Mtazamo kuhusu Hotuba ya JK kuzindua Bunge Maalum la Katiba

Mtazamo kuhusu Hotuba ya JK kuzindua Bunge Maalum la Katiba

Lipo suala moja muhimu ambalo halijajadiliwa hapa kuhusiana na nini JK atagusia, nalo ni juu ya kazi ya bunge la katiba.

Tangia bunge hili maalum lianze kikao, na hata kabla kidogo, kumekuwepo mjadala mkali unaohoji mamlaka ya bunge hilo juu ya rasimu ya katiba iliyowasilishwa na tume. Katika mijadala hii, wapo waliojadili kwamba bunge hili lina mamlaka ya kubadilisha na hata kuondoa chochote itakachoridhia, huku upande mwingine wa hoja ukijadili kwamba hilo haliwezekani. Makada wengi wa ccm wamekuwa kwenye upande unaojenga hoja kwamba bunge hili lina uwezo wa kubadilisha na hata kuondoa vifungu mbalimbali vitakavyo ridhiwa; nadhani Kikwete atagusia hili, huku akiegemea kwenye hoja ya makada wa ccm;

Ukweli unabakia wazi kwamba bunge la katiba halina mamlaka ya kubadili rasimu kama ilivyowasilishwa na tume ya mabadiliko ya katiba. Kuna tatizo moja kubwa:

Kifungu cha 25(2) kikisomwa kwa kiingereza kinaweka suala hili la bunge kutokuwa na mamlaka hiyo lakini tafsiri yake kwa kiswahili ndio imetoa upenyo kwa wavurugaji kuingiza siasa zao. Pamoja na haya, ujumbe wa kifungu hiki kisheria ni kwamba- rasimu hii, kama itakavyowasilishwa na tume ya mabadiliko ya katiba ndiyo itakuwa msingi wa utekelezaji wa madaraka ya bunge katika kutengeneza/kuandika katiba mpya; kwa maana hii:

Kinachoweza kufanywa na bunge la katiba ni kuboresha au kuongeza hapa na pale lakini bila ya kuathiri msingi mkuu wa rasimu hiyo. Hivyo rasimu inabakia kuwa ndiyo mhimili mkuu wa katiba mpya inayotarajiwa;

Nimejaribu verify uelewa wangu huu na wataalam wa sheria, wanasema nachojadili ni sahihi na kuongeza kwamba vinginevyo, bunge la JMT lilitunga sheria ambayo haikulipa bunge la katiba mamlaka ya kubadili vifungu vya rasimu kwa jinsi inavyofaa; na iwapo bunge la JMT lingekuwa limetunga sheria hiyo, basi ingesemwa wazi kwani sheria huwa haipindi pindi mambo bali hunyoosha mambo, hivyo sheria ingetungwa na bunge la JMT kusema kitu kama:
Bunge la katiba halitafungwa kwa namna yoyote ile na rasimu ya katiba

Au sheria ingetumia maneno yanayofanania na haya; vinginevyo kwa jinsi sheria inavyotamka hivi leo, ukweli ambao hauepukiki ni kwamba rasimu ya katiba ilikusudiwa kuwa mhimili na msingi mkuu; tatizo lililojitokeza ni kwamba tume iliamua kutojifunga na matakwa ya chama, na huu ndio msingi wa porojo za sasa za kulitafutia bunge la katiba nguvu ambazo haizistahili;

Kuna hoja pia inayojadiliwa kwamba bunge la katiba kupitia kifungu 25(1) cha sheria husika kinalipa bunge hili mamlaka yasiyo na mipaka katika kujadili na hata kubadilisha vifungu vyote vya rasimu; kifungu hiki kinasema kwamba:

"Bunge la katiba litakuwa na mamlaka ya kutengeneza katiba mpya na kutengeneza vifungu vitakavyohusiana na ufanyaji kazi wa katiba hiyo."

Katika hili, nimepata nafasi ya kumsoma wakili peterr kibatala ambae anasema:

Namna bora ya kutafsiri vifungu vya 25(1) na (2) ni kuvipa uhai vifungu vyote viwili bila ya kuathiri kimojawapo kiasi kwamba kisiwe na maana kabisa. Hii ina maana kwamba ilikuwa lazima kifungu cha 25(1) kiwepo ili kulipa bunge mamlaka kujadili rasimu na kuliongezea nyama inapobidi - kisheria tunaita enabling provision au substantive provision.

Kifungu cha 25(2) unaweza sema ni kifungu elekezi cha namna ya bunge kutekeleza mamlaka yake (procedural provision) - maelekezo yanayojumuisha mipaka ya mamlaka hiyo.

Mipaka na mamlaka ni sehemu muhimu ya mamlaka ya chombo chochote cha kisheria kwani huelezea wapi uhalali wa mamlaka husika huishia.

Kifungu hiki cha 25(2) kitashirikiana a kanuni za bunge katika kuweka misingi ya bunge kufanya kazi zake za kujadili rasimu ya katiba.

Ukiacha tafsiri ya kifungu husika ambacho kinaweza kubishaniwa, namna nyingine ya kutafsiri sheria ni kuangalia mazingira yaliyozunguka kifungu cha sheria husika.

Mchakato wa kuandaa rasimu ulianza kwa tume kukusanya maoni ya wananchi na kisha kuandaa rasimu ya kwanza. Rasimu hiyo ikafanyiwa kazi kwa njia ya kupatiwa mabaraza ya katiba na njia nyingine na kisha tume ikachukua maoni kutoka huko na kuandaa rasimu ya pili ambayo ndiyo hii iliyopelekea bunge kujumuika tayari kuijadili. Swali kuu la msingi ni:

Je, michakato yote hii ya awali iliyojumuisha wananchi moja kwa moja ilikuwa na maana gani iwapo tena kila kitu kinaweza kufumuliwa kwa kadri ya utashi wa bunge la katiba?

Hapa siyo sahihi kusema kwamba michakato yote miwili inapumuliana na kubebana (complement each other).

Na pegine ni mchakato upi unaowapa wananchi sauti ya moja kwa moja katika katiba mpya kati ya rasimu iliyosheheni maoni yao na bunge la katiba ambalo halijachaguliwa moka kwa moja na wananchi; na wala wananchi hawana namna yoyote ile ya kulidhibiti?

Mtu anaweza kuja na hoja kwamba bunge la katiba linajumuisha wabunge waliochaguliwa moja kwa moja na wananchi, na hivyo wanawakilisha maoni yao;

Hoja hii ingekuwa na nguvu iwapo maelekezo ya mchakato mzima kwa mujibu wa sheria yangekuwa kwa tume kukusanya maoni na kuandaa rasimu na kisha kuyawasilisha katika bunge la JMT na baraza la wawakilishi ili yajadiliwe na kisha kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.

Mchakato wa namna hii ambao binafsi ningeupendelea zaidi ungebakisha umiliki wa mchakato mzima na hasa rasimu yenyewe na hatimaye katiba, moja kwa moja kwa wananchi;

Huu ungefanana na njia ambayo wenzetu wa Kenya walipitia, ambapo ile rasimu maarufu kama rasimu ya Bomas (Bomas Draft) ndio ulikuwa msingi mkuu wa majadiliano bungeni (bunge la kawaida) kabla ya kufikishwa kwa wananchi kwa kura ya maoni.

Kuna suala lingine muhimu kibatala anajadili kuhusiana na sintofahamu kubwa inayoweza tokea iwapo BLK litafanya kosa linalopigiwa debe na makada wa CCM:

Tufikirie tu kwa mfano bunge la katiba linaamua kwamba linaweza kubadilisha vitu vyote vya msingi katika rasimu na katiba inapelekwa kwenye kura ya maoni na kupitishwa na baadae mahakama inasema tafsiri sahihi ya sheria ni kwamba rasimu haikutakiwa kubadilishwa na bunge la katiba.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kikwete na wana-ccm walioko Dodoma wana options 2: Kuheshimu wananchi wakiwemo wana-ccm wa ngazi chini (tukumbuke mabaraza ya katiba yalijaa wana-ccm), au kuitumbukiza Tanzania kwenye mgogoro wa kisiasa.
 
Wanaduru
Tunafuatilia kwa ukaribu sana yanayoendelea Dodoma.
Hadi sasa kitendo tulichokisema atakifanya amekifanya.

