Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Nimepata taarifa za ndani kuwa mambo si shwari pale New Habari tangu gazeti la Mtanzania liliporipoti habari yenye kichwa cha habari cha Madudu ya Serikali.
Habari hiyo ilikuwa na ripoti za ufujaji wa pesa za umma na utendaji mbovu wa serikali inayomaliza muda wake, huku Wizara ya Ujenzi ikivurunda zaidi.
Kwa mara ya kwanza habari hiyo ilichapishwa kwenye Mtanzania lakini gazeti likadhibitiwa ili kutosambaa, lakini kwa kuwa Mtanzania huchapishwa katika mitambo ya Mwanza, gazeti hilo lilisambaa kanda ya ziwa.
Kutokana na hilo, wahariri wa Mtanzania wakakubaliana kuirudia habari hiyo siku iliyofuata, lakini taarifa zikafika kwa JK kabla gazeti kuingia mtamboni.
JK akaamua kuwasiliana na RA na kumuuliza hiyo ya gazeti la kesho ndio zawadi ya birthday? Kwani kesho yake ilikuwa ni birthday ya JK.
Kutokana na hilo ikabidi RA avute waya na kuongea na wahariri wake kwa kuwaagiza kuiacha habari hiyo na kupunguza kumuandika vizuri EL na kumpa nafasi JM.
Wahariri walikubali kuitoa habari hiyo, na katika kikao chao wakaamua kutoandika kabisa habari za kampeni za uchaguzi, kwani walipinga kuingiliwa kazi yao.
Baada uamuzi huo gazeti la Mtanzania likaporomoka sana kimauzo, hali iliyofanya kuwe na mvutano juu ya kurejea katika habari za kampeni, mwishowe kuna mhariri mmoja akasimamishwa na kupitishwa agizo toka juu kuwa lazima waandike kampeni na watoe nafasi kubwa kwa JM. Agizo hilo likafanyiwa kazi pamoja na kuwekwa mabango katika gazeti la Dimba.
Kwa bahati mbaya mauzo yakashuka sana ikilinganishwa na wakati ambao picha za EL zilikuwa zinapata nafasi kubwa ukurasa wa mbele, hivyo uongozi wa juu ukaamini jopo la wahariri linahujumu ili kushusha mauzo.
Wakati ukweli ni kwamba habari za kumpamba JM zimekuwa hazifanyi vizuri kimauzo.
Sasa wakati huu nimepata taarifa kuwa Absalom Kibanda, Kulwa Kaledia na Arodia Peter wamesimamishwa.
Ova
PIA, SOMA: