Mtazamo kuhusu Hotuba ya JK kuzindua Bunge Maalum la Katiba

Mtazamo kuhusu Hotuba ya JK kuzindua Bunge Maalum la Katiba

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
YATAKAYOJIRI HOTUBA YA JK KESHO

Sehemu ya I

Hali ya taharauki imetanda Dodoma. Wabunge wakitishiwa kwa kamera 13 ndani ya ukumbi na viongozi 4 wa kundi linalompinga Sitta kukiuka taratibu wamehojiwa na vyombo vya usalma.

Tishia ya kamera imewalenga wana CCM ili kupunguza nguvu ya wapinzani.
Usalama wa taifa ni kutishia wabunge.
Hakuna sheria inayoweza kumtia hatiani yoyote atakayezomea au kupiga kelele

Mkakati uliotumika ni mbovu sana. Badala ya kulifanya Jambo liwe dogo akina Sitta na Usalama wa taifa wameliwekea hamira . Wananchi wa kawaida watachunguza kila kitu na hapo wanazidi kumu expose Rais .

TARATIBU KUKIUKWA
Kukiukwa ka taratibu kulilenga kutoa nafasi kwa Rais kupitia hoja za Warioba na kuja na counter attack. Ni mkakati mbaya unaomweka Rais katika wakati mgumu kuliko ilivyotarajiwa. Kikwete anakwenda Dodoma kama Rais wan chi, siyo mwenyekiti wa chama.

Kazi yake ni kuzindua bunge si kujadili agenda za bunge.
Alichopaswa kufanya ni kuzindua bunge ambapo nafasi yake ingekuwa kubwa sana kusikilizwa kama Rais tofauti na ilivyo sasa anapoonekana kama mpizani wa Warioba

Kwasasa nafasi yake ni kumjibu Warioba ili kukidhi mkakati aliopangiwa na wasaidizi na wale wa bunge (anakuwa mpinzani), huku akitakiwa kuchukua nafasi ya Urais kwa To strike the balance ni kitu kigumu na siyo sifa ya uongozi au kiongozi.

CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI KIKWETE
Kikwete anakwenda Dodoma akikabiliwa na changamoto nyingi.

  1. Kwenda kuthibitishia umma kuwa alikuwa na nia njema na mchakato(Rais)
  2. Kwenda akitakiwa kuwaridhisha wahafidhina wa CCM wasiotaka mabadiliko
  3. Kwenda akitakiwa kukabiliana na CCM wanaotaka mweleko mpya wa nchi
  4. Kuzuia kuparaganyika kwa CCM ya mivutano ya Warioba Vs wahafidhina
  5. Kukabaliana na wazanzibar waliogawanyika kwa siri na kwa wazi
  6. Kuwashawishi wazanzbar kuhusu chanzo cha matatizo waliyosababisha
  7. Kukabiliana na wabunge huru wanaoitakia mema nchi hii
  8. Kukabiliana na hoja za tume ya Warioba ili kuzuia mabadiliko
  9. Kuepusha kuvunjika kwa muungano nusu uliobaki mikononi mwake
  10. Kuwaleta wabunge wote kwa ajili ya muafaka wa kitaifa.
 
Sehemu ya II

UMUHUMI WA HOTUBA YAKE

Kama ingekuwa ni Marekani ingaitwa ‘state of union', na Uingereza ‘Throne speech.

Kwamba anahutubia chombo cha uwakilishi wa wananchi kwa pamoja.

Ndivyo ilivyo katika BMLK(Bunge maalumu la katiba)


Matarajio ya wananchi ni Rais kutoa mweleko na dira ya nchi katika kuandika nyaraka muhimu ya taifa kwa miongo kama si karne zijazo.

Kuzuia kuvunjika kwa muungano ambalo ndilo tishio kubwa lililopo

Lakini pia ni kulileta taifa linaloonekana kugawanyika kwa pamoja.