Amevuka mipaka yake na kuwa mjumbe wa BMLK.
Anaanza kuikataa tume aliyoiunda

Baada ya hapo tutajadili kwa undani hotuba yake hapa.
 
Mpaka muda huu ...Dr. Kikwete kaonyesha diplomasia katika kujadili hili swala...bila kujari wale wanaompigia makelele.

===========

....Ila kitendo cha kusema yupo 'optimistic' na serikali mbili kutatua matatizo ya muungano anapunguza nguvu ya diplomasia yake.

======
...Kusema kuwa wao katika CCM wanaamini migogoro ya sasa wanaweza kuyatatua bila kuwa na serikali ya tatu..kunamuondolea sifa muhimu ya udiplomasia katika mjadala muhimu kabisa wa kutunga Katiba mpya.

======
Kwa maelezo haya ya kutetea Zanzibar iendelee kuwepo huku Tanganyika ikizikwa ....sikubaliani naye kabisa....anachotaka kufanya Dr. Kikwete ni kuibua sintofahamu kwa watu wa Tanzania bara.
 
Leo ilikuwa ni siku ya kipekee kwa rais Kikwete kutoa hotuba ambayo ingewekwa maktaba ya nchi vizazi vijavyo visome hoja za rais katika uandikwaji wa hotuba mpya na ya kwanza kushirikisha wananchi.

Niseme hivi; Kikwete ni binadamu na kama rais ana majukumu mengi hivyo anaweza kukosa nafasi ya kuandaa hotuba yenye hoja nzito. Lakini rais ni taasis kubwa inaweza kuajiri au kuongeza nyenzo pale inapobidi.

Hadi sasa rais Kikwete anaelekea kutupilia mbali (waste) hii fursa adimu ya kutoa hotuba yenye mashiko. Sijui tatizo ni nini?
 
Wanaduru
Tunafuatilia kwa ukaribu sana yanayoendelea Dodoma.
Hadi sasa kitendo tulichokisema atakifanya amekifanya.

Amevuka mipaka yake na kuwa mjumbe wa BMLK.
Anaanza kuikataa tume aliyoiunda

Baada ya hapo tutajadili kwa undani hotuba yake hapa.

Mkuu ninamsikiliza lakini naona kama kashindwa kusimama kama rais ila kasimama kama mwanachama na mtetezi wa serikali 2 kwa nguvu zote tena kwa hisia za kichama zaidi.
 
Kikwete na wana-ccm walioko Dodoma wana options 2: Kuheshimu wananchi wakiwemo wana-ccm wa ngazi chini (tukumbuke mabaraza ya katiba yalijaa wana-ccm), au kuitumbukiza Tanzania kwenye mgogoro wa kisiasa.

Na ninavyoona huko mbele tutakua na mtafaruku mkubwa sana kisiasa hadi kiutamaduni na ndo mwanzo wa kutokea machafuko
 
Mwenyekiti Sitta ilitakiwa aseme kwamba sasa namkaribisha Mwenyekiti wa CCM kuja kujibu mapigo ya Mwenyekiti wa tume ya katiba, Jaji Warioba.

Alianza vizuri mno but he has taken a very wrong exit.

Nadhani imetosha, angeliaga bunge, kuanza mjadala wa kanuni kunaweza leta mtafaruku asipokuwa makini.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwa hali niliyoiona leo nategemea marumbano na mapigano makali bungeni aidha ya hoja au ya ngumi yatatokea wakati wa mjadala wa rasimu.
 
wakuu mwenye hotuba yake yote aitupie humu, nimeshimdwa kumsikia mambo mengi maana kulikuwa na makelele mengi ya kumshangilia, nimesikia msemo wake mmoja tu wa ''MTU KITU, ASIYE NA KITU KINYAMA MWITU'' JK 21/03/2014
 
Nitashangaa kama kuna mtu atakuwa anashangaa kwa Rais Kikwete kutoa hotuba inayojenga kutetea muhimili wa serikali anayoiongoza na kikubwa kabisa, kutetea sera kuu ya chama chake kinachoongoza taifa. Kama kuna mtu anadhani Rais Kikwete asingetetea hoja ya serikali mbili, basi huyo hayuko kwenye uharisia wa mambo ya siasa za Tanzania.

