DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Usijekuta kuna mtu kamsomesha halafu alivyofika huko jamaa akimtafuta anamwambia hawezi kuolewa na yeye kwa sababu sio wa hadhi yake!
 
Acha kabisa, nakumbuka rafiki yangu naye alikutwa na hili, jamaa alikuwa very smart darasani bahati mbaya mwisho mwisho na kumaliza chuo akachizika aisee, mbinu zote za kitaalumu zimetumika lakini wapi Hadi Leo hii ana mawenge japo ana afadhali, maisha haya unaweza kusoma vizuri ukapata A's Kila somo kama mshikaji wangu lakini ukaishia vibaya.
Hili suala siwezi kusema maana watu wana imani tofauti .

Sadly, rafiki yangu ndugu yangu wa karibu kutoka sehemu moja alipata uchizi wa kuvua nguo kabisa,nae alikuwa smart sana na alikimbia kwao akakutwa huku Temeke tena watu wa msikitini ndio walimtangaza , walimpa chakula . Mwanzo alidhaniwa kuwa ni mwizi maana aliingia msiktini na kujificha na vile ana nguo chafu chafu .

Scenaria nyingine, jamaa alipata scholarship huyu alikuwa mkubwa kwangu , kabla ya kwenda Marekani walipelekwa Uganda ila alipofika huko alipata ukiziwi (hearing loss) mpaka kesho plus mawenge kibao , unamuulza hiki anajibu hiki ila alikuwa mwanafunzi bora huko chuoni.

Mwingine sister alikuwa anaitwa Irene , alienda chuo hivi vya certificate huko singida akapata kichaa ila ilihusishwa na kumkataa jamaa ambaye ni mwanafunzi mwenzie, pia huko mwanzoni watu walipiga kumgombania yeye.

Mambo haya sipendi kuongelea kweny ushirikina ila nimeona live , acha rafiki yangu alikuwa anafungwa kweny magongo.
 
Unatakiwa kuelewa mipaka yako na kuheshimu privacy ya mtu.

Kwanza umeenda kumrekodi bila ya ridhaa yake, unalazimisha kumpa msaada wa hela ambao auhitaji; halafu unamposti mitandaoni huo ni udhalilishaji.

Pili unalazimisha msaada kwa mtu ambae ajakuomba na hataki hiyo ni kuingilia rights zake. Dada anaonekana ni mzima maana unakiri umewahi kuongea nae na hata hapo kwenye video inaonekana anajielewa huo uchizi unampa wewe.

Tatu hujui changamoto zake za maisha hadi kua homeless, ungeanzia kudadisi hapo kimetokea nini kwenye maisha yake hadi kufikia alipofika.

Nne kama lengo ni kutaka ndugu zake wapate habari ungeweza anzisha mada kwa title yoyote na ku-crop sura yake tu na kuomba msaada kama kuna mtu anamfahamu huyo dada wakupe details za ndugu zake uwape taarifa, wao ndio wana mamlaka ya kwenda serikalini na kuomba msaada arudishwe.

Umemkosea sana huyo dada na kumdhalilisha.
Nyinyi ndo wachawi sasa. Roho Mbaya mbaya tu
 
Shit happens hizo nchi unakuta mtu hana makaratasi na hana marafiki au wanamtosa anaishia kuwa homeless and stressed.

Binafsi binamu yangu ni ‘on and off’ teja. Ugonjwa wake mkewe, mara mwisho mkewe kumtibua na jumba kubwa (home office) kuto renew makaratasi yake ya kusafiri (japo ana haki zingine) amekuwa teja na kibaka zaidi ya miaka 10 sasa anaishi mtaani. Ana ndugu zake wa tumbo moja na cousins kadhaa watu wamepigana kumsaidia mpaka wamechoka.

Kuna watu wanaanza kutumia madawa ya kulevya wanajiaribia maisha wenyewe.

Kuna watu hawana kazi au rent wanaishia kufukuzwa kwenye nyumba wanazoishi na hakuna wa kuwasaidia na kuna watu wana stress za papers.

Sababu ni luluki

Mwisho kabisa kwenye medical ethics kuna dhana ya right ‘uwezi kumpa mtu dawa au matibabu’ ambayo yeye hataki.

Alikadhalika kwa kanuni za Geneva convention on human right ‘kila mtu ana haki ya privacy and being treated with dignity’ uwezi kwenda kurekodi maisha ya mtu tena akiwa at her worst na kuitangazia dunia, wakati mwenyewe anamwambia hataki.

