DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Kitendo cha ku-post hiyo video, tena mwenyewe anamwambia niache sitaki; ame-violate kanuni kadhaa za afya na human rights naweza kukujazia uzi nikitaja zote.

Mambo mengine yanataka uelewa na experience ya maisha hayo mambo ni kawaida hata kwa wazungu wenyewe huko kwao kulała rough kipindi ambacho unashida na huna msaada.

You cant educate me shit. Save your energy for your metabolism and stuff.
 
Kitendo cha ku-post hiyo video, tena mwenyewe anamwambia niache sitaki; ame-violate kanuni kadhaa za afya na human rights naweza kukujazia uzi nikitaja zote.

Mambo mengine yanataka uelewa na experience ya maisha hayo mambo ni kawaida hata kwa wazungu wenyewe huko kwao kulała rough kipindi ambacho unashida na huna msaada.
Nadhani unafikiri ukionekana unachangia mambo ya Nje ya nchi utaonekana unajua kwanza toa maoni kiswahili tu kingereza ni lugha tu sio elimu hili neno privacy nadhani hata hujui maana yake au jinsi ya kulitumia nikujulishe Tena na watanzania kwa ujumla huyu dada Ana ugonjwa wa akili sisi Ndio tunamuona hakuna mgonjwa wa akili Unaweza kusema anamaamuzi pia usidhani wagojwa wa akili ni waiopo maporini tu kuna wengine humu kina privacy nao wanahitaji msaada 😂
 
Unatakiwa kuelewa mipaka yako na kuheshimu privacy ya mtu.

Kwanza umeenda kumrekodi bila ya ridhaa yake, unalazimisha kumpa msaada wa hela ambao auhitaji; halafu unamposti mitandaoni huo ni udhalilishaji.

Pili unalazimisha msaada kwa mtu ambae ajakuomba na hataki hiyo ni kuingilia rights zake. Dada anaonekana ni mzima maana unakiri umewahi kuongea nae na hata hapo kwenye video inaonekana anajielewa huo uchizi unampa wewe.

Tatu hujui changamoto zake za maisha hadi kua homeless, ungeanzia kudadisi hapo kimetokea nini kwenye maisha yake hadi kufikia alipofika.

Nne kama lengo ni kutaka ndugu zake wapate habari ungeweza anzisha mada kwa title yoyote na ku-crop sura yake tu na kuomba msaada kama kuna mtu anamfahamu huyo dada wakupe details za ndugu zake uwape taarifa, wao ndio wana mamlaka ya kwenda serikalini na kuomba msaada arudishwe.

Umemkosea sana huyo dada na kumdhalilisha.
Sema wakati mwingine mjitahidi kukaa kimya kuficha ubovu wa akili mengine yawapitege
 
Nadhani unafikiri ukionekana unachangia mambo ya Nje ya nchi utaonekana unajua kwanza toa maoni kiswahili tu kingereza ni lugha tu sio elimu hili neno privacy nadhani hata hujui maana yake au jinsi ya kulitumia nikujulishe Tena na watanzania kwa ujumla huyu dada Ana ugonjwa wa akili sisi Ndio tunamuona hakuna mgonjwa wa akili Unaweza kusema anamaamuzi pia usidhani wagojwa wa akili ni waiopo maporini tu kuna wengine humu kina privacy nao wanahitaji msaada 😂
Toa tafsiri ya ugonjwa wa akili tuanzie hapo.
 
Sasa wew unategemea huyo dada angefanyaje wakati unaona hali yake masuala ya privacy sidhani Kama yanamhumi kwa hali aliyonayo kikubwa
Wewe peke yako ndio unaishi ulaya kwenye hii mada.

Wakują utawajua tu
Nina hakina hujui unacho kisema ungekua huko ulaya unakosema ungejitambua pia jua tu Mimi siko ulaya 😂😂
 
Here to keep the tread alive. Even if it takes a million times quoting you.
Well then I am gonna keep giving you medical principles why the act is wrong.

Health is heirerachial you don’t just assume things are right nor just do things as you wish. There are guidelines.

What do you know about safeguarding the patient?
 
Nina hakina hujui unacho kisema ungekua huko ulaya unakosema ungejitambua pia jua tu Mimi siko ulaya 😂😂
Sina muda wa kujibizana na watu wanaodhani kuishi huko ni big deal.

Una arguments za position ya huyo dada na kwanini unadhani nakosea sawa. Iła wewe kuwa wapi duniani doesn’t interest me.
 
Well then I am gonna keep giving you medical principles why the act is wrong.

Health is heirerachial you don’t just assume things are right nor just do things as you wish. There are guidelines.

What do you know about safeguarding the patient?

Bring it on. It wont change an alphabet of the original content posted for the lady in need.
 
Balozi zetu za Tanzania huwa zinatuona wa maana Rais akiwa anataka kutembelea na wanataka twende kuonana nae ila zaidi ya hapo ni kutusisitiza tu kujaza taarifa zetu kwenye database yao basi. Kifupi ni kwamba hata ukiwa na shida wala usitegemee msaada wa aina yoyote ile kutoka ubalozini. Kwanza hata simu tu kupokea ni mpaka waamue.
 
