Mtanzania Joyce Msuya ateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mataifa Mazingira

Naaam, kitu cha Kipare hicho, Siku Malaika Mkuu akifika UN atamtimua.... Sijui lini?
 
Ulaya bana..! Mtu yupo na masters of science in microbiology amekuwa world bank special representative ukija bongo kuwa bank teller tu wanataka uwe na degree ya accountant..! [emoji25] [emoji25] [emoji25]
Degree ya account mshahara laki sita,bora nchi za wenzetu na makampuni makubwa wanangalia uwezo wako wanakupa nafasi.Kuna Dr mmoja alisoma Chemical Engineering marekani huku tz alifanya kazi kama mkuu wa masuala ya fedha na mipango kwenye Tasisi moja kubwa,nilichogundua wenzetu awangalii micheti wanangalia uwezo wako.
 
Hivi serikali ya Kenya haiwezi kumnyima kibali cha kufanya kazi akiwa Kenya?
Coz serikali ya Tanzania ilimnyima kibali yule wa vodacom katoka Kenya.
Ameshafanya kazi pia hapo Kenya kwa muda mrefu akiwa Benki ya Dunia
 
Huyu ni mtanzania kwa majina na asili tu,
Lakini kiuhalisia maisha yake yote amekuwa nje ya nchi tu ivyo huenda hata hana taarifa kuwa Tanzania ya leo tumefikia hatua ya kutawaliwa na."Jiwe"
 
Inashangaza kwamba hajawahi kufanya kazi Tanzania.Is it an oversight?Ila nadhani hajapitia kwenye mifumo ya elimu ya Tanzania,nadhani "ni mtu wao".Hata hivyo hongera zake
 
Tuna kichwa pale wizara ya fedha Mr. Mpango alikua huko World bank. Mpaka leo hatuoni matunda ya mipango yake. Bila Sera na utawala bora hata umlete nani sujui nae atakua Mipangoless.
Kumbe Mipango naye alikuwa World Bank.Kwa hiyo yuko hapo kulinda maslahi ya World Bank?Dah,hawa jamaa noma.
 
Ni yule aliyesoma Weruweru sec miaka ya nyuma au mwingine? Hongera kwa kuiwakilisha Tz
 
ms. msuya alaf married tena au lugha nimeelewa vibaya.
 
Hivi bila kujua Kingereza, hii position angeipata ..!!

Hii ya kujua Kingereza siyo kuelimika. ... awadanganye wengine!!
Kwa dunia ya leo hususan kwa nyanja za kimataifa kama taasisi za UN, kiingereza fasaha ni muhimu sana , ukiona mtu anakwambia lugha za kimataifa si muhimu, I can say he is not thinking beyond our borders, na lugha zinazotambulika rasmi kwa taasisi za UN ni kiingereza na kifaransa ukiwa na ufahamu na lugha nyingine zaidi ya hizo ni added an advantage kulingana na sehemu husika unayokwenda kufanyia kazi, ila baada ya kuona CV yake nikajiridhisha siyo zao la shule za kata na vyuo vyetu hivi vya baadhi ya Wahadhiri kutishia kuwala vichwa wanafunzi, na hii ni ishara ya kwamba kwa elimu yetu hii ya hapa nchini, we still have a long way to go, thnx and I concur with you!
 
immunology na Fedha wapi na wapi, au unadhan kujua kiingereza ndo kuujua uchumi?
Soma habari kwa utulivu uone posts alizowahi kushika katika nyanja za kimataifa usikurupuke tu. Utajisaidia chini kwa haraka zako wakati choo kipo mbele yako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…