Waterbender
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 7,573
- 10,063
Ndo maana wazazi wengine wanawa kataza watoto kwenda kusalimia kwao madhara yake ndo haya
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah mkuu we acha tu yani ni balaa umeongea ukweli mtupuWaafrika tunapigana vita nyingi sana, mtu uhangaike kusoma, kutafuta pesa, huku wengine wanakuroga na ukifa pia hakuna kupumzika unageuzwa mzimu aise, mungu amsimamie maskini binti wa watu
Kumbe ni muda mrefu sana. Aiseeeeee. Dkt. Gwajima D tunaomba mumsaidie dada yetu anayedharirika huko USA. Najua mama yetu unaweza fanya jambo au ukawa ni sehemu ya kuanzia kumsaidia binti yako ndio maana tumekuomba. Tunaomba uanze na kitu kwani tunajua wewe ndio Waziri unayefikika kwa urahisi pia una respond nzuri. Fanya kitu kwa Dada yetu na Mungu atakulipa.Ni mwaka wa saba (7) sasa tangu hili tangazo lilipo tolewa kwa mara ya kwanza.
Anyways, tuombe ndugu zake wapatikane mkuu, maana huko US hata rafiki hawezi akawa radhi kumuhifadhi mtu alie na shida ya akili.
Comment kama hii ndio inaonyesha maana halisi ya utanzania.Unatakiwa kuelewa mipaka yako na kuheshimu privacy ya mtu.
Kwanza umeenda kumrekodi bila ya ridhaa yake, unalazimisha kumpa msaada wa hela ambao auhitaji; halafu unamposti mitandaoni huo ni udhalilishaji.
Pili unalazimisha msaada kwa mtu ambae ajakuomba na hataki hiyo ni kuingilia rights zake. Dada anaonekana ni mzima maana unakiri umewahi kuongea nae na hata hapo kwenye video inaonekana anajielewa huo uchizi unampa wewe.
Tatu hujui changamoto zake za maisha hadi kua homeless, ungeanzia kudadisi hapo kimetokea nini kwenye maisha yake hadi kufikia alipofika.
Nne kama lengo ni kutaka ndugu zake wapate habari ungeweza anzisha mada kwa title yoyote na ku-crop sura yake tu na kuomba msaada kama kuna mtu anamfahamu huyo dada wakupe details za ndugu zake uwape taarifa, wao ndio wana mamlaka ya kwenda serikalini na kuomba msaada arudishwe.
Umemkosea sana huyo dada na kumdhalilisha.
Sasa hapo kuna issue nyingi, miaka 10 Marekani huna makaratasi ni uzembe.Kuna binamu yangu naye ni binti alipiga six fresh kwa ufaulu mzuri pale msalato girls miaka ya 97, akakacha kwenda chuo, akaenda Marekani, alikaa huko zaidi ya miaka 10 hakuna mafanikio yoyote ukizingatia wenzake waliamua kupambana hapa Bongo wengi wapo kwenye position na maisha mazuri , so ndugu zake wameamuakumrudisha Bongo baada ya kupata Sonoma na kurun mental health, siku hizi anafungiwa tu ndani maskini, kumuona na urembo wake utasikitika sana.
Akaita tu police akapelekwa kwa nguvuNinachofahamu mimi Marekani hata uwe huna hata mia utatibiwa kwanza mambo mengine baadaye.
Huyu aliyeleta hizi taarifa ameshindwa vipi kukutana na Watanzania wachache kumsaidia huyu dada kupelekwa kwenye matibabu?
Hatuwezi kusaidia MTU aliyepo US, wakati kuna wenye shida kibao zaidi ya hiyo huku nyumbani,Mbwa anahudumiwa vzr UK/US kuliko Bongo,Mimi ni Mtanzania ninayeishi Marekani, kuna Mtanzania mwenzetu mbaye alikuja kama Mwanafunzi hapa, sijui vizuri kuhusu historia yake huko nyuma.
Miaka kadhaa iliyopita alipata changamoto ya Afya ya Akili, sijui nini kiliendelea baada ya hapo kati lakini kilichofuata amekuwa chizi na analala barabarani, amekuwa akifanyiwa ukatili wa kingono na Wanaume mara nyingi bila kuwa na msaada.
Nilienda Ubalozini mara kadha pia kuripoti ili ikiwezekana huyu Mtanzania asaidiwe lakini kinachoonekana wao (Ubalozi) ndio wanataka nianze kufanya kazi yao.
Wanataka kufuatilie na kujua details zaidi kuhusu huyo Mtanzania na mambo mengine kama hayo, mimi siwezi kuingilia hayo masuala ya wao, wenyewe ndio wataalam, mimi nikiwapa taarifa wanatakiwa kujua nini cha kufanya baada ya hapo.
Huyu mtanzania ninamfahamu kwa jina moja tu anaitwa Jane, mitaa ya Houston ndani ya Texas.
Maisha yake ni chini ya Daraja, amekuwa hivyohivyo akiishi chini ya Daraja.
Nilivyoanza kumjua
Kuna siku nikiwa na mke wangu kwenye bustani flani akasikia tunazungumza Kiswahili, akajumuika nasi na kuanza kuzungumza na kisha kujitambulisha.
Tukazungumza naye kwa Kiswahili na akajieleza naye anatoka Ukanda wa Kaskazini kama nilivyo mimi hapo nyumbani Tanzania.
Bahati mbaya nimesahau jina lake la pili na hata sas aukisema umuulie huwezi kupata jibu hilo.
Nimeshatoa picha zake mara kadhaa sehemu tofauti ili anayemjua iwe ni ndugu zake, jamaa au marafiki wamsaidie lakini sijafanikiwa katika hilo, ndio maana nimeona nitumie JamiiForums kufikisha ujumbe huu nadhani utawafikia wahusika na wanaweza kumsaidia.
Nipo tayari kuto ushirikiano kwa ambaye anaweza kuhitaji kumsaidia huyu au kama anawez kumtambua, nimewasilisha mawasiliano yangu kwa JamiiForums kwa mtu ambaye atahitaji kuwasiliana nami.
Acha ujinga Kaka.Kuwa homeless ni mental issue tangu lini?
Mbona anaonekana anajitambua tu.
Wakumsaidia ni ndugu zake kama yeye awezi kumuweka kwake.
Vinginevyo angeweka picha yake na kuomba msaada kwa anaemjua amtafute anashida ya kuongea na ndugu zake bila ya kuweka narrative (which is pretty his interpretation of her situation) on what is going on with her life.
Uwezi kuvunja rights za mtu, invade her privacy and ignore her dignity; kisa unataka kumsaidia huo ni udhalilishaji.
Yes apige 911.Akaita tu police akapelekwa kwa nguvu
Nashangaaa na huko texas watz ni wengi sana
Aiseee.....Kuna kijana alipata ufadhili wa kwenda kusoma nje na kwa kuwa wazazi wake walikuwa mkoa ikabidi akawaage ikiwa pamoja na kupata baraka pia, siku aliyoamka kurudi dar kwa ajili ya maandalizi alianza kuongea kauli tata na akavurugukiwa kabisa hata safari haikuwepo tena.
Balozi zetu hazina msaada zimejaza watu wasiojitambua
Bora hata ungeilipia hiyo huruma kuliko kuiona bure.Nimemuonea huruma bure daah 🥺🥺🥺
T
TZ Kila kitu hovyo TU! Yapo ubalozini yanakula yananenepeana TU!