ALIYOYASAHAU RAIS KIKWETE
Mara ya mwisho kwa jaji warioba na rais kikwete kukutana katika suala la katiba mpya ilikuwa ni kwenye makabidhiano ya ripoti ya tume kwa rais kikwete na rais shein kwenye viwanja vya Karimjee, miezi mitatu tu iliyopita (december 30, 2013). Katika tukio hilo la kihistoria, picha mgando na video zipo zikionyesha jinsi gani viongozi hawa wawili wakiwa na furaha kwamba taifa sasa lilikuwa linaelekea kuzuri - kupata katiba itokanayo na wananchi. Katika hili, jaji warioba alitamka haya:
...Sura tano za mwanzo za rasimu ya katiba zinatokana na mchango mkubwa kutoka kwa wananchi, hasa kuhusu misingi ya taifa,tunu za taifa, maadili na miiko ya uongozi, dira ya taifa na haki za binadamu. Wananchi pia wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala wa nchi, ikiwa ni pamoja na nafasi ya wawakilishi wa bungeni.
Katika hotuba yake ya juzi, Kikwete hakuona umuhimu wa kujadili haya zaidi ya lile la wawakilishi. Katika hili, Kikwete alimsikia vizuri sana warioba siku ile pale karimjee na alielewa kwamba ni wananchi ndio waliopendekeza kwamba wabunge wapewe kikomo cha vipindi vitatu. Lakini juzi Kikwete akajadili suala hili kama vile ni wazo la warioba. Katika hili, Kikwete alitumia muda mwingi sana kuienga hoja kwamba ubunge ni grooming ground ya viongozi wa kitaifa, kwahiyo mapendekezo ya "warioba" ya ukomo wa vipindi vitatu vitazuia hilo lisitokee. Binafsi sikuwa convinced na hoja hii kwamba njia pekee ya kutengeneza viongozi wa kitaifa ni ya ubunge; hakuna scientific explanation juu ya hili zaidi ya siasa tu; isitoshe, moja ya matukio ambayo yalimfanya baba wa taifa Nyerere kuanza kung'aa kama kiongozi wa kitaifa ni pale alipokataa kuwa mbunge maslahi/mbunge wa kutumikia wanasiasa; Kama njia ya kupunguza kasi ya TANU, serikali ya kikoloni ilimteua Nyerere kwa mjumbe wa baraza la kutunga sheria (bunge) Julai 1957; aliyemteua alikuwa ni Gavana Twining; lakini baada ya miezi chini ya sita na baada ya kuhudhuria vikao viwili tu vya bunge lile, nyerere aliamua kujiuzulu kwa vile nafasi ile haikuwa na manufaa yoyote kwa wananchi ikiwa mfumo ulikuwa ni mbovu; hali hiyo tunayo leo - mfumo mbovu unaofanya wabunge wawe ni wala posho tu za walipa kodi huku wakitumika kama rubber stamp; mwalimu katika hotuba yake ya kujiuzulu alitamka haya:
I have given everything that was in my power to give and what I have given has been rejected; I came to the council expecting a little of the spirit of give and take. That spirit is not there. I would feel that I am cheating the people and cheating my own organization if I remained on the council receiving allowances and attending sundowners as an Honorouble Member, giving the impression that I was still of the service to the council when in fact I know that I am useless. I had therefore no alternative but to tender my resignation and to ask that my resignation take effect from Friday 14th December 1957, the day my last compromises were rejected by Government.
Source: Towards Ujamaa: Twenty Years of TANU Leadership, Gabriel Ruhumbika (1974).
Hapa, nyerere alikuwa amekataa kutumika kama wabunge wa ccm juzi waliokuwa wanaruka kwa shangwe na kucheza mdundiko kumshangilia Kikwete katika suala ambalo mwalimu 1957 angeenda kinyume chake - nalo ni "kukataa kutumikia status quo kwa kusaliti wananchi";
Tukiachana na mfano wa Nyerere, pia wapo viongozi kama kina Salim Ahmed Salim ambao
Nguruvi3 amewajadili. Salim hajawahi kuwa mbunge wa aina ambayo kikwete anaijadili (wabunge wa jimbo) lakini bado wanabakia kuwa ni moja ya viongozi ambao historia itawaweka kama miongoni mwa viongozi bora waliopata kutokea; mifano mingine ipo mingi - mzee pius msekwa, huyu hajawahi kuwa mbunge wa aina anayojadili Kikwete; hata leo hii, watu kama asha rose migiro, umaarufu wao ni kupitia ubunge wa kulazimisha, sio kutokana na matakwa ya wananchi; kwa kifupi, hoja kwamba kuweka kikomo cha vipindi vya ubunge kutazuia taifa kupata viongozi ni hoja ya kisiasa na isiyokuwa na tija kwa taifa;
Sambamba na hoja hii, Kikwete pia alijadili madhara yatakayojitokeza iwapo mawaziri watakoma kutokana na wabunge, kwamba shughuli zitakuwa haziendi kwa vile wabunge hawatakuwa na fursa ya kuwahoji au kubadilishana mawazo na mawaziri kwa ufanisi kama ilivyo sasa ambapo mawaziri ni sehemu ya wabunge; katika hili, Rais Kikwete hakuweza kuelezea faida za mawaziri kutotokana na wabunge, ambazo ni nyingi na tume ilizijadili kwa kina; ukiangalia hasara zilizowasilishwa na Kikwete juu ya hili kisha ukafananisha na faida zilizowasilishwa na tume kisha kufanya a cost-benefit analysis ndogo tu utabaini kwamba the benefits outweighs the costs;
Hotuba ya Jaji Warioba Karimjee wakati akikabidhi ripoti ya tume kwa Rais Kikwete na Rais Shein Desemba 30, 2013 ilihudhuriwa na viongozi wakuu wa kitaifa, marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu pamoja na mabalozi wa nje. Karibia wote hawa walikuwepo Dodoma pia. Katika hafla ile ya karimjee, warioba alisema haya:
Hii ni mara ya kwanza kwa nchi yetu kuwashirikisha kwa ukamilifu wananchi katika kutunga katiba ya nchi yao. Nia ya mchakato huu ni kupata katiba inayokubalika na wananchi. Ili katiba ikubalike na wananchi ni jambo la msingi maoni yao yapewe uzito unaostahili. Nayasema haya kwa sababu tangu rasimu ya kwanza itolewe maneno yaliyopewa uzito na wananchi hayakupewa uzito katika mijadala ya viongozi, wasomi na vyombo vya habari.