Kama Jaji Warioba alitumia kigezo cha malalamiko ya Wazanzibari kwa maana kwamba, kuondoa malalamiko ya Wazanzibari ndiyo kuondoa kero za muungano, vivyo hivyo hata Rais Kikwete ametumia dhana hiyo hiyo katika kujenga hoja kwenye hotuba yake kwa kujikita kwenye malalamiko ya Wazanzibari katika kuyatafutia dawa ya kisiasa kwa matumaini kwamba, hata magonjwa ya kisiasa yanayoibuliwa na Watanzania bara yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi.

Ninashukuru sana kwa tume ya Jaji Warioba kuja na hoja ya serikali tatu. Kama tume ya Jaji Warioba ingekuja na hoja ya serikali mbili, ninaamini tusingezisikia taasisi kuu za Tanzania na CCM zikijitahidi kutushawishi na kuelezea chanzo cha matatizo na njia zinazofanya au zinavyotaka kuzifanya katika kukabiliana na wimbi la watu wanaotaka njia nyingine mbadala za kuondoa kero za muungano.

Hoja ya kuwepo kwa serikali tatu imezitingisha taasisi kuu za Tanzania kwa maana kuwa serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano bila kusahau, CCM katika kujiangalia na kufahamu mapungufu katika muungano kutokana na msukumo kutoka kwa wananchi walioitikia na kukubaliana na hoja za serikali tatu. Muda mrefu aliotumia Rais Kikwete kuongelea swala la Muungano unadhihirisha jinsi serikali yake na CCM walivyotingishwa kuhusiana na hoja ya serikali tatu.

Ninafahamu kuwa CCM watakuja na rasimu mbadala lau majibu ya hoja ya serikali tatu akini pia kutokana na kutingishwa na hoja za serikali tatu kutoka kwenye Kamati ya Jaji Warioba, lazima hiyo mbadala iwe kweli ni mbadala kutokana na political trends zinazochipuka huku zimebeba mawazo ya kukubaliana na serikali tatu. Political actions za serikali mbili na CCM kwa sasa ndizo zitakazo determine their political fate katika uwepo wa serikali mbili.

Siyo kwamba wananchi wanaotaka serikali tatu hawataki muungano, la hasha. Matatizo ya muungano ndiyo yamepelekea watu kuja na aina nyingine ya muungano wakitegemea ndiyo utakuwa mwarobaini wa matatizo ya muungano. Hii imesababishwa na matokeo ya kushindwa au kusua sua kuziondoa kero kuu za muungano kwa zaidi ya miaka 35.

Ninafahamu wale wanaotaka serikali za mkataba wana mantiki ya kuvunja muungano hasa ukiziangalia component za serikali inayoingia kwenye mkataba katika mantiki ya serikali za Tanganyika na Zanzibar.

Ngoma ya muungano iko kwa serikali za Muungano kwa sasa ambazo zinaongozwa na CCM.
 
Ili hoja ya serikali 3 ijadilike sharti katiba ya Zanzibar irekebishwe kwa kuondoa vifungu vinavyoifanya Zanzibar nchi na kubagua raia wa Tanzania wenye asili ya Tanganyika. Bila kufanya hivyo hatuna katiba mpya. Je, Zanzibar watakubali kubadilisha?
 
Kwanza niseme swala la wengi kulaumu kwamba JK amechukua picha ya kichama zaidi ya uraisi kwenye speech yake ya leo, lina sehemu mbili za shilingi.

Sehemu moja ilikuwa ni lazima JK kuchukua vazi hilo sababu Jaji Warioba alipokuja siku moja iliyopita alitumia muda mwingi kushawishi umuhumi wa serikali tatu kwa kutumia maono mengi (opinions) na uhalisia (facts) mchache, hivyo ilikuwa ni lazima JK aweke level sawa (Balance the cards). Nadhani kwa hili Mh. Raisi amefanya vizuri kwani sasa wanaotaka kusikia pande zote za arguments wameweza kuzikia. Lakini sehemu ya pili ni kwamba Mh. Raisi ni sehemu ya Watanzania, na hawezi kusema kwamba yupo katikati (neutral) hili haliwezekani, hivyo nadhani ametumia utashi mkubwa kuleta argument anayo iyona yeye ni valid.

Nadhani kuna sehemu kubwa sana ya katiba hii ambayo wote tunafunga macho kuitazama, na tunaweka mawiwo na machewo kwenye sehemu moja tuu ya katiba nayo ni muungano. Hii inaweza kuleta madhara makubwa sana.
 
Nitashangaa kama kuna mtu atakuwa anashangaa kwa Rais Kikwete kutoa hotuba inayojenga kutetea muhimili wa serikali anayoiongoza na kikubwa kabisa, kutetea sera kuu ya chama chake kinachoongoza taifa. Kama kuna mtu anadhani Rais Kikwete asingetetea hoja ya serikali mbili, basi huyo hayuko kwenye uharisia wa mambo ya siasa za Tanzania.

Kama Jaji Warioba alitumia kigezo cha malalamiko ya Wazanzibari kwa maana kwamba, kuondoa malalamiko ya Wazanzibari ndiyo kuondoa kero za muungano, vivyo hivyo hata Rais Kikwete ametumia dhana hiyo hiyo katika kujenga hoja kwenye hotuba yake kwa kujikita kwenye malalamiko ya Wazanzibari katika kuyatafutia dawa ya kisiasa kwa matumaini kwamba, hata magonjwa ya kisiasa yanayoibuliwa na Watanzania bara yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi.

Ninashukuru sana kwa tume ya Jaji Warioba kuja na hoja ya serikali tatu. Kama tume ya Jaji Warioba ingekuja na hoja ya serikali mbili, ninaamini tusingezisikia taasisi kuu za Tanzania na CCM zikijitahidi kutushawishi na kuelezea chanzo cha matatizo na njia zinazofanya au zinavyotaka kuzifanya katika kukabiliana na wimbi la watu wanaotaka njia nyingine mbadala za kuondoa kero za muungano.

Hoja ya kuwepo kwa serikali tatu imezitingisha taasisi kuu za Tanzania kwa maana kuwa serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano bila kusahau, CCM katika kujiangalia na kufahamu mapungufu katika muungano kutokana na msukumo kutoka kwa wananchi walioitikia na kukubaliana na hoja za serikali tatu. Muda mrefu aliotumia Rais Kikwete kuongelea swala la Muungano unadhihirisha jinsi serikali yake na CCM walivyotingishwa kuhusiana na hoja ya serikali tatu.

Ninafahamu kuwa CCM watakuja na rasimu mbadala lau majibu ya hoja ya serikali tatu akini pia kutokana na kutingishwa na hoja za serikali tatu kutoka kwenye Kamati ya Jaji Warioba, lazima hiyo mbadala iwe kweli ni mbadala kutokana na political trends zinazochipuka huku zimebeba mawazo ya kukubaliana na serikali tatu. Political actions za serikali mbili na CCM kwa sasa ndizo zitakazo determine their political fate katika uwepo wa serikali mbili.

Siyo kwamba wananchi wanaotaka serikali tatu hawataki muungano, la hasha. Matatizo ya muungano ndiyo yamepelekea watu kuja na aina nyingine ya muungano wakitegemea ndiyo utakuwa mwarobaini wa matatizo ya muungano. Hii imesababishwa na matokeo ya kushindwa au kusua sua kuziondoa kero kuu za muungano kwa zaidi ya miaka 35.

Ninafahamu wale wanaotaka serikali za mkataba wana mantiki ya kuvunja muungano hasa ukiziangalia component za serikali inayoingia kwenye mkataba katika mantiki ya serikali za Tanganyika na Zanzibar.

Ngoma ya muungano iko kwa serikali za Muungano kwa sasa ambazo zinaongozwa na CCM.

Mkuu mimi nadhani kuwalaumu CCM kwa hili sio katika kuwatendea haki, ukweli ni kwamba Jaji Warioba na wenzie wamekuja na swala serikali ya tatu kama kimbilio la kuondoa kero za muungano, lakini ukitazama kwa undani utaano kabisa hakuna kero itakayotatuliwa kwa kuongeza serikali bali ni kuongeza mzozo na matatizo tuu.

