hatuna tena muungano, kilichobakia ni ushirikiano
baba wa taifa mwalimu nyerere katika kitabu chake cha "uongozi wetu na hatima ya tanzania", ukurasa wa 15, mwalimu anasema hivi:
Mwalimu anaendelea kufafanua kwamba - kwa muungano wa aina ya kwanza hapo juu (serikali moja), kila nchi inafuta serikali yake na nchi mpya inayozaliwa baada ya hapo inakuwa ni nchi yenye serikali moja. Katika muungano wa pili (shirikiko la serikali tatu), kila nchi itajivua baadhi ya madaraka ambayo yatashikwa na serikali ya shirikisho, na serikali yake (iliyojivua baadhi ya madaraka) itakuwa na mamlaka juu ya mambo yaliyosalia (yasiyo ya shirikisho). Mwalimu anaendelea kufafanua kwamba - mambo yatakayosimamiwa na serikali ya shirikisho ni yale ambayo kama yakiendelea kubaki katika nchi zilizoungana:
Hali hii anayoijadili nyerere ndiyo inayoendelea leo. Muungano aliouasisiwa na karume - muungano wa nchi moja - muungano huu leo haupo tena, na hata siku kikwete anaenda hutubia bunge maalum la katiba, muungano huu haukuwepo. Kilichokuwepo siku ya hotuba ya kikwete na hata leo, ni ushirikiano wa nchi mbili huru, nchi ya zanzibar na nchi inayoitwa tanzania bara (iliyovaa koti la muungano). Misingi ya muungano haipo tena, kilichojitokeza ni ushirikiano na uhusiano wa udugu, ujirani na maingiliano ya kijamii na kiuchumi, huku uchumi wa tanzania bara (tanganyika) ukiwa ndio unabeba mzigo zaidi wa ushirikiano huu.
Kikwete juzi ameenda bungeni kupigania muungano wa serikali mbili, suala ambalo sio wananchi wengi walilipendekeza. Ushahidi wa video na sauti za watoa maoni zipo kwenye rekodi za tume. Na isitoshe, ili kuokoa muda, tume ilikuwa na utamaduni wa kuzuia wachangiaji wasirudie hoja ambazo tayari zilishazungumzwa na wachangiaji waliowatangulia, vinginevyo iwapo tume ingejua kwamba takwimu zake zingekuja chakachuliwa, ni dhahiri ingeruhusu wachangiaji kurudia hoja zile zile, hivyo matokeo yangekuwa ni makubwa zaidi (wanaotaka serikali tatu). Ushahidi wa hili upo, na ilitokea hivyo licha ya ccm kujaza watu wake kwenye mabaraza ya katiba. Pengine kwa kujua hili, ndio maana ccm inajitahidi kupotosha umma juu ya takwimu za tume kwani inajua itaumbuka kwenye kura ya maoni. Yale yaliyozuiliwa tume yatajitokeza kwenye sanduku la kura.
Katika pita pita zangu mitaani, nimegundua kuna uelewa mkubwa sana miongoni mwa wananchi kwamba nchi mbili zilizoungana 1964 kuwa nchi moja, kwahiyo nchi mmoja haiwezi kuwa na mamlaka kamili halafu bado tukasema tupo kwenye muungano ulioasisiwa na nyerere na karume. Kilochopo sasa na uhusiano na ushirikiano tu ambapo mshirika mmoja ndiye anayetoa zaidi. Isitoshe, hivi leo, i vigumu kutofautisha kwa asilimia mia moja yepi ni ya muungano na yepi ni ya tanzania bara. Hata tume ya warioba imeeleza hili kama sababu moja wapo ya kupendekeza serikali tatu.
Hatua ya zanzibar (2010) kujichukulia mamlaka ya muungano tena kimya kimya maana yake ni kwamba hakuna muungano wa nchi mbili. Tazama katiba ya znz (2010) na ya sasa ya jmt (1977) zinavyopishana.
Ccm haitaki kukubali ukweli - zanzibar imejiondoa katika muungano wa serikali mbili ulioasisiwa na nyerere na karume, na kujitangazia mamlaka yake kamili. Kinachotakiwa kufanyika ili kulinda muungano ni kwa mshirika wa pili wa muungano (tanganyika) kuzinduliwa ili hali iendane na katiba ya znz na pia rasimu ya katiba. Isitoshe, hili suala sio geni na wala sio la warioba bali ni la mkataba wa muungano (1964). Vinginevyo ccm kuendelea kung'ang'ania muungano ambao mshirika mmoja amepora mamlaka ya muungano ni kutaka kuuvunja muungano uliopo. Hakuna jinsi ya kurekebisha hili zaidi ya kuizindua tanganyika - serikali tatu, la sivyo muda sio mrefu muungano utavunjika tu kwa sababu:
Kitendo cha ccm kulazimisha muungano wa serikali mbili wakati umma tayari unajua kwamba hakuna tena nchi moja alizoacha mwalimu bali kuna nchi mbili na serikali mbili kwa kweli ni kutaka kupandikiza chuki miongoni mwa wananchi wa "tanzania bara". Na atakaye beba lawama iwapo vurugu na maafa yatatokea itakuwa sio mwingine bali ccm.
Taratibu umma unaanza kuelewa kwamba misingi mikuu ya dola ni:
1.watu
2.ardhi
3.mamlaka kamili, na
4.uhusiano wa kimataifa.
Zanzibar kupitia katiba yake ya 2010 ipo katika hatua za mwisho kabisa za kufanikisha masuala haya, na hakika hawawezi rudi nyuma. Ili kurudi nyuma, katiba yao inaelekeza ifanyike kura ya maoni ambayo itahitaji robo tatu ya kura kufanikisha hilo. Hilo kamwe halitatokea kwani the "union question" has always been the "zanzibar question"; ndio maana hata tume ya warioba baada ya kujiridhisha na umma wa wazanzibari na pia viongozi wao na opinion leaders, ikawa dhahiri kwa tume kwamba kura ya maoni haitaweza badilisha safari ya zanzibar waliyoanza 2010. Lakini kama alivyojadili
nguruvi3, hotuba ya jk juzi iliacha kabisa kugusia suala hili muhimu.
Kwa vile zanzibar haiwezi kurudi nyuma kwenye suala la muungano wa nchi moja, sasa ni wakati wao kuelewa kwamba hatua hiyo haitoshi kwani bila ya tanganyika, zanzibar yenye mamlaka kamili haiwezekani.
Tanzania kwanza, tanganyika kabla.
Sent from my blackberry 8520 using jamiiforums