Mtazamo binafsi: Wasichana wengi waliomaliza vyuo vikuu ni mizigo na hawafai kuolewa!

Mtazamo binafsi: Wasichana wengi waliomaliza vyuo vikuu ni mizigo na hawafai kuolewa!

Hiv umefkria ulichoandika ama ulikutana. Na mwanachuo mmoja tu ndo umeamua utusemee ,wakituacha utatuoa wewe ??? Dah kwakweli eeh mbegubora
Mada iko nyepesi kabisa vijana wakiume tukimbilieni darasa la Saba au kidato cha nne aliyeshindwa Kwani wengi wao ndo wake sahihi ukimkuta mwenye dini.

Msichana wa chuo kikuu anaamini ndo ni smartphone na kuweka bando tu kucheki sinema.

Wanajua out Mara zawadi eeeh za kitoto kabisa lakini hawawezi hata kukaanga mihogo maana wanataka biashara za vyumba vya kukodi.

Ushauri wangu
Vijana mkubali kufa na utamu wako kuliko kutafuta mke wa chuo kikuu utajuta ndugu, waacheni hao waolewe na elimu zao!?
tu
 
Kwahiyo tushindwe kusoma na kuwa na hizo PHDs sababu hatutakua wife materials? Aargh mkuu tuache utani tabia ya mtu hategemei sana elimu yake mtu anaweza fika chuo ila akawa mstaarabu na yule std 7 akawa na tabia mbaya ajabu. Suala la mke na mume ni kuomba tu ukutane na mtu mnayependana bila kujali elimu na exposures.
Bora umemwambia ,ye akipata mtoto wa kike sjui asimsomeshe . wanaume wajifunze kuwa na akiba ya maneno .
 
Mama mlezi wa familia sasa iko hivi
MAMA KILAZA WATOTO JE
Mtakavyoendelea kuishi mtafanana basi bana nae atakua ma akili ua mama nae ni kilaza
KILAZA,KILAZA=KILAZAAAA
 
Mada iko nyepesi kabisa vijana wakiume tukimbilieni darasa la Saba au kidato cha nne aliyeshindwa Kwani wengi wao ndo wake sahihi ukimkuta mwenye dini.

Msichana wa chuo kikuu anaamini ndo ni smartphone na kuweka bando tu kucheki sinema.

Wanajua out Mara zawadi eeeh za kitoto kabisa lakini hawawezi hata kukaanga mihogo maana wanataka biashara za vyumba vya kukodi.

Ushauri wangu
Vijana mkubali kufa na utamu wako kuliko kutafuta mke wa chuo kikuu utajuta ndugu, waacheni hao waolewe na elimu zao!?
Kwa imani hizi za kijinga,wewe hauna Elimu ya juu,nchi ina watu Millioni 50,vyuo Vinatoa wahitimu wa kike zaidi ya laki 600 kwa mwaka,surely haiwezekani wote wawe hawafahi kuwa wake,na kuolewa.uoe kasichana ka darasa la saba,kanakoamini lazima kaende kushinda kanisani kwa mwamposa Ili maendeleo yaje,

Wanawake wote wanaotoka kwa mwamposa jumapili kuelekea Mbagara,bunju,bagamoyo,wengi wao ni darasa la saba,wanaamini watapata maendeleo wakija kupakwa mafuta na "nabii"upuuzi mtupu.

Mabinti wasomi,wapo wanachapa kazi,kama wewe ni mkazi wa Dar,nenda pale tegeta,wazo hill jioni uone wasomi wa kike wakiwa wanatoka kuchapa kazi,ukiingia pale kiwandani,utaamini,wanawake wanafanya welding,wanatengeneza mitambo,wanajenga,civil works,

Kama ni mkazi wa Arusha,fika kisongo kiwanda Cha nguo Ato Z,uone mabinti wanaojitambua,. Wakati wa darasa la saba wanakimbilia kwa mwamposa kulamba chumvi,wale wa vyuo vikuu,wapo kwenye ndinga zao,wanaenda site kucheki ujenzi wa mahekalu,hao wa darasa la saba utaowaonea huruma ikifika jioni,wanarudi mbagara,vitoto mgongoni,wanagombea daladala.

Wewe maskini,unaenda kuoa maskini,maanake watoto wako watakuwa na wajomba maskini,mama wadogo maskini,acha ujinga.
 
Mpuuzi kweli kweli. Unafikiri kila mtu ana mawazo ya kukaanga mihogo tu. Poor mindset. Halaf wewe ni mwanaume kamili kweli? Majukumu yako unataka yafanywe na mke? Kaoe huyo ambaye hana Elimu kwakua huyo ndo anafit kwenye maisha yako. Upeo wako usitake limit wengine. Na si lazima wote tuanze kwa kuuza genge. You can start with a supermarket. Or else tuwachome na petrol tu. Mnapenda mtelezo sana. Wewe mke bora kwako ni yule mwenye ajira. Je wewe ukipotexa hiyo ajira mke akuache siyo?
Mkuu msituchome bana. Ila mwamba ana mentality ya kiwango cha vumbi. Kila mtu aoe mwanamke anaeona wana common interests. Ila mkiwa mna uelewa wote kuna happiness flan hivi unaipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada iko nyepesi kabisa vijana wakiume tukimbilieni darasa la Saba au kidato cha nne aliyeshindwa Kwani wengi wao ndo wake sahihi ukimkuta mwenye dini.