Huu muungano ulikosewa tangu mwanzo kwa kutumia mfumo wa wachache wape, viongozi wetu watukufu wa awali waliukosea huu muungano, lengo lilitakiwa kuwa kutengeneza muungano ambao utamea kuwa serikali moja. Na hapa ndio waliposhindwa, na sasa leo sisi ndio tunacheza sindimba. Lakini kukosea kwao wao sio sababu ya sisi kizazi hichi kutokutafuta suluhisho. Na kutafuta suluhisho hilo lazima kufuate misingi ambayo haitoweka gharama kwa vizazi vijavyo na misingi ambayo haitokuwa na nyufa.

Swali kuu ni hili jee misingi hiyo ni ipi? Kusema kweli swala la kuongeza serikali haliingi hakilini hata kwa hao wanaotaka serikali ya tatu iongezwe. Sababu kubwa ni moja mzozo wa muungano haupo Tanzania bara, bali mzozo wa muungano upo Tanzania Visiwani. Ndugu zetu wachache wa Visiwani wamekuwa wakiona kwamba nchi yao inapoteza sura na muonekano wake sababu tuu ya Muungano. Na wachache hawa hawata ridhia sababu tuu sisi Tanzania bara tumeanzisha serikali ya Tanganyika. Vilevile, kuna Wanzazibar wengi sana walikimbilia Oman baada ya Mapinduzi hawa wamekuwa wakilaani Mapinduzi na wanasema kwamba Mapinduzi yalikuwa haramu na yalifanywa na Wasukuma kutoka Tabora kupitia Tanga, Pemba kisha Zanzibar. Hawa nao wana nguvu na ushawishi mkubwa, wameandika vitabu na vinasomwa na vitasomwa na vizazi vijavyo hivyo kuunda Serikali ya Tatu sidhani kama kutakomesha hii dhana.

Ukweli ni kwamba ndugu zanguni, hoja inapingwa kwa hoja na sio kwa ushawishi au kuitana majina kama vibaraka na mengine. Kero za muungano zilikuwepo na haziwezi kuisha sababu tumeamua sisi Watanzania Bara kuanzisha serikali ya Tanganyika. Dawa ya kutibu tatizo lilopo ni kutengeneza approach ya kuelimisha Watanzania Bara na Visiwani kuhusu faida za muungano baina pande zote.

Vilevile ni muhimu kuyakabili matatizo na kutengeneza approach ambayo itaondoa matatizo na kupunguza gharama za uendeshaji. Na kama ikafika sehemu hatuwezi ama kuboresha tulichonacho sasa, au kuanzisha serikali moja, basi kama alivyosema Mh. Raisi tugawaneni mbao tuu kwani jahazi halina kazi tena.
 
Hotuba ya JK imeweka wazi hofu moja kwa wananchi ambayo muda sio mrefu itageuka kuwa ukweli mchungu hasa kwa upinzani, nao ni kwamba Serikali tatu itayumbisha CCM na kupelekea nchi kuyumba, na hii itapelekea ombwe la uongozi wa kisiasa nchini kwa sababu hakuna chama cha upinzani ambacho kimewathibitishia wananchi kwamba kipo tayari kuziba ombwe hilo, lakini pia kulipatia taifa jipya la Tanganyika Dira Mpya (dira ya uliberali haiwezi milikiwa wala milikishwa kwa wananchi). Hii haina maana kwamba JK is right, it doesn't mean kwamba Tanganyika haihitajiki, na wala it doesn't justify taifa kuendelea kuwa chini ya mfumo mbovu wa CCM.

Kinachoendelea kuwaangusha watanzania wataka mabadiliko na kuwagharimu wapinzani, hivyo kuipa CCM muda zaidi madarakani (not neccessarily legitimacy) ni kukosekana kwa chama chenye upinzani madhubuti kiitikadi, kitaasisi na kimkakati ambacho kinatoa Dira Mbadala na yenye kuwapa motisha, ari, na matumaini ya kurekebisha historia yao kwa kuizindua Tanganyika huku chama hiki kikiwapa imani na uhakika wa 100% kwamba ombwe litakalo jitokeza baada ya CCM kudhoofishwa na ujio wa Tanganyika, ombwe hilo litajazwa kikamilifu. Nitafafanua zaidi baadae kidogo.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Vinachanganya kwa kweli, sababu tume ya mabadiliko ya katiba imefanya kazi na kutoa rasimu yake. Kimsingi tume ndio ina misingi mizuri ya hoja kwasababu ya kazi iliyopewa na uhalisia wa kwamba zoezi lili kukusanya maoni nchi nzima. Tume ndio yenye taarifa/maoni angalau yanayoelekea kwenye usahihi wa matakwa ya wa TZ. Sasa mtu mwingine ambaye yeye hana msingi kama huo anataka kutuaminishwa kwa mawazo yake ambayo pia kwa namna nyingine yanashambulia ripoti ya tume, ni mvurugano kwelikweli.

Pia mwishoni mwa kikao cha leo kwenye hilo Bunge maalumu nilisikia shukurani nyingi kwa watu mbalimbali toka kwa mgeni rasimi na baadaye msemaji maalumu kwa niaba ya wabunge. Lakini sikusikia shukurani kuelekea tume na ripoti yake ukizingatia kwamba rasimu hiyo ni moja ya msingi/njia kuu ya wao kutengeneza katiba mpya.
 
Mkuu mimi nadhani kuwalaumu CCM kwa hili sio katika kuwatendea haki, ukweli ni kwamba Jaji Warioba na wenzie wamekuja na swala serikali ya tatu kama kimbilio la kuondoa kero za muungano, lakini ukitazama kwa undani utaano kabisa hakuna kero itakayotatuliwa kwa kuongeza serikali bali ni kuongeza mzozo na matatizo tuu.

Huu muungano ulikosewa tangu mwanzo kwa kutumia mfumo wa wachache wape, viongozi wetu watukufu wa awali waliukosea huu muungano, lengo lilitakiwa kuwa kutengeneza muungano ambao utamea kuwa serikali moja. Na hapa ndio waliposhindwa, na sasa leo sisi ndio tunacheza sindimba. Lakini kukosea kwao wao sio sababu ya sisi kizazi hichi kutokutafuta suluhisho. Na kutafuta suluhisho hilo lazima kufuate misingi ambayo haitoweka gharama kwa vizazi vijavyo na misingi ambayo haitokuwa na nyufa.

Swali kuu ni hili jee misingi hiyo ni ipi? Kusema kweli swala la kuongeza serikali haliingi hakilini hata kwa hao wanaotaka serikali ya tatu iongezwe. Sababu kubwa ni moja mzozo wa muungano haupo Tanzania bara, bali mzozo wa muungano upo Tanzania Visiwani. Ndugu zetu wachache wa Visiwani wamekuwa wakiona kwamba nchi yao inapoteza sura na muonekano wake sababu tuu ya Muungano. Na wachache hawa hawata ridhia sababu tuu sisi Tanzania bara tumeanzisha serikali ya Tanganyika. Vilevile, kuna Wanzazibar wengi sana walikimbilia Oman baada ya Mapinduzi hawa wamekuwa wakilaani Mapinduzi na wanasema kwamba Mapinduzi yalikuwa haramu na yalifanywa na Wasukuma kutoka Tabora kupitia Tanga, Pemba kisha Zanzibar. Hawa nao wana nguvu na ushawishi mkubwa, wameandika vitabu na vinasomwa na vitasomwa na vizazi vijavyo hivyo kuunda Serikali ya Tatu sidhani kama kutakomesha hii dhana.

Ukweli ni kwamba ndugu zanguni, hoja inapingwa kwa hoja na sio kwa ushawishi au kuitana majina kama vibaraka na mengine. Kero za muungano zilikuwepo na haziwezi kuisha sababu tumeamua sisi Watanzania Bara kuanzisha serikali ya Tanganyika. Dawa ya kutibu tatizo lilopo ni kutengeneza approach ya kuelimisha Watanzania Bara na Visiwani kuhusu faida za muungano baina pande zote.