HOTUBA YA RAIS

Itakuwa katika muundo wa mambo mawili makubwa

1: Kuzungumzia utaifa , kuwaunganisha wananchi na kuondoa tension iliyopo


Hotuba itaeleza kuhusu


  1. Umuhimu wa kuandika katiba ukilifanya suala la muungano dogo sana
(Rejea changamoto 10, 9, 1 bandiko I)

  1. Kumsifia Warioba kwa kazi nzuri na ngumu (Rejea 4,1 bandiko I)
  2. Kuwahakikishia wananchi maoni yao yatazingatiwa bila kuingiliwa
  3. Kutumia muungano kama nembo ya umoja wa kitaifa na historia ya Afrika
  4. Kuelezea faida za muungano kwa pande zote kwa kutumia mifano rahisi ya kuoelana, ajira na biashara (Rejea changamoto 3, 6, 9 bandiko I)
  5. Kuepuka kutumia takwimu za uchumi kama alivyotumia Warioba kwasababu hazitajibu hoja za Warioba (Rejea 2 na 9 changamoto bandiko I)
  6. Kuwatumia Nyerere na Karume kuonyesha jinsi muungano ulivyoasisiwa bila kuingia katika undani wake ili kuepuka maudhi (Rejea 2, 5, 6 Bandiko I)
  7. Kuelezea changamoto za muungano kama ilivyo kwingine duniani(Rejea 2,4,5,7)
  8. Kueleza mchakato uachwe kwa maamuzi ya wananchi ili kuepuka kuuudhi makundi ( Rejea 2,3,6,7 bandiko I)

AU


2: Hotuba inaweza kuwa na muundo wa pili kama ifuatavyo


  1. Kukabiliana na hoja za Warioba bila kumtaja kwa kuanza kumsifia(1(b) hapo juu)
  2. Kutoa picha kuwa wapinzani ndio chanzo cha vurugu bila kuwataja direct
  3. Kutumia gharama kama kigezo muhimu cha kuamua muundo wa muungano
  4. Kumtumia Nyerere na Karume kupangua hoja za Warioba (1(g)
  5. Kuelezea faida za muungano zaidi kuliko matatizo hata kama matatizo ni makubwa kuliko faida ili kuwapumbaza wananchi
  6. Kueleza hatua zilizofikiwa katika kukabliana na kero za muungano
  7. Kuwaridhisha Wazanzibar kwa mwelekeo wa ahadi zaidi
  8. Kuwatisha wazanzibar endapo wataamua vinginevyo

 
Sehemu ya III

MATATIZO YATAKAYOTOKANA NA HOTUBA YAKE


1. JK akiongea kama Rais na mwenye nia ya dhati atahitaji kusimama katika ukweli.

Kwa haulka ya JK ya kutaka kupendeza kila upande na kutotaka kuudhi upande wowote hatafanikiwa.


Atatengeneza mgogoro mkubwa kuleta sintofahamu kuliko ilivyo.

Ndivyo takavyofanya kesho.Tatizo kubwa litakuwa ni kuthibitisha kile kinachosemwa udhaifu wake.


2. JK akiamua kuongea kwa dhati na ukweli atajikuta katika mgogoro na makundi.

a) Wazanzibar hawatakubali matatizo yaliyozua mgogoro, kauli za JK zitakuwa kutia mafuta katika kuni zinazowaka.

b)Wahafidhaina wa CCM hawatakubali kusikia ukweli kuhusu muundo mpya.

JK ni dhaifu mbele yao na hilo litamlazamisha aegemee upande wa wahafidhina

c) Kuegemea huko kutaudhi CCM progressive, wapinzani, wazanzibar na wale wa makundi. Nguvu ya wahafidhina itategemea mbinu na ulaghai.


Mbele ya safari wahafidhina hawatkuwa na nguvu ya kukabiliana na wananchi.

Muungano utahitimishwa bila ridhaa ya JK au wahafidhina


3. JK akiamua kumshambulia Warioba au kumjibu kwa namna yoyote ile iwe ya upole au ukali bado atatakiwa ajibu hoja za Warioba kwa mantiki.


Kwa hali ilivyo, kama ukweli wa kuvunjwa katiba, takwimu za uchumi, na historia ya muungano pamoja na muda wa matatizo yaliyopo( miaka 50) JK ana nafasi ndogo ya kumjibu Warioba napengine ni salama akiepuka hilo


Endapo atajibu basi ni lazima awe katika kiwango cha juu sana, kinyume chake atadhalilika sana.


