Mtanganyika
JF-Expert Member
- Jul 18, 2007
- 1,601
- 955
Mtanganyika,
Nakusoma sana na takwimu zako za ki-serengeti advisors ambazo hazitoi hata chembe za majibu ya hoja zetu kwamba: sio kweli znz hawatakuwa na uwezo wa kuchangia gharama za muungano katika yale mambo saba na hilo limeshajadiliwa kwa hoja lakini anaamua kubaki mbugani serengeti. Pili ni hoja yetu kwamba Kwa mfumo wenu, mnatuumiza walipa kodi kwani mfumo wenu una:Ya muungano, ya Tanzania bara na ya mchaganyiko; sasa kwa vile mnatuelewa, sasa mmekuja na baraza la wawakilishi wa Tanzania bara, which means mabunge matatu, serikali mbili. Kwa kweli mmelewa sana ukada. Nitakuja na takwimu zangu tena kama bado haujatembelea threads zangu za nyuma.vinginevyo una kiporo cha maswali yangu kwako haujajibu.
Na swali kwamba mfumo wa sasa ni nafuu kwa mlipa kodi kuliko serikali tatu, tuonyesheni namba? Mnajificha mbugani serengeti.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Watachangia vipi wakati pato lao la taifa ni 200 Million Dollar, matumizi ya serikali yao ni 650 Million dollar, serikali yenu ya Tatu aka Serikali ya Muungano nimewaambieni ikiwa na hayo mambo 7 itatugharim 2.5 Billion dollar. Mkiwaambiza Zanzibar wachangie 11% kama mnavyonadi hiyo ni sawa na 71% ya pato lote la Zanzibar, wao watabaki na pesa ya kuendesha nchi kwa Mwezi mmoja. Unajua any development bank haiwezi kukupa mkopo at 100% ya pato lako, sababu hakuna debt covenants yoyote inayokubali hilo.
Mkuu mchambuzi, mnataka kushona suti ya mtu mzima kwa kitambaa cha robo meter? Mwalimu alikuwa anasema "shona suti kutokana na ukubwa wa kitambaa". Kama kitambaa robo mita shona bukta tuu. Huu muungano ni kuumizana kichwa tuu.
Kinachofuata tutafanya headcount analysis ili kuwaonyesha kwamba bado gharama za kuendesha serikali mbili ni better than tatu. Sababu 21% ya budget ya Tanzania inalipa mishahara.
Kama mnataka tujadilini practicality ya serikali mbili hapo nakubaliana na hoja zenu zote. Lakini kama mnataka tujadili kuhusu cost za serikali tatu, sisi nyinyi tuu hamna jibu, Bali Jaji Warioba na wenzie wote, Juma Duni, Maalim Seif na wengine wote die hard 3 serikali hawajakaa chini wakaangalia namba.
Kumbuka usemi wa kingereza "Number don't lie" however, politician does.