Msichana wa chuo kikuu anaamini ndo ni smartphone na kuweka bando tu kucheki sinema.

Wanajua out Mara zawadi eeeh za kitoto kabisa lakini hawawezi hata kukaanga mihogo maana wanataka biashara za vyumba vya kukodi.

Ushauri wangu
Vijana mkubali kufa na utamu wako kuliko kutafuta mke wa chuo kikuu utajuta ndugu, waacheni hao waolewe na elimu zao!?
Mimi nitaoa mwenye degree yake
 
Nasema hivi..mimi binafsi nimelelewa na mama alieishia darasa la saba. Lakini ni mama bora sana na ametulea katika njia nyoofu tena alikuwa mkali kweli. Hata watu wa nje wakija wanasema dah bi mkubwa si mchezo.

Pamoja na hayo amesimamia elimu zetu mwanzo mwisho sisi kama mabinti. Akahakikisha pamoja na yeye kutokusoma sisi tuwe wanawake wasomi wanaojitambua. Tukifunga shule nyumbani kazi kama kawaida tena zifanyike kwa ustadi. Hakukuwa na cha house girl wala poo.

Akasema mimi sijasoma na nyie msisome hapana kwahyo anatambua fika juu ya elimu kwa mtoto wa kike. Kinachoendelea saivi katika dunia ni inferiority complex kwa watoto wa kiume coz hawajui kitu bora ni kipi. Mke mwema ni Mungu tu anamjua, wewe kazi yako kuchagua mwanamke huku unaisikiliza sauti yake kwamba huyu yes huyu no..na Mungu hawezi kuacha kukushauri sema tu hakuna anaemsikiliza.

Wengi wenu wanaume mnakuwa na vigezo vyenu kwenye makaratasi katika kuchagua mke. Kumbe Mungu anajua what you need not what you want. Msipotuliza akili katika kumsikia Mungu anasema nini mkatumia mioyo yenu idanganyayo, hakika mtaula wa chuya.

#niushaurituwapendwa#
 
Mimi nitaoa mwenye degree yake

Ndoa haina kanuni, kuna waliooa wenye degree na maisha yanaenda safi kabisa , kuna waliooa la saba wakiamini kwa level yao ya elimu watakua submissive lakini wakakuta patupu. pia kuoa mke uliyemzidi sana elimu ni tabu. Mnapishana sana kwenye uelewa na uwezo wa kuchanganua mambo. Ukimkosoa ataona unamdharau sababu umemzidi elimu, wengi wao upeo wa kufikiri upo chini. Elimu inasaidia kufuta ujinga, wengi wao wako na ka ujinga flani hivi kwenye mindset zao
 
Nasema hivi..mimi binafsi nimelelewa na mama alieishia darasa la saba. Lakini ni mama bora sana na ametulea katika njia nyoofu tena alikuwa mkali kweli. Hata watu wa nje wakija wanasema dah bi mkubwa si mchezo.

#niushaurituwapendwa#

Wanaulizana wao kwa wao kama huyu demu anafaa ama la, wanaacha kuuliza toka kwa Mungu aitazamaye mioyo. Wakiangukia pua wanaanza kulaumu wasomi.
 
Leo jamaa angu kanimbia Kuna demu wa kichaga demu anamkubali mno mchiz ingawa Ana mtu wake yule demu juz demu. Kaleta iPhone kumpa jamaa ili kusema kule kwa mshikaji wake yaani mtu wake kuwa simu imeibiwaa ili anunuliwe sumsung ..jamaaa Ni muhasibu wa bodi flni uko Moshi
 
Mkuu msituchome bana. Ila mwamba ana mentality ya kiwango cha vumbi. Kila mtu aoe mwanamke anaeona wana common interests. Ila mkiwa mna uelewa wote kuna happiness flan hivi unaipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaan kusoma ni kosa kweli? Ilihali maandiko yanasisitiza mshike sana Elimu usimwachie? Hili jamaa la wapi arifu? Marioo kila mahali. Lazima tuwabanike aisee... sasa huyo ambaye hajaenda shule kazi yake ndo housewife?

Asante Mungu kwa wazee wangu hawakua masikini hivi wa kifikra. Yaani mimi nikakaange mihogo saa hizi? Hapana. Watu tunataka vitu vikubwa. Na siyo dhambi kuota mambo makubwa zaidi. Bado sijawaza hilo baba. Na Mungu aninyime mume kama huyu. Pooh mbaka
 
Atakua na mawili, inferiority complex hata kama kasoma au hajasoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo tushindwe kusoma na kuwa na hizo PHDs sababu hatutakua wife materials? Aargh mkuu tuache utani tabia ya mtu hategemei sana elimu yake mtu anaweza fika chuo ila akawa mstaarabu na yule std 7 akawa na tabia mbaya ajabu. Suala la mke na mume ni kuomba tu ukutane na mtu
Good morning mama, hii comment imenibariki [emoji23][emoji23], ila hako ka laki per month sio poa [emoji4]
 
Back
Top Bottom