Sasa wew unategemea huyo dada angefanyaje wakati unaona hali yake masuala ya privacy sidhani Kama yanamhumi kwa hali aliyonayo kikubwa msaada
Sijasema asimtafutie msaada lakini hakuwa na sababu ya kutuletea life story na kwenda kum-record anapolala chini ya daraja bila ya ridhaa yake.

Angeweza kufikisha ujumbe kwa njia nyingine labda kwa passport size photo na kuelezea kuomba wenye kumfahamu yeye au ndugu zake wamtafute.

Sio kuanza kumnyanyapaa kwanza ana mrekodi nina hela yako, dada mwenyewe anaonekana wala hana shida na hiyo hela. Anakuja humu anampa label ya uchizi wakati hana medical records zake wala hajui ana medical condition gani. Hiko kitendo ndio nipo against nacho huo ni udhalilishaji usio na lazima.
 
Mimi ni Mtanzania ninayeishi Marekani, kuna Mtanzania mwenzetu mbaye alikuja kama Mwanafunzi hapa, sijui vizuri kuhusu historia yake huko nyuma.

Miaka kadhaa iliyopita alipata changamoto ya Afya ya Akili, sijui nini kiliendelea baada ya hapo kati lakini kilichofuata amekuwa chizi na analala barabarani, amekuwa akifanyiwa ukatili wa kingono na Wanaume mara nyingi bila kuwa na msaada.

Nilienda Ubalozini mara kadha pia kuripoti ili ikiwezekana huyu Mtanzania asaidiwe lakini kinachoonekana wao (Ubalozi) ndio wanataka nianze kufanya kazi yao.

Wanataka kufuatilie na kujua details zaidi kuhusu huyo Mtanzania na mambo mengine kama hayo, mimi siwezi kuingilia hayo masuala ya wao, wenyewe ndio wataalam, mimi nikiwapa taarifa wanatakiwa kujua nini cha kufanya baada ya hapo.

Huyu mtanzania ninamfahamu kwa jina moja tu anaitwa Jane, mitaa ya Houston ndani ya Texas.

Maisha yake ni chini ya Daraja, amekuwa hivyohivyo akiishi chini ya Daraja.

Nilivyoanza kumjua
Kuna siku nikiwa na mke wangu kwenye bustani flani akasikia tunazungumza Kiswahili, akajumuika nasi na kuanza kuzungumza na kisha kujitambulisha.

Tukazungumza naye kwa Kiswahili na akajieleza naye anatoka Ukanda wa Kaskazini kama nilivyo mimi hapo nyumbani Tanzania.

Bahati mbaya nimesahau jina lake la pili na hata sas aukisema umuulie huwezi kupata jibu hilo.

Nimeshatoa picha zake mara kadhaa sehemu tofauti ili anayemjua iwe ni ndugu zake, jamaa au marafiki wamsaidie lakini sijafanikiwa katika hilo, ndio maana nimeona nitumie JamiiForums kufikisha ujumbe huu nadhani utawafikia wahusika na wanaweza kumsaidia.

Nipo tayari kuto ushirikiano kwa ambaye anaweza kuhitaji kumsaidia huyu au kama anawez kumtambua, nimewasilisha mawasiliano yangu kwa JamiiForums kwa mtu ambaye atahitaji kuwasiliana nami.
Umeonesha upendo na uzalendo wa hali ya juu....
 
Kwanza Hongera kwa. kufuatilia na kutoa taarifa. Nakushauri na kukuomba kwa kuwa mamlaka zina taarifa NENDA MCHUKUE USIMUACHE ADHALILISHWE KINGONO NA KIMWILIl na KIHISIA pia. Fanya hivyo. Lkn Wizara yetu husika IHUSIKE SASA KUPITIA UZI HUU. Roho moja ya Mtz ni bora kuliko kuleta muwekezaji
 
Sijasema asimtafutie msaada lakini hakuwa na sababu ya kutuletea life story na kwenda kum-record anapolala chini ya daraja bila ya ridhaa yake.

Angeweza kufikisha ujumbe kwa njia nyingine labda kwa passport size photo na kuelezea kuomba wenye kumfahamu yeye au ndugu zake wamtafute.

Sio kuanza kumnyanyapaa kwanza ana mrekodi nina hela yako, dada mwenyewe anaonekana wala hana shida na hiyo hela. Anakuja humu anampa label ya uchizi wakati hana medical records zake wala hajui ana medical condition gani. Hiko kitendo ndio nipo against nacho huo ni udhalilishaji usio na lazima.
Unafkiri bila kufanya hivyo watu wangeamini hilo analolisema....
And unapataje lidhaa kwa mtu mwenye matatizo ya akili tena uliyokuwa neglected.
 
Wizara ya Mambo ya nje should do more to protect and check the welfare of all Diaspora ....
Kama unashindwa kutafuta fursa za uwekezaji, atleast hata upande wa watz wenzetu muwajali.
 
Back
Top Bottom