John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Uongozi wa Klabu ya Simba umetoa pole kwa aliyewahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Hassan Dalali kufuatia ajali aliyoipata Jumatatu Machi 7, 2022 jijini Dar es Salaam.
Dalali alianguka na Bodaboda aneo la Rangi Tatu njia ya kuingilia Chamanzi, polisi ndiyo waliomtambua baada ya kumfikisha kituoni, na baadaye alikimbizwa Hospitali ya Mbagala Zakiem.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ametoa pole na kumuombea kheri kiongozi huyo wa zamani.
Ahmed amesema walishutushwa na taarifa za ajali iliyomkuta Hassan Dalali, na wamekua bega kwa bega na familia ya mzee huyo ambaye bado ana mapenzi ya dhati ya klabu ya Simba SC.
“Tupo pamoja na familia ya Mzee Dalali katika kipindi hiki ambacho ni kigumu kwake, tunaamini Mungu atamuwezesha kuwa na afya njema na kurejea katika majukumu yake,” amesema Ahmed Ally.
Mzee Dalali, alipata ajali ya kuangushwa na Bodaboda kwenye korongo, akitokea Uwanja wa Benjamin Mkapa, kushuhudia timu yake ikicheza dhidi ya Dodoma Jiji, Jumatatu (Machi 09).
Source: Wasafi FM