4.JK ataongea kuhusu makundi na interest zao.

Jitihada zake zitakuwa kuepuka kutaja vyama vya siasa na misimamo yao.


Katika kutaja makundi atayapa nafasi yasikilizwe .

Hapo atakuwa ametupa mpira kwa CCM kutumia bunge na wingi kukamilisha azma yao.


5. JK atawahakikishia wananchi umadhubuti wa vyombo vya dola ili kuwatisha wabunge na wananchi kwa ujumla



Matatizo atakayokumbana na yao kwa kufanya hivyo

i) Mpasuko wa wazi kabisa ndani ya BMLK ambao utavunja bunge kabla ya wakati

ii) Kupalilia mgogoro hasa katika CCM Zanzibar ambao hadi sasa upo unafukuta

iii) Kuchonganisha wazee, wahafidhina na CCM mabadiliko, mpasuko utakaoendelea hadi chaguzi zijazo.

vi)Kuwagawa wananchi kwa makundi ya vyama, Utanganyika na Uzanzibar.

Muungano utakuwa unahitimisha safari yake.



 
Sehemu ya Mwisho

Hotuba ya JK kesho itamwelezea maisha yake ya uongozi na mchango wake katika taifa hili. Ni hotuba itakayo m-define akiwa madarakani na siku za kustaafu.


Itamwacha katika wakati ambao hawezi kuusahau kwa taifa kuparaganyika mikoni mwake,. Itakuwa ndio kithibitisho cha udhaifu wa uongozi wake ambao hadi sasa ni dhaifu


Ni hotuba inayotakiwa ililete taifa pamoja. Kuleta taifa pamoja si kucheka au kupendeza makundi na wala si kutaka kumfurahisha kila mtu kama atakavyofanya.


Ni muda wa kuzungumza ukweli hata kama ni mchungu.

Ni wakati wa kuonyesha dira hata kama haikubaliki na kundi fulani


Ni muda JK anatakiwa akubaliane na wananchi kwa kile wanachokisema na kukipendekeza. Hatakiwi awe kiongozi anayejenga mpasuko zaidi.


JK atafanikiwa akiwa mkweli, kutoona haya wala kutaka kusifiwa au kumpendeza mtu. Hatakiwi kuendeleza malumbano ya vyama bali kuleta muafaka wa kudumu wa taifa hili.


Hotuba yake inaweza kuchochea hali tusiyoizoe nchini. Na hilo likitokea basi ndio mwisho wa muungano. Hata kama ikibidi muungano ufe, bado anajukumu la kuhakikisha kuwa kifo hicho hakiachi taifa lenye vurugu au kuhasimiana.


MATARAJIO YA WANANCHI


Wananchi wanatarajia mengi kutoka kwa Rais.

Kwa hali ilivyo na msimamo wa JK hakuna lolote jipya tunaloweza kusema litatokea.


  1. Itakuwa hotuba ya kupendeza watu na kufurahisha kila kundi
  2. Itakwepa ukweli wa historia
  3. Itakwepa kiini cha matatizo kama uchumi na mabadiliko ya kijamii/kizazi
  4. Itakuwa na lengo la kuwasuta wasiokubaliana na serikali
  5. Itajenga hofu kwa washiriki kwa kutumia rungu la dola na chama
  6. Haitakuwa na ufumbuzi wa mtatizo yaliyopo na yajayo.
  7. Itafungua ‘pandora box' kwa pande zote
  8. Na inaweza kuwa hotuba itakayoleta sintofahamu na kuparaganyika kwa taifa.


Tusemezane.

 
Asante sana mkuu Nguruvi3 na nina uhakika kesho JK kwa namna yeyote ile lazima atapita miongoni mwa hoja ulizozitoa.

Kwa kuongezea tu ni kwamba endapo ataamua kutoa vitisho kwa wabunge na wananchi nina uhakika kesho ndio utakua mwisho wa bunge la katiba endapo tu wabunge watakua imara na kama wataamua kusimama upande wa wananchi.

Pia kuna tetesi zimeenea leo kuhusu uwezekano wa jk kukumbana na zomeazomea, vipi mkuu Nguruvi3 unazo taarifa zozote kuhusu hili? Kama ndivyo hebu tuwekee ufafanuzi japo kwa kifupi.
 
Last edited by a moderator:
Kama alivyojadili Nguruvi3, Rais Kikwete hana uwezo tena wa kuvunja nguvu ya hoja iliyowasilishwa na jaji warioba kuhusu muundo wa muungano. Uwezo wa Kikwete utategemea mabavu peke yake na sidhani kama atashauriwa kufanya hivyo kwani hatua hiyo inaweza kupelekea sio tu bunge la katiba kuvunjika bali pia itatengeneza njia nyeupe kwa muungano kuvunjika huku CCM ikibeba lawama juu ya hilo.
Kufuatia umakini wa hoja za jaji warioba ambazo zimewafungua wananchi wengi kuelewa kwamba kumbe tatizo sio warioba bali CCM yenyewe katika kulea migogoro ya muungano ambayo leo imeibatiza jina la "changamoto" kama vile ni inherent kwa muungano wowote, Kikwete hataweza tena kuushawishi umma kwamba mfumo uliopo ndio bora kwao, kwa nchi shiriki, muungano na taifa kwa ujumla. Kama alivyojadili nguruvi3, kufanikisha hilo, itabidi Kikwete aje ne presentation ya hali ya juu hasa ambayo haitakuwa na chembe yoyote ya partisan politics. Hata hivyo, haina maana kwamba hilo litafanya hoja za warioba irrelevant, sana sana zitamfanya tu Kikwete avuke event ya kesho salama japo kwa muda. Vinginevyo suala la serikali tatu haliepukiki tena, na kikwete atajikuta kwamba alichagua the wrong side of history katika maisha yake ya ustaafu kwa ajili ya kulinda maslahi ya chama chake cha CCM.

Ni vigumu kubaini Kikwete atapangua vipi hoja zifuatazo za warioba ambazo zilizaa vigelegele bungeni majuzi:

Tume imependekeza kuwapo na mamlaka huru ya zanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka huru ya muungano ili kuwepo muungao imara na usio na visingizio vya kero
Nape Nnauye ameendelea kusikika akijenga hoja kwamba msimamo wa serikali mbili utapiganiwa na ccm ndani ya bunge la katiba na kwamba serikali itafanyia kazi "changamoto" zilizopo kwa kuboresha maeneo yenye mapungufu. Umma wa watanzania utakuwa makini kusikia Kikwete atafafanua vipi hili, hasa ikizingatiwa kwa ccm kupitia nape hadi leo haijaja na majibu kwa wananchi juu ya kipi kipya itakifanya hasa katika mazingira ya mgogoro baina ya katiba ya znz na ile ya muungano. Bila ya kujalisha Kikwete atajadili vipi suala hili ambalo umma una shauku kubwa ya kumsikia, hapo papo watazamaji wengi wata recall hoja nyingine ya warioba juzi bungeni kwamba:

Muungano ule ulikuwa wa nchi moja yenye serikali mbili. Hivi sasa kuna muungano (kama utaitwa muungano) wa nchi mbili, serikali mbili.

Hoja hii haitapatiwa majibu na kikwete, na iwapo atajaribu kuipangua kwa kuelezea jinsi gani ccm ina mkakati endelevu wa kufanyia kazi changamoto za muungano, wananchi watakumbuka maneno ya warioba juzi kwamba:

Kila kukicha kila hatua inayochukuliwa na watawala inakuwa ya kuondoka kwenye muungano wa nchi moja na kwenda kwenye nchi mbili ambako kunahitaji serikali tatu ili kuhudumia muungano wa nchi hizo mbilii

Ikumbukwe kwamba rais kikwete anaenda bungeni huku yafuatayo yakiwa yamemtangulia:

1. Vurugu bungeni kutokana na sitta kuvunja kanuni, kanuni ambayo ililenga kumsaidia kikwete.
2. Kikwete akiwa tayari amekiasa ccm kujiandaa kisaikolojia kukubali maoi ya wananchi juu ya mfumo wa muungano wanaoutaka hata ule wa serikali tatu.
3. Warioba kutoa siri kwamba maoni ya BLW, Bunge la JMT, Ofisi ya waziri mkuu, ofisi ya makamu wa rais, wataalamu mbalimbali, kote huku mapendekezo ni serikali tatu.
4. Zanzibar imejiandikia katiba 2010, katiba ambayo kwa sasa ni superior kwa katiba ya JMT inayompa kikwete madaraka ya kuendesha shughuli zote za serikali ndani ya JMT. Hadi leo, hakuna kiongozi wa juu wa chama ambae amelijadili hilo zaidi ya umma kusikia tishia tishia ya Ccm kwa wajumbe wa BLW kwamba wabadilishe vipengele vitakavyoangusha hoja ya ccm ju ya serikali mbili.

Masuala haya manne yatakuwa yanagonga kama kengele vichwani mwa wananchi wengi ambao watakuwa wanamsikiliza Kikwete. Suala muhimu kuliko yote kati ya haya pengine ni lile la katiba ya znz. Unless kikwete aje na news kwamba muafaka umepatikana na kwamba znz watafanya marekebisho husika.

That said and done, kikwete kutumia muda mwingi kujibu hoja za warioba pia itakuwa ni tatizo na liinaweza mgharimu sana iwapo focus yake kubwa itakuwa hapo kwani kama alivyojadili nguruvi3, role ya rais katika hatua hii sio kwenda kushiriki na kuchangia hoja za rasimu kwani pale sio mahala pake, kazi yake ni kwenda tu kufungua bunge na kulipa baraka zake kama kiongozi wa nchi. Ndio maana kikanuni, ilitakiwa warioba aende kuwasilisha rasimu baada ya Kikwete, sio kabla.



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Namtahadharisha Kikwete awe muangalifu sana na maneno atakayoyatamka kesho bungeni...sababu ya kumpa hiyo tahadhari ni vifungu hivi viwili katika Katiba ya nchi jirani ya Zanzibar;

  1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
  2. Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yoyote inatofautiana na Katiba hii, basi Katiba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.
Je hicho kifungu 80 kinasemaje?

80. (1) Kwa masharti ya kifungu hiki Baraza la Wawakilishi linaweza kubadilisha kifungu chochote katika Katiba hii.

Katiba ya Zanzibar haitambui mamlaka ya Raisi wa Jamhuri. Yawezekana hii ndiyo sababu Raisi hakuthubutu kuikemea Zanzibar ilipovunja Katiba ya Jamhuri! Kwa mbali nakumbuka yalomkuta Mizengo Pinda alipojaribu kuhoji Zanzibar kujiita nchi.
 
Namtahadharisha Kikwete awe muangalifu sana na maneno atakayoyatamka kesho bungeni...sababu ya kumpa hiyo tahadhari ni vifungu hivi viwili katika Katiba ya nchi jirani ya Zanzibar;

Je hicho kifungu 80 kinasemaje?



Katiba ya Zanzibar haitambui mamlaka ya Raisi wa Jamhuri. Yawezekana hii ndiyo sababu Raisi hakuthubutu kuikemea Zanzibar ilipovunja Katiba ya Jamhuri! Kwa mbali nakumbuka yalomkuta Mizengo Pinda alipojaribu kuhoji Zanzibar kujiita nchi.

Katika hili, Kikwete ataweza kuchomoka iwapo atakuja na taarifa kwamba makubaliano yameshafikiwa kwamba vifungu husika vya katiba ya zanzibar vitabadilishwa. Nje ya hapo, sasa ni zamu ya President of the United republic of Tanzania to be a stranger on zanzibar's soil baada ya miaka mingi ya president of zanzibar kuwa a stranger in the union cabinet;

Ama kweli CCM's politicians are short on "memory" and long on "power";


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Katika hili, Kikwete ataweza kuchomoka iwapo atakuja na taarifa kwamba makubaliano yameshafikiwa kwamba vifungu husika vya katiba ya zanzibar vitabadilishwa. Nje ya hapo, sasa ni zamu ya President of the United republic of Tanzania to be a stranger on zanzibar's soil baada ya miaka mingi ya president of zanzibar kuwa a stranger in the union cabinet;

Ama kweli CCM's politicians are short on "memory" and long on "power";



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Zanzibar ni kiboko. Ni Mwalimu tu aliweza kuwa contain kwa silaha mbili;

1. Nguvu ya hoja, one on one and without mincing words.
2. Utawala wa sheria, no one is above the Law.

Bahati mbaya kwa Kikwete, ni dhaifu hana ujasiri. Wazanzibari si watu watu wa kuwachekea. Huko Dodoma watakubaliana nawe lakini wakipanda boti tu kurudi Unguja washakugeuka.
 
KUVUNJWA KWA KATIBA

Katika mambo yanayosumbua ni lile la Zanzibar kuvunja katiba ya muungano kama alivyoonyesha Mag3 #8 hapo juu.

Kikwete akiingia ofisini aliapa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT.
Kiapo hicho alikula Nyerere ambaye aliyesimama kwa vitendo kukataa kuvunjwa kwa katiba.
Marais waliofuata walijitahidi hata kama si kwa kiwango chote.

Kikwete ameshuhudia katiba ikivunjwa 2010 akiwa mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya muungano.
Wananchi watahitaji kusikia JK amelinda na kuitetea vipi katiba iliyopo ambayo aliapa kuilinda.

Wananchi watahitaji kusikia kauli ya kukemea uvunjwaji au baraka alizotoa katika jambo hilo.
Kinyume na hapo JK umma utamhoji uwezo wake wa kuitetea katiba iliyopo na kama yupotayari kushuhudia uandikwaji wa nyingine katika mazingira aliyoshindwa kuyazuia.

JK akishindwa kukemea uvunjaji wa katiba basi atakuwa anajenga mazingira mazuri sana ya kuvunja katiba na hilo litaanza na muungano. Ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa muungano

KUKWEPA WAJIBU
JK atatumia muda kueleza matatizo yaliyopo ni ya kurithi.
Hilo litakuwa ni kosa kwasababu matatizo hayo yakitokea alikuwa katika system akitumikia chama kama katibu wake, mbunge, naibu waziri na waziri kamili.
JK alikuwepo wakati wa sakata la G55 na mengine yaliyofuata. Kaishi kote bara na visiwani.

Litakuwa jambo la kushangaza kama atautupa mzigo wa muungano katika historia.
Historia itamhukumu kwani alipoingia madarakani 2005 aliahidi kutatua migogoro.

Miaka 8 baada ya kusema bungeni matatizo yamekuwa makubwa zaidi kuliko aliyoyakuta.
Katiba imevunjwa akiona kwa macho yake tena baada ya kipindi kimoja.
Kwa hili hana nafasi ya kuisngizia historia na kama atatamka hilo hataeleweka.

UCHAMBUZI Vs UKWELI
Tume ya Warioba imekuja na uchambuzi wa matatizo kwa analysis, data and facts.
Ukisoma taarifa nzima ya Warioba hakuna sehemu iliyozungumziwa kisiasa.
Na kila tatizo lililoainishwa limewekewa ufumbuzi kwa maana ya suggestions.

Rais Kikwete anatakiwa aeleze ukweli wa matatizo siyo uchambuzi.
Ukweli ni jinsi tatizo lililpoanzia lilivyopanuka hadi kufika hapa.
Nini chanzo chake, suluhu gani zimefanywa,mafanikio yapi yamepatikana na changamoto zipi zilizopo na kwanini hazina ufumbuzi.

Atakapokuja na hoja za 'yanazungumzika' itabidi aende mbali na kuwaeleza wananchi ni kwanini katika kipindi chake ufumbuzi haukuwepo na tatizo limezidi hadi kutishia taifa kusambaratika.
Hapa hakuna siasa bali kueleza ufumbuzi kwa neno moja hadi jingine na si kama @Nape

Endapo atachagua kumjibu Warioba, itabidi apitie hoja moja baada ya nyingine.
Kwa kiwango cha hotuba ya Warioba uwezekano wa kukanyaga miba ni mkubwa sana.
Hata kama atafikia kiwango (jambo gumu sana) bado atakuwa chini ya maoni ya akina Warioba. Hiyo ni dhalili kwakwe.

Na katika kueleza ukweli, Rais hapaswi kukwepa hoja za msingi. Ni lazima akabiliane nazo. Atakapochagua hoja atakuwa analea donda, litakapofumuka hatakuwa na mahali pa kushika.
 
Skype;9012268]Pia kuna tetesi zimeenea leo kuhusu uwezekano wa jk kukumbana na zomeazomea, vipi mkuu Nguruvi3 unazo taarifa zozote kuhusu hili? Kama ndivyo hebu tuwekee ufafanuzi japo kwa kifupi.
Kuna mambo yamefanyika baada ya tetesi za kuzomewa kuzagaa.

1. Spika amesema kuna kamera 13 kubaini watakaozomea.
Hakukuwa na sababu za Sitta kutaja uwepo wa kamera au idadi,tunajua zipo kwa usalama.
Kitendo cha kutamka kimelenga kuwatisha wabunge wachache huru na kundi kubwa la CCM lislokubaliana na mambo yalivyo

2. Kuna idadi kubwa ya usalama wa taifa ambao nao kama Sitta wameingia katika kutangaza marufuku ya kuzomea ikiwa ni pamoja na kunukuliwa jana wakisema wanawahoji viongozi wanaoongoza harakati za kuzomea

3. CCM na uongozi wa bunge umeaalika marais wote wastaafu kutoka zanzibar na JMT.
Hili ni katika jitihada za kujenga mazingira ya kuzuia uzomeaji kwani viongozi wengine wanaheshimika

4. Zipo taarifa za uhakika za kuhamasishana kwa baadhi ya wabunge wa CCM wasiotaka mabadiliko, kushangilia kwa nguvu hata kwa hoja dhaifu. Lengo ni kutaka kuonyeshawabunge wengi wanakubaliana na JK.
Mpango huo wa kushangilia unaweza kuwa chanzo kingine cha kuzomea.

Jambo moja la kujiuliza, kama tumefika mahali vitisho vinatolewa ili rais ahutubie basi lipo tatizo.
1. Kwamba Rais haaminiki na wala haheshimiki. Kwanini inakuwa hivyo, jibu lake ni gumu
2. Watu hawana imani na uongozi wa bunge kwa njia za kihuni inazotelekeza.
Nini kitatokea mbele ya safari, jibu ni gumu

Kwa upande wa Rais, wapinzani na watu wa makundi mengine wajejaribu sana kumuheshimu kila alipotaka wamsikilize.

Kitu kilichoondoa imani ni undumila kuwili. Akiwa na wapinzani JK anazungumzia utaifa. Akiwa na CCM JK anazungumzia UCCM. Ni mgumu kueleweka anasimamia wapi na kwanini kwasababu tu ya ujanja ujanja ambao kimsingi si jambo zuri kwa kiongozi. Undumila kuwili unamuondolea kiongozi ile trust aliyopewa na wananchi.

Mfano, kesho JK hawezi kuzungumzia upande mmoja wa muungano ni lazima atatafuta hoja mbadala ya upande wa pili ili kutoonekana ni mbaya au kupendeza sehemu zote.
Hilo tutalijadili kwa kuonyesha tunayoyasema baada ya hotuba yake.
 
Hii kitu ni msiba wa Muungano leo, tujiandae tuu kuvunja Muungano kwa amani.
Salute mkuu Nguruvi3 kwa hizo predictions na ninahisi mkulu atacheza humohumo. Bahati nzuri kila part umeweka negative and positive effects zake. Leo ni leo
 
Last edited by a moderator:
Katika hili, Kikwete ataweza kuchomoka iwapo atakuja na taarifa kwamba makubaliano yameshafikiwa kwamba vifungu husika vya katiba ya zanzibar vitabadilishwa. Nje ya hapo, sasa ni zamu ya President of the United republic of Tanzania to be a stranger on zanzibar's soil baada ya miaka mingi ya president of zanzibar kuwa a stranger in the union cabinet;
Ama kweli CCM's politicians are short on "memory" and long on "power";
Katika hoja ya kuondoa vipengele, Rais ana njia mbili za kuyeyusha hilo kwa kurudia kauli ya Zanzibar ni nchi ndani na si nchi nje.

Hatari zinazomkabili katika hoja ya znz ni nchi au si nchi ni pamoja na
1. Akigusia znz kuwa nchi lazima agusie mabadiliko ya katiba ya znz ya 2010 ambayo imevunja katiba ya JMT.
Hili si eneo zuri kugusa ingawa anapaswa kulizungumzia kama mlinzi wa katiba ya nchi.
Kama atalizungumzia itakuwa kijuu juu tu na wala hatagusa katiba. Maelezo ya kina yatabaki kwa hoja za Warioba.

2. Kutamka kubadili vipengele kutaleta mtafaruku mkubwa miongoni mwa wazanzibar. Tunafahamu Pandu Kificho aliandika waraka wa serikali 3, baada ya kutishwa kabadili na sasa ni serikali 2. Kundi analoongoza bado lina masimamo huo.

Tunafahamu Vua na Seif Idd wao n serikali 2. Makundi haya ni ya CCM ambayo kauli ya znz ni nchi au si nchi itayaunganisha kwa wakati mmoja, lakini itayagawa kuhusu muundo wa muungano.

Kugawanyika kutaongeza nguvu kwa kundi la akina Seif Hamada na Jusa ambao katika baraza la wawakilishi CUF ni nusu ya CCM. Inahitaji wajumbe wachache tu kupata majority.

Hivyo kauli ya znz ni nchi au si nchi itazua mambo. Ajira ya Pandu kificho BLW itakwa mashakani sana kwasababu nilizozieleza. Kuna uwezekano kura ya maoni ikapinga rasimu kwa upande wa znz.

Lakini pia msimamo wa nchi utaibua jingine, utawaunganisha Wabunge waliobaki dhidi ya znz.
Hapa ndipo uhai wa bunge la katiba unapoweza kufikia tamati.
 
VIPENGELE TATA

Bado kuna vipengele byenye utata katika kanuni. Haitawezekana hata kidogo Rais kuviongelea hata kwa bahati mbaya kwanini kufanya hivyo ni kuingilia mamlaka ya BMLK. Hilo halitatokea.

Kitakachotokea ni kuongea kwa njia ya mzunguko akitaka watu wajadiliane na kupata muafaka zaidi.
Hapa anaweza kuwatumia wananchi kuwa wanafutailia na kuhuzunishwa na yanayotokea hasa vurugu.

Atakapokuwa naongelea vurugu atakuwa anawasukumia wananchi hoja ya wapinzani kususia baadhi ya mambo akimaanisha ni sehemu ya vurugu.
Itakuwa ni njia ya kufagilia kura ya wazi bila kutaja au kutamka ila kwa kupitia hoja za vurugu.
 
Inaonekana mpango uliopo ni rais kuijibu hotuba ya Warioba ndio maana wana hofu ya zomeazomea. Tusubiri huo muda wa hotuba tuone ataongelea nini.
 
Inaonekana mpango uliopo ni rais kuijibu hotuba ya Warioba ndio maana wana hofu ya zomeazomea. Tusubiri huo muda wa hotuba tuone ataongelea nini.

Na kwa uthibitisho zaidi imeripotiwa kua jk ataongozana na 'ujumbe mzito', mpaka hapo sina la kuongeza isipokua nasubiri 'purukushani' za jioni.
 
Na kwa uthibitisho zaidi imeripotiwa kua jk ataongozana na 'ujumbe mzito', mpaka hapo sina la kuongeza isipokua nasubiri 'purukushani' za jioni.

Huo ujumbe mzito nadhani azma yake ni kama alivyosema Nguruvi3 katika bandiko lake mojawapo hapo juu kuwa lengo lake ni kupunguza hiyo zomeazomea inayohofiwa kutokea hapo baadae.
 
Last edited by a moderator:
Huo ujumbe mzito nadhani azma yake ni kama alivyosema Nguruvi3 katika bandiko lake mojawapo hapo juu kuwa lengo lake ni kupunguza hiyo zomeazomea inayohofiwa kutokea hapo baadae.

Je, ujumbe huo mzito utafanikiwa kuipoza zomeazomea? Yetu macho na masikio zikiwa zimebaki dakika 154 toka sasa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom