DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

DOKEZO Mtanzania huyu alikuja Marekani kusoma, akapata changamoto ya Akili, sasa hivi anaishi Mtaani, anahitaji msaada

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Zile ni nchi wa watu, zina taratibu tofauti na kwetu, msamaria kaleta huku hii ni mara nyingine baada ya kufanya hadi jitihada za kuwasliana na balozi wa Tanzania nchini marekani toka 2018, amekutana naye tena labda ni mazungumzo aliyoona ayaanzishe ili aone kama huyo dada anaweza kuwa bado anaweza kuwasliana vizuri. Je ingekuwa ni wewe ungewezaje kuanza kuongea naye? Na mpaka kuleta clip yake hujaona ameshajitahidi kumsaidia ili apate msaada? Wewe unaweza chukua mtu mwenye tatizo la akili ukamweka kwako? Mnakuwaga wepesi kujudge kabla ya kufikiri kwa upande wake wewe ungefanyaje
Kulikuwa kuna umuhimu wa kuweka hio clip anayomrekodi bila ya ridhaa yake, na mambo ya nimekuletea hela yanatoka wapi kama kweli huyo ni kichaa, kichaa ana uwezo wa kutambua matumizi ya hela ?
Hujiulizi kwanini anamfukuza na anasisitiza aondoke ?
Wapi nimesema amchukue na kumuweka kwake?
Kuna njia nyingi za kumsaidia au na yeye anaishi kimagumashi ? anaogopa kwenda social services za homeless huko Houston kama ubalozi hawana msaada mbona nimegugo na kuziona zaidi ya 30 kwa haraka haraka ?
Niambie kumuweka hapa itasaidia nini ? tena kwa kutumia anonymous ID, kama wewe ndie ndugu yake uko bongo ungeaazaje kumtafuta mtu asiye na makazi maalumu kwa taarifa iliyoletwa na mtu ambaye hawezi tena kuchangia katika hii mada?
 
Unatakiwa kuelewa mipaka yako na kuheshimu privacy ya mtu.

Kwanza umeenda kumrekodi bila ya ridhaa yake, unalazimisha kumpa msaada wa hela ambao auhitaji; halafu unamposti mitandaoni huo ni udhalilishaji.

Pili unalazimisha msaada kwa mtu ambae ajakuomba na hataki hiyo ni kuingilia rights zake. Dada anaonekana ni mzima maana unakiri umewahi kuongea nae na hata hapo kwenye video inaonekana anajielewa huo uchizi unampa wewe.

Tatu hujui changamoto zake za maisha hadi kua homeless, ungeanzia kudadisi hapo kimetokea nini kwenye maisha yake hadi kufikia alipofika.

Nne kama lengo ni kutaka ndugu zake wapate habari ungeweza anzisha mada kwa title yoyote na ku-crop sura yake tu na kuomba msaada kama kuna mtu anamfahamu huyo dada wakupe details za ndugu zake uwape taarifa, wao ndio wana mamlaka ya kwenda serikalini na kuomba msaada arudishwe.

Umemkosea sana huyo dada na kumdhalilisha.
Wewe ni kenge
 
Kulikuwa kuna umuhimu wa kuweka hio clip anayomrekodi bila ya ridhaa yake, na mambo ya nimekuletea hela yanatoka wapi kama kweli huyo ni kichaa, kichaa ana uwezo wa kutambua matumizi ya hela ?
Hujiulizi kwanini anamfukuza na anasisitiza aondoke ?
Wapi nimesema amchukue na kumuweka kwake?
Kuna njia nyingi za kumsaidia au na yeye anaishi kimagumashi ? anaogopa kwenda social services za homeless huko Houston kama ubalozi hawana msaada mbona nimegugo na kuziona zaidi ya 30 kwa haraka haraka ?
Niambie kumuweka hapa itasaidia nini ? tena kwa kutumia anonymous ID, kama wewe ndie ndugu yake uko bongo ungeaazaje kumtafuta mtu asiye na makazi maalumu kwa taarifa iliyoletwa na mtu ambaye hawezi tena kuchangia katika hii mada?
Nadhan ndugu zake wakiona hii watawasiliana na uongozi wa jf kumpata uyo jamaa,kwa professional yangu uyu dada ana tatizo la afya ya akili anaitaji msaada wa aina yeyote then shit kweli zinahappen anaezaishi na madhara ya baada kuliko ivi trust me
 
January Makamba angekuwa ni mtu anayejali hakika huyu mtanzania angesaidiwa!
 
