Mtanzania kwafukuta, Absalom Kibanda kupewa likizo ya lazima kupisha uchaguzi Mkuu

Mtanzania kwafukuta, Absalom Kibanda kupewa likizo ya lazima kupisha uchaguzi Mkuu

Owner sio Manji? Manji ni.ukawa au ccm? Ccm.i.think. Mtanzania limenunulika sana kwa kuandika ukweli. Kama watachange wahesabu maumivu kununulika
 
Owner sio Manji? Manji ni.ukawa au ccm? Ccm.i.think. Mtanzania limenunulika sana kwa kuandika ukweli. Kama watachange wahesabu maumivu kununulika

Mbona mnatuchanganya wakuu mara la Manji mara Rostam, mmiliki halisi ni nani?
 
Wakuu,

Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda, ametakiwa kuenda likizo kwa lazima kwa ajili ya kupisha uchaguzi Mkuu unaotegemewa kufanya Oktoba 25, 2015.

Imebainika kuwa sababu kubwa itakayotolewa na ndugu Kibanda ni kuwa anaenda kwenye matibabu nje ya nchi.

Aidha Mhariri Mwandamizi, Kulwa Karedia, ataenda likizo ya lazima kwa kipindi hicho na nafasi za wawili hao zitachukuliwa na ndugu, Michael Mande amabaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyegombea kura za maoni za ubunge kwa tiketi ya CCM na kuanguka huko Masasi.

Kwa hali ilivyo sasa, haijulikani ninani yuko nyuma ya hili jambo, ninaendelea kufuatilia sakata hili kw akaribu zaidi, pindi nitakapopata taarifa kamili nitawajulisha.

Itakumbukwa kuwa Kibanda kwa muda mrefu sasa amekuwa mtu wa karibu na Mgombea Urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa, tangu alipotangaza kujiunga na chama hicho.

Asante

=========
UPDATE:

JamiiForums imeongea na Absalom Kibanda (ambaye pia ni mwanachama wa JamiiForums), amekiri kuna jambo kama hili lakini akasisitiza lipo tofauti na lilivyoandikwa hapo juu. Ataingia JF kufafanua akipata muda lakini kasisitiza kuwa yeye hajalazimishwa kwenda likizo bali kaamua kukaa kando kwa muda
Mkuu Anonymous, kwanza asante kwa habari kama hii, toka jikoni kabisa!, unaonyesha wewe uko mule mule kunako, sasa for curiosity tuu, why toka Join Date : 3rd February 2006, hadi leo, umePosts : 11 tuu?!.

Hili la kupunzishwa Kibanda iwe ni likizo or not, hata lisinge tokea sasa, lingetokea tuu baada ya October 25!, kwa sababu kwa maoni yangu, huyu ndiye ata head ile Kurugenzi!.

Lowassa anaingia Ikulu kwa ulaini kama kumsukuma mlevi!, no one can stop him!.
Pasco
 
Ushauri kwa waandishi wa habari! Jaribuni kusoma vitu kabla hamjaandika mambo! Kumeungia kasumba ya kuandika vitu kwa ushabiki na kujifanya mnajua kila kitu!

Taarifa ya PPRA mliipindisha sanaa na najua tatizo ni kutojua sheria ya ununuzi na kanuni zake na pia kutojua kusoma report!

Kibanda huyo kwenye gazeti lake la mtanzania kama mhariri aliandika uongo mkubwa kisa tu kumchafua Magufuli kuhusu ukaguzi ndani ya wizara ya ujenzi.

Ujuaji na kupenda bahasha utatufikisha pabaya! Taifa haliwezi kuendelea kwa kuwa na waandishi wanaondeka kuandika mambo bila hata kufanya tafiti!

Taifa hili litaangamia kwa vijana mnaopenda kuendesha vigari vidogo mjini msivyojua vinatoka wapi! Jengeni Nchi! Wazee wanawatumia vibaya!
 
ImageUploadedByJamiiForums1444680513.839321.jpg
 
Katiba ipi inaruhusu uanzishwaji wa hiyo mahakama?

Kati ya mafisadi 11 waliotangazwa Mwembeyanga, 10 wapo CCM akiwemo JK, hiyo mahakama itakuwa ni kwa ajli ya hao!
Hiyo mahakama ipo ilianzishwa na Nyerere tangu mwaka 1984, ukimsikiliza mgonjwa wa akili amtafananishwa akili, muulize mwanasheria anayepractise law atakueleza, siyo wanasheria aina ya Riziwani wanaojuwa wizi na mlango wa mahakama hawajawahi kukanyaga.
 
Mkuu Anonymous, kwanza asante kwa habari kama hii, toka jikoni kabisa!, unaonyesha wewe uko mule mule kunako, sasa for curiosity tuu, why toka Join Date : 3rd February 2006, hadi leo, umePosts : 11 tuu?!.

Hili la kupunzishwa Kibanda iwe ni likizo or not, hata lisinge tokea sasa, lingetokea tuu baada ya October 25!, kwa sababu kwa maoni yangu, huyu ndiye ata head ile Kurugenzi!.

Lowassa anaingia Ikulu kwa ulaini kama kumsukuma mlevi!, no one can stop him!.
Pasco

Pasco nilichokiona Mwanza leo kama CCM hawataki kukabidhi madaraka kwa amani nchi itaingia vitani, CCM inabidi wapelekewe jopo la consultant wa namna ya kufanya power end over deal in peace, na siyo majopo ya mshirikina January kucheza na hisia za Watanzania ambao tayari wameshafanya maamuzi wanasubiri kudumbukiza tu, otherwise hakuna haja ya kupoteza pesa kufanya uchaguzi.

