Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #141
Mwongo mkubwa! Usiudanganye umma. Lazima ujiridhishe na maandiko kabla ya kuandika. Katika jukwaa hili ustaarabu hutamalaki na ni nadra kusoma neno kama muongo. Kwako tunalitumia kwasababu huoenkani kuliheshimu jukwaa.Nilipo underline,
Naomba nikusahihishe kidogo.
Pesa za waliokuwa wafanyakazi wote wa EAC zilitolewa na UK baada ya tafiti na kujua stahili za wafanyakazi wote kutokana na mishahara yao na nchi wanazotoka na zikapelekwa kwa nchi zote husika. Kenya na Uganda waliwalipa kama ilivyoelezwa katika mchanganuo wao. TZ walizitumia katika Vita ya Uganda na hivyo kutowalipa wastahafu hao mpaka leo.
Jumuiya ya Afrika mashariki ilikufa mwaka 1977.
Vita ya Kagera ilikuwa 1978 chini ya mwaka mmoja tangu EAC ivunjike.
Dr Victor Umbrich alimaliza mediation of assets and liabilities of the defunct EAC mwishoni mwa miaka ya 1988-90.
Baada ya taarifa ya Victor Umbrich mgawanyo wa mali ukamalizika na kuundwa chombo kingine cha kuangalia namna ya uhusiano wa siku za baadaye. Wakati huo waliokuwa madarakani ni Ali Hassan Mwinyi, Moi na Museveni.
Nyerere hakuwa madarakani wala Amin hakuwepo Uganda. Hiyo research iliyofanyika umehadithiwa bila kuingia maktaba kujiridhisha na ulichosikia mitaani. Haiwezekani jumuiya ife 1977 na mwaka 1978 research imekamilika. Na labda ujiulize UK ilitoa pesa katika misingi gani. Hadithi za mitaani kwa mtu wa doctorate level ni aibu.
Wafanyakazi wa nchi nyingine walilipwa miaka zaidi ya 15 baada ya kifo cha EAC.
Sijui inakusaidia nini kusema uongo. Tafadhali sana jiridhishe na unachoandika. Too low