ngome1838
JF-Expert Member
- Feb 20, 2019
- 2,027
- 2,490
Suala la kuoa ni nyeti sana na zaidi mhusika ama wahusika, tunachofanya ni kutoa ushauri tu, mengine atajua mwenyewe kwani liko kibinafsi zaidi.Mada iko nyepesi kabisa vijana wakiume tukimbilieni darasa la Saba au kidato Cha nne aliyeshindwa Kwan wengi wao ndo wake sahihi ukimkuta mwenye dini
Msichana wa chuo kikuu anaamini ndo Ni smartphone na kuweka bando tu kucheki sinema.
Wanajua out Mara zawad eeeh za kitoto kbs lkn
Hawawez hata kukaanga mihogo maana wanataka biashara za vyumba vya kukodi.
Ushaur wangu
Vijana mkubali kufa na utam wako kulko kutfta mke wa chuo kikuu utajuta ndugu,waacheni hao waolewe na elimu zao!?
Kwa kuwa hakuna kigezo kimoja cha kuoa au kutaka kuolewa kwani unaweza ukasema ni Kijiji ndo pahala sahihi lakini bado pia ukaingia mkenge, unaweza kusema asiyezaa kabla bado ukajuta, unaweza ukasema asiye na elimu bado pia ukawa umeingia Chaka, unaweza ukasema mcha Mungu, nani anamjua mcha Mungu isipokuwa Mungu pekee?
Unasema mcha Mungu kumbe ni mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo,unaweza ukasema mweusi na mrefu bado ukakuta ni jehanamu.Suala la kuoa au kuolewa ni vema ukaomba sana Mungu, kibinadamu ni ngumu hasa katika nyakati hizi ambazo wazazi au walezi hawashiriki kuwachagulia wahusika wenza kwani jamii imebadilika sana.Vijana wapo mjini wakiwa wanafanya kazi kama sio vibarua huku wazazi wapo Kijiji na hata huko kijijini watu wako "so mobile".
ZAMA HIZI KUOA NI MTIHANI MGUMU KULIKO WA HESABU.