#COVID19 Mtazamo hasi juu ya chanjo ya Korona ni matokeo ya kivuli cha Hayati Magufuli kinachoishi

#COVID19 Mtazamo hasi juu ya chanjo ya Korona ni matokeo ya kivuli cha Hayati Magufuli kinachoishi

Wewe ndo umenena sahihi,maana watu wengi wanakzana kuwaona watanzania wabishi au akili wamekopesha kumbe shida ni serikali iliyopita,hata baadhi ya viongozi walioko sasa na wenyewe walikuwa na msimamo huo huo,leo tunalaumu watu haiwezekani
Kwahiyo wanaopinga huko Marekani na Ulaya wooote Magufuli aliwapandikiza ushawishi wake? Basi ana akili zaidi.
 
Kuficha data au laa ukiacha ushabiki wa kisiasa na chuki binafsi utaelewa ninachokielezea. Kwa msongamano wa kwenye madaladala, sokoni. Mashuleni bila kinga wala tahadhari ukilinganisha na idadi ya vifo utakuwa hujielewi kutambua kuwa herd immunity ndio iliyotuvusha

Kwahiyo ni herd immunity na sio Magufuli tena!?
 
Kumbe alie authorize heard immunity itumike nchini Vs vaccinations ni nani?

Hata dhalimu asingesema herd immunity haitokani na matamko ya viongozi madhalimu. Hayo magonjwa mengine yaliyowahi kutokea yeye ndio aliintroduce hiyo herd immunity?
 
Hakuna mtazamo hasi hata marekani watu wamekataa chanjo ndio mana ukikubali kutega bega unapewa na dola mia juu.
 
Swala la chanjo halijakaa sawa kuna maswali mengi yanayohitaji majibu,
  • Unaambiwa kuchanjwa hakukuzuii kupata Corona bado kuna uwezekano wa kupata. Sasa swali ni kwanini tuchanje?
  • Hata baada ya kuchanjwa unashauriwa kuvaa barakoa - why?
  • Chanjo uliyopewa haizuii new variants wa Corona kukudhuru. So inamaana kila strain mpya ya Korona inabidi upate chanjo yake?
Naamini Serikali ya awamu ya tano ilikuwa inatupeleka katika kujenga herd immunity na ndio iliyotuvusha awali.
Hiyo doz si kwa ajiri ya corona mkuu soon utaona majibu yake baada ya miaka kadhaa huko nikilio na kusaga meno! Chajo gani unachanja bado tu unaweza kuambukizwa sasa unachanja ili iweje! Wazungu wanainyoosha africa mmezid kuzaliana
 
Tukubali tukatae Sumu aliyoacha amepandikiza mwendazake ndiyo inayolitafuna taifa kwa Sasa kuhusiana na mtazamo hasi juu ya chanjo ya Korona.
Hapana. Approach ya Serikali ndio imeleta haya mambo.

1. Waziri wa Afya alituaminisha kwamba Chanjo haifai na akatoka na list ya dawa "approved" na Serikali yetu sikivu kwamba tutumie hizo kummaliza corona. Bahati nzuri Waziri na Naibu wake ni walewale (thanks to Samia) na tunawashangaa tu na wanavyotaka kupiga u-turn

2) Unapomwambia Mwanachi kwamba hutahusika na consequences baada ya kudungwa chanjo unampa wasiwasi mkubwa sana. Hili wala JPM (RIP) hapaswi kuhusishwa nalo

3) Hatujawahi kutakiwa kujaza "consent form" ili tuchanjwe katika chanjo zote zilizopita. Mara zote tumezoea kuona hizo form hospitalini wakati mgongjwa mahututi anapofikia hatua ya kufanyiwa operation. Consent form ile ni kukubali kwamba ndugu wa mgonjwa umekubalina na matokeo yoyote ya ile operation (kufa ama kupona). Fast forward kwenye chanjo, wananchi wanahusisha kujaza form kwanza ili uchanjwe na life & death matter. JPM anaingiaje hapa?

4) Kule zinakotoka chanjo kwa wazungu tunasikia kuna wengi tu wamegomea kuchanjwa na sasa Serikali inaplan kutoa bakshishi ya $100 ili kuhamasisha watu. Kulikoni?

5) Hakuna mwenye uhakika kama chanjo ya sasa ilikuwa kwa ajili ya ile wave ya kwanza au huyu Delta variant wa sasa. Infact cases zimeanza kuibuka upya, zikiwatandika hata wale waliokwisha chanja. Mwanchi wa kawaida anapoona haya mambo na kuamua kutochanjwa, huwezi kumlaumu third party
Dawa.jpg
 
  • Unaambiwa kuchanjwa hakukuzuii kupata Corona bado kuna uwezekano wa kupata. Sasa swali ni kwanini tuchanje?
  • Hata baada ya kuchanjwa unashauriwa kuvaa barakoa - why?
  • Chanjo uliyopewa haizuii new variants wa Corona kukudhuru. So inamaana kila strain mpya ya Korona inabidi upate chanjo yake?
awamu ya tano ilikuwa inatupeleka katika kujenga herd immunity na ndio iliyotuvusha awali.
Asante kwa kuuliza maswali ya maana, isipokuwa majibu yapo tena yanafahamika tangu muda mrefu.

"kuchanjwa hakukuzuii kupata Corona bado kuna uwezekano wa kupata. Sasa swali ni kwanini tuchanje?"
Kwa sababu chanjo inapunguza sana hatari ya kuwa mgonjwa na hali mbaya ya ugonjwa. "Kupata COVID" - maana yake virusi vinaingia mwilini vinaweza kupimwa. Hapa unahesabiwa umeambukizwa. Ila ambukizo hili halina madhara makubwa kwa wengi sana waliopata chanjo (bila shaka umeshasikia hakuna tiba ya 100%, na usio na hatari fulani kwa wachache - sawa kabisa na chanjo nyingine ulizopata tayari ulipokuwa mtoto) . Vipimo vyake vinapatikana: katika nchi ambako wazee wameshachanjwa vifo vya COVID kati ya wazee vimpungua sana.

"baada ya kuchanjwa unashauriwa kuvaa barakoa - why?"
Kukinga wengine! Na kupunguza idadi ya virusi utakavyopokea maana hata baada ya kupokea chanjo unaweza kubeba virusi na kuwa hatari kwa wengine wasiochanjwa. Kwa hiyo kama idadi ya maambukizo katika jamii inapanda juu, ushauri ni kuvaa tena barakoa. Pia asilimia ndogo ya waliochanjwa wanaweza kupata hali kali ya COVID - ni tahadhari kuvaa barakoa.

"Chanjo uliyopewa haizuii new variants wa Corona kukudhuru. So inamaana kila strain mpya ya Korona inabidi upate chanjo yake?"
Hapana, maana hadi sasa inaonekana kwamba Astra na chanjo nyingine zinasaidia pia dhidi ya COVID-Delta, ingawa si kwa kiwango sawa kama dhidi ya ina za mapema.
Lakini wakati virusi vya COVID vinabadilika sana, tutapata chanjo mpya.

Hii ni kawaida. Maana virusi vya influenza (ambavyo ni pia aina ya Koronavirus, ingawa si hatari vile kama Korona-Covid) hubadilika haraka. Hivyo katika nchi ambako wanatoa chanjo yake, chanjo hizi kutolewa upya kila baada ya miaka michache.
 
Back
Top Bottom