Hawa wanaotukana mleta uzi watakuwa hawataki hii habari iwafikie viongozi na ndugu wa huyo dada.
kwa kifupi tu ubalozi wa Tanzania Marekani hauna msaada wowote kwa watanzania wanaoishi huko ata ndugu Isanga family kuna uzi alizungumza hilo kuhusu balozi zetu.
 
Uwezi kuwa educated kwenye hii dunia kama kichwa chako umekifunga na unabisha tu bila ya kuelewa kanuni za afya zenye kupinga unyanyapaaji wa wagonjwa.

In this instance huyo Jane sio mgonjwa (maana humu ni shida people can’t distinguish between an hypothetical statement) and the actual view stance of the contributor. Mara utaona poyoyo mmoja si ulisema Jane mzima sasa tena mbona unasema mgonjwa. The nonsense with some people in this forum is beyond me.

Responsible media outlet wangeshaifuta hiyo video ya jamaa it is just insubordination and patronising nothing else .

Sasa huko kwenye lugha kama kijijini kwenu kizungu ni issue au wewe ndio wa kwanza kufika developed nation kwenye ukoo wenu; elewa huo umuhimu wa hivyo vitu ni kwenye chako tu sio vya wote humu JF.
Wewe sio tu mgwanjwa wa akili Bali Nikichaa wa kwenye mitandao ningeomba wana jamii forum mtaarifu ndugu wa huyu kiumbe nayeye anahitaji msaada kwani amechanganyikiwa kuliko hata Jeni mwenyewe du kumbe wagonjwa wa akili niwengi hivi🙆🏿‍♀️🙆🏿‍♀️🙆🏿‍♀️
 
Hawa wanaotukana mleta uzi watakuwa hawataki hii habari iwafikie viongozi na ndugu wa huyo dada.
kwa kifupi tu ubalozi wa Tanzania Marekani hauna msaada wowote kwa watanzania wanaoishi huko ata ndugu Isanga family kuna uzi alizungumza hilo kuhusu balozi zetu.
You're wasting your time and energy ktk kujadili utendaji kazi wa Balozi za Tanzania huko nje ya nchi. Kuna ushahidi mwingi sana unaothibitisha kwamba Balozi za Tanzania huko nje hazina faida yoyote Ile kwa wa-Tanzania na wala hazina msaada wowote ule kwa Raia wa Tanzania, sasa kwa nini bado mnaendelea kuzijadili???
 
Mh Dkt. Gwajima D Nafikiri umeupata ujumbe huu anaweza kusaidia sana kwenye hili pamoja liko kwa waziri mwingine lakini yeye kama Waziri kwenye maswala haya anahusika na watu wengi wanatarajia kutoka kwake kwakuwa yuko active sana humu na binafsi nimemtumia PM aje asome huu uzi ajue atamsaidia vipi huyu binti akishirikiana na Mh January Makamba pamoja na mabalozi kwani walio huko wametoa mawasiliano yao kwa Jamii forums hivyo waziri @Dkt.gwajima anayo nafasi ya kumsaidia huyo binti adiendelee kufedheheka na kudhalilishwa uko nchi za watu kwakweli ina sikitisha sana sana….yani miaka saba taifa lenye mabalozi na wamebadilishwa kila muda wanashindwa kumsaidia huyo binti? Dkt. Gwajima D Tunaomba ufatilie hili jambo ikiwezekana utuletee mrejesho maana hatuna wa kumuagiza zaidi yako maana wewe ndio tunakufikia kirahisi na ndio kimbilio letu…tuna hakika huyu binti lazima ana ndugu lakini kuna sehemu wana kwama tunaomba msaidie….
Cc Dkt. Gwajima D

@Mtagi Dk. Dorothy anaweza akasaidia
 
Hapana mkuu watu wamechangia kwa mahaba mda wa masaa 24 zikafika 10m
Kwanini tusiwe na ubinadamu wa kuchanga ili arudi nyumbani?
Niko tayari kwa msaada
Ni wazo zuri, lakini hizi nchi za wenzetu, huwezi kumshutisha mtu arudi nyumbani bila hiari yake. Sasa, ukiunganisha na maradhi ya akili ndio kabisa. Cha kwanza nadhani ni tiba halafu hayo mengine ndio yatafuata. Ni suala Tata sana lisilokuwa na majibu.
 
Mchawi Ndugu....!

Ni vita vya Kiroho..... Shetani anaongoza 1 - 0.....!
 
Back
Top Bottom