina moja tu anaitwa Jane, mitaa ya Houston ndani ya Texas.

Maisha yake ni chini ya Daraja, amekuwa hivyohivyo akiishi chini ya Daraja.

Nilivyoanza kumjua
Kuna siku nikiwa na mke wangu kwenye bustani flani akasikia tunazungumza Kiswahili, akajumuika nasi na kuanza kuzungumza na kisha kujitambulisha.

Tukazungumza naye kwa Kiswahili na akajieleza naye anatoka Ukanda wa Kaskazini kama nilivyo mimi hapo nyumbani Tanzania.

Bahati mbaya nimesahau jina lake la pili na hata sas aukisema umuulie huwezi kupata jibu hilo.

Nimeshatoa picha zake mara kadhaa sehemu tofauti ili anayemjua iwe ni ndugu zake, jamaa au marafiki wamsaidie lakini sijafanikiwa katika hilo, ndio maana nimeona nitumie JamiiForums kufikisha ujumbe huu nadhani utawafikia wahusika na wanaweza kumsaidia.

Nipo tayari kuto ushirikiano kwa ambaye anaweza kuhitaji kumsaidia huyu au kama anawez kumtambua, nimewasilisha mawasiliano yangu kwa JamiiForums kwa mtu ambaye atahitaji kuwasiliana nami.
Pongezi nyingi kwa mtoa taarifa na kwa aliyerekodi video . Hio inaitwa usamaria mwema kutoa msaada wa hali na Mali kwa mtu usiyemjua .
Sasa ubalozi kazi Yao nini katika kutoa Huduma kwa wananchi ?
Kazi Yao ni kutoa viza na paspoti mpya na kula bata la marekani ?
Nini kimempata dada wa watu ? Alisoma sana akili ikafyatuka au alitumia vilevi au watu wabaya wametumia nguvu za giza
Mimi Naona mtoa taarifa ungeanza na kupigania mamlaka za USA wenyewe wamtrace ndugu zake maanake Kama wanaweza ku trace gaidi hawatashindwa kwa Hilo Suala na wazungu wanajali sana.

Picha yake ikiingizwa Kwenye database za immigration na state department zao jibu linapatikana Mara moja
 
Nchi za nje kunakua na Umoja wa Watanzania hivyo pia ilibidi wamsaidie kwa kumpeleka hospital au kumrudisha nyumbani na sio kuishia kumrekodi na kumuacha. Balozi nyingi za Tanzania Ulaya huaga hazina msaada wa matatizo kama hayo ila mkianzisha watanzania naona wanatoa michango yao.
 
Back
Top Bottom