Katika hotuba yake juzi, Kikwete alianza vizuri kwa kurudia maneno haya kwamba mchakato huu tofauti na nyuma umehusisha wananchi moja kwa moja; Lakini kitendo cha Kikwete baadae kuja kujadili yaliyomo kwenye rasimu kama vile ni ya warioba inatoa tafsiri mbili: kwanza aidha Kikwete hajaisoma vizuri rasimu ile na badala yake amesomewa na wasaidizi wake; au warioba yupo sahihi anaposema hapo juu kwamba. "tangu rasimu ya kwanza itolewe maneno yaliyopewa uzito na wananchi hayakupewa uzito katika mijadala ya viongozi, wasomi na vyombo vya habari."
Kuna uwezekano kwamba maneno yaliyopewa uzito na wananchi hayajapewa uzito katika mijadala ya viongozi wa CCM, na hii ndio sababu kubwa kwanini ccm imekuwa na mtazamo kwamba rasimu hii ni ya warioba, na sio ya tume ya katiba iliyoteuliwa kwenda kusikiliza maoni ya waanchi;
Kikwete na CCM wamepuuza kabisa maneno ya warioba siku ile karimjee kwamba:
Utangulizi wa katiba unaeleza kuwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imetungwa na wananchi wa Tanzania; utangulizi unatoa taswira na picha halisi ya jamhuri ya muungano na watu wake, historia yao, matarajio yao, misingi ya taifa na masuala muhimu ambayo wananchi wanataka kuyaendeleza katika jamii, kizazi hadi kizazi.
Kwa kauli ya Kikwete juzi, tusitarajie yafuatayo kutimia baada ya mchakato wa katiba kumalizia:
"utangulizi ambao utatoa taswira na picha halisi ya jamhuri ya muungano na watu wake, historia yao, matarajio yao, misingi ya taifa na masuala muhimu ambayo wananchi wanataka kuyaendeleza katika jamii, kizazi hadi kizazi."
Katika hotuba yake juzi, Kikwete alijadili suala la serikali tatu kama vile tume ya katiba ililipendekeza bila ya kuweka maandalizi pamoja na misingi ya uendeshwaji wake; Kikwete anasahau kwamba katika hotuba ya Warioba pale Karimjee, Warioba alisema yafuatayo:
Sura ya kumi na saba inapendekeza muda wa mpito wa miaka minne, kuazia tarehe ya kuanza kutumika kwa katiba mpya hadi tarehe 31 Disemba 2018; katika kipindi hicho sheria zilizopo hivi sasa zitaendelea kutumika hadi zitakapobadilishwa. Sheria zinazotumika Tanzania bara zitakuwa za Tanganyika na sheria zinazotumika Tanzania bara na zanzibar zitakuwa sheria za jamhuri ya muungano. Yapo pia mapendekezo kuhusu masuala ya kufanyiwa kazi katika muda wa mpito. Mambo haya ni pamoja na:
1. Kutungwa kwa katiba ya Tanganyika.
2.Kurekebisha katiba ya zanzibar ya mwaka 1984 ili kuwiana na masharti ya katiba ya jamhurir ya muungano wa Tanzania ya mwana 2014.
3.Mgawanyo wa rasilimali baina ya serikali ya jamhuri ya muungano na serikali za nchi washirika.
4.Kuundwa kwa tume na taasisi za kikatiba zilizoanishwa kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2014 na kwa kuzingatia masharti ya katiba hiyo;
5.Kufanya maandalizi na kuendesha uchaguzi mkuu wa mwaka 2014 kwa kuzingatia masharti ya katiba ya jamhuri ya muungano ya mwaka 2014; na
6. Kufanya maandalizi ya mambo yote muhimu kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye katiba ya jamhuri ya muungao wa Tanzania ya mwaka 2014.
Aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya, Kikwete hakugusia kabisa maelezo haya ya warioba aliyoyatoa miezi mitatu tu iliyopita, licha ya Kikwete kurudia mara kwa mara kwamba ameisoma sana rasimu husika.
Inaendelea bandiko linalofuata...
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums