Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Mgombea Ubunge Jimbo la Ismani Emmanuela Mtatifikolo ameendelea na kampeni katika Kata ya Mlenge ambapo amewaahidi wananchi wa Kata hiyo kuwa endapo wakipiga kura za ndiyo na kuchagua Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika Juni Mosi, 2026 atatafuta Wawekezaji kwaajili ya Ujenzi wa Kiwanda cha Sukari kitakachosaidia kukuza uchumi wa Wananchi wa Mlenge kupitia kilimo cha Miwa.