Ati leo chama kinamtegemea kipofu Mpanju awaeleze watu wenye macho maendeleo!!.........
kwa vituko kama hivi andika neno maccm tuma kwenda namba 2015 utapata vichekesho bure.
 
India ndio destination ya watalii wa muda mrefu na mfupi kutoka tz..
 
That move is late... Watu wameshaamua muda mrefu na mambo kama hayo kwa mtazamo wangu ndio yanaweza kupunguza kura zaidi kwa ccm.
Ccm wanashindwa kabisa kuzichanga karata zao vema.. Mfano wanapoamua ivi sasa kumtumia mtu kama Mkapa ambae alishawatusi watz pale mwanzo na watu walishaanza kusahau hawaoni kabisa kuwa that's a negative move.
 
Wakuu,

Ni dhahiri kabisa ndugu yetu mpenda haki na usawa bwana Absalom Kibanda amepewa likizo ya lazima, ili awekwe kada wa CCM alietokea Mtwara UVCCM. Nimeona kwenye mtandao gazeti hili limeandika kuwa membe kazungumzia kifo cha Balali,
Na kwanini wasingeandika membe:"iwe isiwe lazima tushinde tusiposhinda tutakutana msituni na Lowassa."

Nataka niwaeleweshe wanaccm ambao mliitwa mavuvuzela na babu kingunge.lowasa hakusema atamleta balali bali alikuwa anawaquote wananchi waliokuwa wanapiga kelele kumtaka balali.gazeti hili la mtanzania limekuja na kwa speed ya ajabu ya kutetea ufisadi wa ccm ikiwa ni siku moja tu tangu mpenda haki absalom kuachia ofisi.

Sasa nasema hivi wananchi walishaamua hata mnunue vyombo vyote vya habari lakini kura wanampa Lowassa

CCM ni jopo la mafisadi
 
Sasa Hapo Unalalamika Nini?Mbona Gazeti La Mwananchi Lilivoandika "Magufuli Akutana Na Nguvu Ya Ukawa" Mbona Mlifurahia?Inamaana Hakukua Na Habari Nyingine Zaidi Ya Ile?Nalo Mwananchi Tuseme Linatumika/limenunuliwa Na Ukawa??
 
yes ni kweli kibanda yupo likizo ya lazima ss ni ccm mwendo mdundo...ila too late
 
wakuu ni dhahiri kabisa ndugu yetu mpenda haki na usawa bwana absalom kibanda amepewa likizo ya lazima,ili awekwe kada wa ccm alietokea mtwara uvccm.nimeona kwenye mtandao gazeti hili limeandika kuwa membe kazungumzia kifo cha balali,
Na kwanini wasingeandika membe:"iwe isiwe lazima tushinde tusiposhinda tutakutana msituni na lowasa."

Nataka niwaeleweshe wanaccm ambao mliitwa mavuvuzela na babu kingunge.lowasa hakusema atamleta balali bali alikuwa anawaquote wananchi waliokuwa wanapiga kelele kumtaka balali.gazeti hili la mtanzania limekuja na kwa speed ya ajabu ya kutetea ufisadi wa ccm ikiwa ni siku moja tu tangu mpenda haki absalom kuachia ofisi.

Sasa nasema hivi wananchi walishaamua hata mnunue vyombo vyote vya habari lakini kura wanampa lowasa

Ccm ni jopo la mafisadi

Kulialia huku ni dalili ya maji kuwa shingoni..
Huna hoja ya msingi.
Huwezi lipangia gazeti habari ya kuchapisha.
Ungeweza kulalamika kama gazeti limeandika habari za uongo.

"Shut up.
Na kama unaushahidi peleka mahakamani au MCT."
 
Sasa Hapo Unalalamika Nini?Mbona Gazeti La Mwananchi Lilivoandika "Magufuli Akutana Na Nguvu Ya Ukawa" Mbona Mlifurahia?Inamaana Hakukua Na Habari Nyingine Zaidi Ya Ile?Nalo Mwananchi Tuseme Linatumika/limenunuliwa Na Ukawa??
Gazeti la Mwananchi limenunuliwa, hivyo ni msaliti...!
 
Wakuu,

Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda, ametakiwa kuenda likizo kwa lazima kwa ajili ya kupisha uchaguzi Mkuu unaotegemewa kufanya Oktoba 25, 2015.

Imebainika kuwa sababu kubwa itakayotolewa na ndugu Kibanda ni kuwa anaenda kwenye matibabu nje ya nchi.

Aidha Mhariri Mwandamizi, Kulwa Karedia, ataenda likizo ya lazima kwa kipindi hicho na nafasi za wawili hao zitachukuliwa na ndugu, Michael Mande amabaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyegombea kura za maoni za ubunge kwa tiketi ya CCM na kuanguka huko Masasi.

Kwa hali ilivyo sasa, haijulikani ninani yuko nyuma ya hili jambo, ninaendelea kufuatilia sakata hili kwa karibu zaidi, pindi nitakapopata taarifa kamili nitawajulisha.

Itakumbukwa kuwa Kibanda kwa muda mrefu sasa amekuwa mtu wa karibu na Mgombea Urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa, tangu alipotangaza kujiunga na chama hicho.

Asante..

=========
UPDATE:

JamiiForums imeongea na Absalom Kibanda (ambaye pia ni mwanachama wa JamiiForums), amekiri kuna jambo kama hili lakini akasisitiza lipo tofauti na lilivyoandikwa hapo juu. Ataingia JF kufafanua akipata muda lakini kasisitiza kuwa yeye hajalazimishwa kwenda likizo bali kaamua kukaa kando kwa muda.

Mwaka huu kitaeleweka hata nchi ikibakia bila chombo cha habari lowasa tunampa kura 16million na tutalinda kura zetu 200 metres
 
Hata ikibakia tbc pekee lowasa hana mpinzani
 
Back
Top Bottom