Anonymous
Senior Member
- Apr 6, 2006
- 118
- 339
Wakuu,
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda, ametakiwa kuenda likizo kwa lazima kwa ajili ya kupisha uchaguzi Mkuu unaotegemewa kufanya Oktoba 25, 2015.
Imebainika kuwa sababu kubwa itakayotolewa na ndugu Kibanda ni kuwa anaenda kwenye matibabu nje ya nchi.
Aidha Mhariri Mwandamizi, Kulwa Karedia, ataenda likizo ya lazima kwa kipindi hicho na nafasi za wawili hao zitachukuliwa na ndugu, Michael Mande amabaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyegombea kura za maoni za ubunge kwa tiketi ya CCM na kuanguka huko Masasi.
Kwa hali ilivyo sasa, haijulikani ninani yuko nyuma ya hili jambo, ninaendelea kufuatilia sakata hili kwa karibu zaidi, pindi nitakapopata taarifa kamili nitawajulisha.
Itakumbukwa kuwa Kibanda kwa muda mrefu sasa amekuwa mtu wa karibu na Mgombea Urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa, tangu alipotangaza kujiunga na chama hicho.
Asante..
=========
UPDATE:
JamiiForums imeongea na Absalom Kibanda (ambaye pia ni mwanachama wa JamiiForums), amekiri kuna jambo kama hili lakini akasisitiza lipo tofauti na lilivyoandikwa hapo juu. Ataingia JF kufafanua akipata muda lakini kasisitiza kuwa yeye hajalazimishwa kwenda likizo bali kaamua kukaa kando kwa muda.