Kwenye andiko hili, ukisimama na fikra huru, ukawa mtumwa wa nafsi yako uloyopewa na Mungu, sidhani kama kuna mahali utapinga.
Kiongozi yeyote anayezuia uhuru wa watu na vyombo vya habari, usijiulize ana maovu gani, itoshe tu kusema ni LAZIMA ATAKUWA KIONGOZI MWOVU.
Kama tunajutia mahali serikali ya awamu ya 5 ilitifikisha, kila asiye mnafiki apiganie kufutwa kwa sheria gandamizi na mabadiliko ya sheria yaliyofanywa na awamu ya 5.
Sheria zote zilizotungwa wakati wa awamu ya 5, na mabadiliko yote, yafutwe kwa sababu zilitengenezwa kukiwa na dhamira mbaya ya kutaka kuwakomoa watu.
Tupate katiba mpya itakayoweka mazingira yanayozuia kabisa mtawala kuuburuza umma na kukiuka misingi ya katiba ambayo Taifa limeweka.