Vilevile ni muhimu kuyakabili matatizo na kutengeneza approach ambayo itaondoa matatizo na kupunguza gharama za uendeshaji. Na kama ikafika sehemu hatuwezi ama kuboresha tulichonacho sasa, au kuanzisha serikali moja, basi kama alivyosema Mh. Raisi tugawaneni mbao tuu kwani jahazi halina kazi tena.
Mkuu Mtanganyika ninakubaliana kiasi na wewe.

Ni kweli mtu anayeilaumu CCM kwa kutetea sera zake atakuwa hafahamu maana ya sera katika sanduku la kura. Kama CCM haiwezi kutetea sera zake ambazo ziliwafanya wananchi wengi kuipa nchi kuongoza basi itakuwa haifai kuongoza nchi.

Kuna mwingine atasema, Rais niwa Watanzania wote lakini anasahau kuwa sera alizozikataa kwa kutokumpigia kura Rais Kikwete au kwa kutokukubaliana na sera za chama cha Rais Kikwete ndizo hizo kwa sasa anaziishi. Siasa za Tanzania zinachagizwa na winner take all.

Ninakubaliana na wewe kuhusu madhaifu ya kuyakimbia matatizo badala ya kuyakabili kwa maana kwamba, CCM imekuwa ikizikimbia changamoto za muungano kama alivyoainisha Jaji Warioba. Kwa sasa matatizo yamerundikana na kusababisha hata utatuzi wake kuwa much more complicated.

Mimi ninailaumu CCM kwa kulimbikiza kero za muungano mpaka kiwango cha kuwafanya wananchi watafute ufumbuzi mwingine katika kupambana na 'kero sugu', ndiyo maana nikafikia tamati kuwa, kama hatuwezi kuziondoa, kwa nini tusigawane tu fito kila mtu akaenda zake kuliko kubaki tunalalamika lalamika tukiwa ndani ya uamuzi ambao tuna uwezo wa kuufanya.

Tume ya Jaji Warioba Imeleta changamoto ambazo watawala na viongozi inawabidi wajiandae kikamilifu katika kuzikabili. Swala la muungano kwa sasa lina ukakasi katika mazingira ya vyama vingi kwa sababu hata Katiba ya 1977 ilitengenezwa na kuendelea kufanyiwa marekebisho katika macho ya chama kushika hatamu za uongozi hata pale iliporuhusu vyama nchini.

Watawala na viongozi wetu walikuwa na bahati nzuri ya kuzikabili hizi changamoto bila kuwa na public pressure from Bara and Zanzibar lakini kwa sasa watu wa Bara nao wameamuka baada ya constant shake a leg from Zanzibaris na kujikuta malalamiko kwa sasa yanatoka pande zote za muungano.

Nilishangaa kumsikia Warioba akisema, waliamua kuwa, kuyatafutia ufumbuzi malalamiko ya Wazanzibari automatically, inayapatia pia ufumbuzi matatizo ya watu wa Bara kuhusu Muungano. Hata Rais Kikwete na yeye amekuja na hoja hiyo hiyo. Is it true?. Nina wasiwasi na mashaka na angalizo lao.

Ukiniuliza ni muungano gani napenda, hata nikiwa usingizini nitakuambia serikali moja au kuvunja muungano kwa sababu serikali tatu katika mazingira ya siasa za Tanzania ni mchakato wa kuvunja muungano katika gharama kubwa za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa nini tuingie kwenye gharama kubwa wakati tungegawana tu fito kama serikali moja imeshindikana na kila mmoja akashika njia yake.

Tumeiachia bahati kutoweka pale tuliposhindwa kwanza kupiga kura ya kuwauliza wananchi kama wanataka muungano uwepo au uvunjike. Kama uwepo, basi uwe wa serikali ngapi. Majibu ya wananchi ndiyo yangetupa mzizi wa namna ya kuandika Rasimu ya Katiba kwa sababu hata vyama vya siasa ambavyo ni wadau wakubwa wa muungano, wangekuwa tayari wanafahamu mwerekeo wa Tanzania kuhusu muungano katika katiba mpya.

Kinachofanyika kwa sasa ni marumbano kisera katika Bunge la Katiba kwa sababu vyama vya siasa vyote viliweka/vimeweka swala la muungano kama moja ya sera zao katika mlengo wa kuwabembeleza Wazanzibaris.
 
Back
Top Bottom