Jamaa kamkosea sana huyo dada
Acha udwanzi kuwekwa wazi asaidiwe ni sahihi kuliko kuheshimu your so called privacy huku muathirika anatumbukia kichwa chini kwa kasi katika shimo la uharibifu wa upweke, sonona na ugonjwa wa akili jumlisha na kukosa malazi.
 
Ni mwaka wa saba (7) sasa tangu hili tangazo lilipo tolewa kwa mara ya kwanza.
Anyways, tuombe ndugu zake wapatikane mkuu, maana huko US hata rafiki hawezi akawa radhi kumuhifadhi mtu alie na shida ya akili.
HANA WATOTO? MIAKA 7???
 
Kwenye nchi isiyofuata utaratibu wa medical intervention unaweza ona kilichofanywa sawa.

Huko anakoishi huyo dada akipata hizi habari na kum-report polisi jamaa anaweza kuwa na shida ni violation of her rights and privacy, pamoja na kumuondelea dignity and respect. Mambo ambayo uruhusiwi kufanya kwa mgonjwa, let alone kwa mtu mwenye akili zake timamu kama huyo dada.
Tatizo letu watanzania tunadandia Train kwa mbele wewe hujawahi muona au kukutana naye Leo unasema Ana akili timamu pia una ongea vingereza vyako vya kufugia sungura nchi za watu zipi unajua Mimi Niko wapi pia hiyo privacy unayo Sema unajua maana yake?
 
Alie kuambia siko tayari kumsaidia Ninani? Pia swala lakimsaidia sio langu ni lakibalozi ungekua unajua mateso ya huyu dada usinge Sema hayo usemayo siwezi kukulaumu kwa kua hujui usemalo
Umeni quote kwa kudhamilia, au bahati mbaya. Lol
 
Matatizo ya akili yasikie kwa mwenzio.
Kuna rariki yangu anaishi na wapangaji wenzie mmoja ni rafiki yake. Sasa kumbe jamaa ana matatizo ya akili yaani baada ya miaka kadhaa uwa inamrudia .siku moja usiku yule jamaa mwenye matatizo ya akili akmfuata rafiki yangu usiku mlangoni kwake. Kashika biblia na bakora mbili.akagonga mlango jamaa yangu akamfungulia.yyle mwenye matatizo ya akili akamwambia rafiki yangu na kuuliza swali kila swali moja ukikosa bakora moja.weeee .🤣🤣🤣🤣
Kweli kabisa mkuu. Ugonjwa wa akili usiombee, maana ubongo nadhani ndio organ iliyo complicated kuliko kiungo chochote cha mwanadamu. Yaani cell moja ikitilisika tu, basi dish lote linayumba.

Halafu wengi wetu tunaenda Ughaibuni kutafuta maisha na vikorokoro vingi vikiwemo maradhi kama haya (ambayo labda ni ya kurithi). Sasa unapokumbana na misukosuko ya maisha, mapenzi au upweke ndio hilo zimwi linajitokeza. Sasa kama huna watu wa karibu kama vile ndugu au marafiki wa dhati, ndio ntolee tena.

Mara mtu anaanza kutembea mji mzima bila sababu, analala pasipojulikana. Lakini mwisho wa yote ni njaa. Njaa ndio inayowafanya wagonjwa wa akili waanze kuwa ombaomba, umalya au waingie kwenye mapipa ya takataka kuganga njaa. Na hali ikifikia hapo ndio mwisho Sasa.

Maana baada ya hapo kwa ughaibuni, madawa ya kulevya yanaingia (Crack cocaine au meth ndio matunda ya street life)..... yaani hapo ni Nusra za Mwenyezimungu ndio zitamuokoa mtu. Mwenyezimungu atuepushe sote na hili balaa.
 
Umeni quote kwa kudhamilia, au bahati mbaya. Lol
Andika kiswahili tu nitakuelewa Mimi ni mtanzania ninaye ishi Marekani kingereza ni lugha sio Elimu narudia Tena naomba uelewe mtu yoyote anapokua Nje ya nchi yake akipata matatizo Kama yapo Nje ya uwezo wa jamii inayo mzunguka ni kazi ya ubalozi wa nchi husika kufuatilia na kutoa msaada au wewe unajua kazi ya mabalozi ni kutangaza utalii tu lakini ngoja nikuachie hapo nimesha kuelewa uelewa wako
 
Acha udwanzi kuwekwa wazi asaidiwe ni sahihi kuliko kuheshimu your so called privacy huku muathirika anatumbukia kichwa chini kwa kasi katika shimo la uharibifu wa upweke, sonona na ugonjwa wa akili jumlisha na kukosa malazi.

Kitendo cha ku-post hiyo video, tena mwenyewe anamwambia niache sitaki; ame-violate kanuni kadhaa za afya na human rights naweza kukujazia uzi nikitaja zote.

Mambo mengine yanataka uelewa na experience ya maisha hayo mambo ni kawaida hata kwa wazungu wenyewe huko kwao kulała rough kipindi ambacho unashida na huna msaada.
 
Tatizo letu watanzania tunadandia Train kwa mbele wewe hujawahi muona au kukutana naye Leo unasema Ana akili timamu pia una ongea vingereza vyako vya kufugia sungura nchi za watu zipi unajua Mimi Niko wapi pia hiyo privacy unayo Sema unajua maana yake?
Wewe peke yako ndio unaishi ulaya kwenye hii mada.

Wakują utawajua tu
 
Andika kiswahili tu nitakuelewa Mimi ni mtanzania ninaye ishi Marekani kingereza ni lugha sio Elimu narudia Tena naomba uelewe mtu yoyote anapokua Nje ya nchi yake akipata matatizo Kama yapo Nje ya uwezo wa jamii inayo mzunguka ni kazi ya ubalozi wa nchi husika kufuatilia na kutoa msaada au wewe unajua kazi ya mabalozi ni kutangaza utalii tu lakini ngoja nikuachie hapo nimesha kuelewa uelewa wako
Wee mtu unani quote kwa kudhamilia au unapuyangaa? Sikuelewii.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kweli kabisa mkuu. Ugonjwa wa akili usiombee, maana ubongo nadhani ndio organ iliyo complicated kuliko kiungo chochote cha mwanadamu. Yaani cell moja ikitilisika tu, basi dish lote linayumba.

Halafu wengi wetu tunaenda Ughaibuni kutafuta maisha na vikorokoro vingi vikiwemo maradhi kama haya (ambayo labda ni ya kurithi). Sasa unapokumbana na misukosuko ya maisha, mapenzi au upweke ndio hilo zimwi linajitokeza. Sasa kama huna watu wa karibu kama vile ndugu au marafiki wa dhati, ndio ntolee tena.

Mara mtu anaanza kutembea mji mzima bila sababu, analala pasipojulikana. Lakini mwisho wa yote ni njaa. Njaa ndio inayowafanya wagonjwa wa akili waanze kuwa ombaomba, umalya au waingie kwenye mapipa ya takataka kuganga njaa. Na hali ikifikia hapo ndio mwisho Sasa.

Maana baada ya hapo kwa ughaibuni, madawa ya kulevya yanaingia (Crack cocaine au meth ndio matunda ya street life)..... yaani hapo ni Nusra za Mwenyezimungu ndio zitamuokoa mtu. Mwenyezimungu atuepushe sote na hili balaa.
Huyu ndugu zake wapo.uwa wanaenda kumchoma sindano.alipoambiwa amemchapa bakora rafiki yake amejisikia simanzi sana.anamuonea hadi aibu maana sio kwa bakora zile.swali moja ukikosa bakora moja alafu maswali yenyewe ya biblia na jamaa yangu ni muislam 🤣🤣🤣.kuna wapangaji wamehama mbona na yeye kapewa notisi kahama.sasa jiulize leo kaja na bakora siku nyingine si atakuja na panga itakuwaje?
 
Unatakiwa kuelewa mipaka yako na kuheshimu privacy ya mtu.

Kwanza umeenda kumrekodi bila ya ridhaa yake, unalazimisha kumpa msaada wa hela ambao auhitaji; halafu unamposti mitandaoni huo ni udhalilishaji.

Pili unalazimisha msaada kwa mtu ambae ajakuomba na hataki hiyo ni kuingilia rights zake. Dada anaonekana ni mzima maana unakiri umewahi kuongea nae na hata hapo kwenye video inaonekana anajielewa huo uchizi unampa wewe.

Tatu hujui changamoto zake za maisha hadi kua homeless, ungeanzia kudadisi hapo kimetokea nini kwenye maisha yake hadi kufikia alipofika.

Nne kama lengo ni kutaka ndugu zake wapate habari ungeweza anzisha mada kwa title yoyote na ku-crop sura yake tu na kuomba msaada kama kuna mtu anamfahamu huyo dada wakupe details za ndugu zake uwape taarifa, wao ndio wana mamlaka ya kwenda serikalini na kuomba msaada arudishwe.

Umemkosea sana huyo dada na kumdhalilisha.
Sasa wew unategemea huyo dada angefanyaje wakati unaona hali yake masuala ya privacy sidhani Kama yanamhumi kwa hali aliyonayo kikubwa msaada
 
Back
Top Bottom