TANZIA Mtanzania Mansoor Daya Afariki Dunia, alianzisha kiwanda cha kwanza cha Madawa Afrika Mashariki 1962

TANZIA Mtanzania Mansoor Daya Afariki Dunia, alianzisha kiwanda cha kwanza cha Madawa Afrika Mashariki 1962

Ukisikia Obama kawa Rais huko Marekani unakata hadi mauno kushangilia. Nikiwaambiwa hakuna race inaongoza kwa ubaguzi hapa duniani kupita mtu mweusi mnanibishia.

Mtu mweusi angekuwa na uchumi mzuri hakuna rangi race nyingine wangeacha kuona.
Hakika mkuu ukitaka kujua hili angalia watu weusi wenye fedha na madaraka ya juu utapata picha.
 
Mtanzania 🙄


Mtanzania Mansoor Daya amefariki dunia jijini Dar es Salaam. Daya alikuwa mtu wa kwanza nchini kufungua kiwanda cha madawa Tanzania na Afrika Mashariki mwaka 1962 akianza kwa kuziuzia nchi jirani na baadae akaanza kuuza kwenye soko la ndani.

Mpaka anafariki dunia alikuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya 'Mansoor Daya Chemicals Limited. Kiwanda chake kimekuwa kinazalisha madawa kwa miaka 60 na sasa kina uwezo wa kuzalisha tembe milioni 3 kwa shift moja.

Wateja wake wakubwa ni MSD, mahospitali na cliniki mbalimbali Tanzania na kinachagiza juhudi za kufikia mpango wa Serikali kuhakikisha Tanzania inaagiza chini ya 50% ya dawa zote zinazotumika nchini kufikia mwaka 2030.
Kanjibai
 
Sema huyo Mhindi sijui alisalimika vipi lakini Nyerere hao wahindi ndiyo aliwakomesha kweli kwa uchache tu pale Buguruni kwa Bakhressa kiwanda kilikuwa cha Mhindi.

Halafu kiwanda cha mabati kilikuwa cha Mhindi na Maghorofa yote yale ya kizamani kuanzia Kariakoo, Upanga na Kisutu kote alitaifisha zilikuwa za Wahindi.
Aliwakomesha?
Majengo ya NHC yameoza, hao wahindi wamejenga makubwa zaidi tena.
Viwanda alivotaifisha Nyerere vimekufa, wahindi wame bounce back, wamejenga viwanda vikubwa zaidi.
Huwezi kuua resilience ya wahindi!
 
Aliwakomesha?
Majengo ya NHC yameoza, hao wahindi wamejenga makubwa zaidi tena.
Viwanda alivotaifisha Nyerere vimekufa, wahindi wame bounce back, wamejenga viwanda vikubwa zaidi.
Huwezi kuua resilience ya wahindi!
Mwafrika mtanzania anachojua ni uwizi tu na ufisadi
Anaiba mihela mingiii anakula yeye na familia yake na vimada zake

Ova
 
Ushawahi kumsikia mtu mmoja anaitwa Azim Premji? Nina imani unamjua Jenerali Ulimwengu, hawa walizaliwa hapahapa Tanzania mmoja kazaliwa Dodoma na mwingine kazaliwa Kagera walizaliwa miaka mingi tu iliyopita kabla uhuru yaani walikuwepo kwa zaidi ya hiyo miaka 5 unayosema lakini kufika miaka ya 1990's ilibainika sio Watanzania na ikabidi waombe uraia wa Tanzania.
Inawezekana walipoteza uTanzania wao kwa kuwa raia wa nchi nyingine.
 
Inawezekana walipoteza uTanzania wao kwa kuwa raia wa nchi nyingine.
Siyo kama walipoteza uTanzania wao bali hawakuwahi kuwa Watanzania kabisa kwa sababu baada ya uhuru wageni wote walitangaziwa ama wawe na vibali vya ukaazi ama waukane uraia wa nchi zao walikotoka ili wawe Watanganyika lakini hao wazazi wao hawakuwahi kuukana uraia wao ili wawe Watanganyika wala hawakuchukua vibali vya ukaazi hivyo wakawa ni wahamiaji haramu hivyo na hao watoto wao automatically hawakuwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom