TUACHE UPOTOSHAJI KUHUSU ZANZIBAR KUTOKUWA NA UWEZO WA KUJIENDESHA NA KUGHARAMIA MUUNGANO
Hoja juu ya uwezo wa zanzibar kujitegemea ni hoja iliyojaa mantiki za kisiasa zaidi kuliko kiuchumi. Hoja hii imejaa upotoshaji kuliko ukweli, upotoshaji unaoongozwa na kina
Gamba la Nyoka na wenzao kwa nia ya kuwatisha wazanzibari wasiendeleze harakati zao za kurudi katika mkataba wa muungano wa 1964 ambao uliweka wazi mazingira ya serikali tatu - machache ya kuchangia kwa pamoja kishirikisho, na yaliyobakia kila nchi shiriki kuyasimamia kivyake. Huko nyuma tulijadili suala hili, lakini kama anavyosema
Nguruvi3, kina
Gamba la Nyoka waa utamaduni wa kukimbia hoja, kisha baada ya majumaa au miezi kadhaa, wanarudi humu kurudia hoja zile zile dhaifu.
Kabla ya Mwaka 1964 (mwaka wa muungano), zanzibar ilikuwa ni taifa huru kiuchumi na kisiasa. Lilijiendeshea mambo yake yenyewe, and in actual sense, zanzibar huko nyuma ilikuwa ni moja ya economic power houses barani Africa, ikiwa katika ligi moja na nchi kama Ghana na Misri in terms of economic performance and activities. Hata Tanganyika haikuwa inafua dafu kiuchumi mbele ya Zanzibar, sasa kwanini leo tuseme zanzibar haitakuwa na uwezo wa kujiendesha? Huku ni kuitusi zanzibar kwani wananchi walipomwaga damu kupigania mapinduzi yao, hawakufanya hivyo ili waje baadae kuwa tegemezi kwa Tanganyika.
Ni baada ya muungano tunaona zanzibar ikianza kubadilika kiuchumi. Hii ilitokana na muungano kuwa na sura ya kisiasa zaidi ambapo uchumi ukafanywa mtumishi wa siasa za muungano. katika hali hiyo, masuala ya uchumi yakawa treated kama masuala ya muungano ambayo yakapangwa to be shared equally na pande zote mbili za muungano. Hadi hapo zanzibar ikawa na uchumi imara tu ambao ungeweza kujiendesha na pia kuchangia gharama za mambo (11) ya muungano.
Kilichofuatia baadae katika historia I kuona zanzibar ikichangia mara tatu tu katika gharama za kuendesha muungano - 1964/5, 1965/6, 1966/7, na kila mwaka kiasi kikizidi kupungua. Sasa kina
Gamba la Nyoka wanakuja na viroja hapa pengine kwa kutazama suala hili lakini wanasahau kwamba muda mfupi baada ya muungano, zanzibar ikapewa kilimo cha uchumi na Tanganyika (iliyovaa koti la muungano) kupitia sheria namba (9) ya tarehe 1/5/1964. Sheria hii ilitoka kama amri na haikushirikisha viongozi wa zanzibar bali wa Tanganyika kwa kutumia mamlaka iliyopewa Tanganyika ya kipindi cha mpito. Sheria hiyo ni kama ifuatavyo:
TANGAZO LA SERIKALI Na. 246 lililochapwa 1/5/1966.
SHERIA ZA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, 1964.
AMRI
Kwa mujibu wa vifungu 3(b) na 8 Vya Sheria Zilizotajwa
AMRI YA UTARATIBU WA KIPINDI CHA MPITO, 1964.
1. Amri hii itajulikana kama amri ya utaratibu wa kipindi cha mpito 1964, na itaanza kutumika siku ya muungano.
2. Amri hii itasomwa kama sehemu ya katiba ya muda.
....
....
....
9. Mali na Mikataba:
Mali zote na haki juu ya mali za jamhuri ya Tanganyika na mali zote na haki juu ya mali za jamhuri ya watu wa zanziba zilizokuwa zinamilikiwa au kutumiwa au zilizomilikiwa au kutumiwa kimsingi kuhusiana na mambo ya muungano, zitakuwa kuanzia siku ya muungano chini ya jamhuri ya muungano.
Kimsingi, kupitia sheria hii, assets zote za zanzibar pamoja na savings zake kubwa sana kwenye benki moja huko uingereza, zikahamishiwa kwenye himaya ya muungano. Zanzibar ikabaki kapa in a blink of an eye. Na sheria hii inasema kwamba itaanza kutumika siku ya muungano wakati mkataba ukiwa umeshasainiwa. Huu ulikuwa ni uchakachuaji mkubwa ulioipa zanziba kilema cha uchumi hadi leo. Kina
Gamba la Nyoka,
Nape Nnauye na wengine hawajui haya.
Zanzibar ndio ilikuwa kwanza imetoka katika mapinduzi, na haikuwa hata haija thaminisha mali zake na akiba yake kubwa kwenye benki huko London (Narodny Bank). Akiba ya Zanzibar by the time Karume anafariki 1972 ilikuwa about 25 Million Pounds Za mwingereza. Fedha hizi zilichangiwa na bei nzuri ya karafuu soko la dunia ambapo ilirurka kutoka $550 kwa tani miaka ya mwanzo ya mapinduzi na kufikia $1,500 kwa tani 1967-8; Karume alitumia fedha nyingi kujengea wananchi makazi, miundo mbinu kwa mafanikio makubwa;
Fedha na mali zote hizi zikachukuliwa na Tanganyika iliyovaa koti la muungano. Lipo suala lingine la kifedha ambapo Zanzibar Bank ambayo ilitakiwa iwe ni benki kuu ya zanzibar, nayo ikavurugwa na sheria za muungano.
Licha ya yote haya, leo zanzibar bado wana uwezo wa kusimama kiuchumi kwa mafanikio tu kwani uchumi unategemea natural resources, human capital, leadership na political will among others. Zanzibar wana rasilimali nyingi tu - wana mafuta, gesi, utalii, uvuvi, a free port, kutaja vichache tu. Lakini yote haya yamevurugwa na muungano wa kisiasa. Kwa mfano, Katiba ya muungano (1977) haisemi hadi leo zanzibar watanufaika vipi na rasilimali zake, na wala haizungumzi economic justice za wazanzibari. Uchumi na rasilimali zinatajwa kijuu juu tu na kisiasa.
Iwapo zanzibar watapewa fiscal and economic autonomy, hakuna shaka kwamba wataweza kuamka kiuchumi pengine kuliko hata Tanganyika. Sisi Tanganyika hatuna nia ya kujenga uchumi wa wananchi, je Zanzibar wakiamua to build a strong domestic economy kwa manufaa ya wananchi, kwanini wasifanikiwe? Haitachukua zaidi ya miaka 15, tutabaki midomo wazi. Lakini ni iwapo wataamua leo na wataendelea na juhudi zao zilizoanza na katiba yao ya 2010.
Kuna many wealthy small islands in the world ambazo zilikuwa na chanhamoto kama tu zanzibar kwa maana ya idadi ndogo ya watu na eneo dogo la ardhi, lakini kwa vile they had political will, leo sio tu wapo huru kiuchumi, bali pia wapo mbele sana ya nchi kubwa na zenye rasilimali zaidi yao.
Zanzibar ina urefu wa kilometa 1,500 na upana wa kilometa 30, huku idadi yake ya watu ikiwa ni karibia 1.4 million. Tufananishe na nchi jirani yake ya Mauritius:
Mauritius ukubwa wake haufikii zanzibar, ni kama robo mbili tu ya zanzibar - ina urefu wa Kilometa 45 na upana wa kilometa 65. Lakini bado it performs better sio tu zaidi ya Zanzibar bali Tanzania kwa ujumla. Most major economic and commercial indicators zinadhihirisha ukweli huu. Kwa mfao, kwa mujibu wa World Economic Forum's Travel and Tourism Competitiveness Index ya hivi karibuni juu ya Middle East and Africa, Mauritius wapo ranked top FIVE, wakati Tanzania ipo ranked 19th. Tanzania hii hii yenye wanasiasa wanaobeza potentials za nchi ndogo wakati chini ya utawala wao, "ukubwa wa pua haujawahi kuwa wingi wa makamasi". Vile vile, kwenye Global Index, Mauritius is 40th, Bwana mkubwa Tanzania is 98th.
Tukumbuke kwamba tofauti na Tanzania yenye kila aina ya vivutio vya kitalii - mbuga za wanyama, mlima wenye barafu south of equator, olduvai gorge alipopatikana binadamu wa kwanza,Mauritius hawana vivutio vya maana kama hivi lakini bado wanapokea watalii wengi kuliko Tanzania kwa zaidi ya asilimia ishirini. Kwa mfano, Takwimu za World Tourism Organization zinaonyesha Tanzania hupokea watalii 700,000, na Mauritius watalii 900,000.
Pia katika "Doing Business Report", inayoangalia ease of doing business/ubora wa mazingira ya kufanya biashara, Mauritius is 17th in the world, sisi Tanzania na ukubwa wetu wa pua, we are 131st.
Mauritious ina GDP ambayo ni nusu tu ya Tanzania (kama USD 12 Billion, compared na ya Tanzania inayovuka USD 25 Billion sasa), lakini bado wananchi wa mauritious wana maisha bora kwa mbali sana ikilinganishwa na Watanzania. Wananchi wa mauritious ni miongoni mwa wananchi wenye hali bora za maisha sio afrika tu bali katika nchi zinazoendelea. Isitoshe, na udogo wao, hawapo tena katika low income countries bali middle income. Tanzania na ukubwa wetu wa pua, hii bado ni ndoto licha ya matumaini mengi wanayotoa wanasiasa kwa wananchi.
Tusiwatishe wazanzibari, bali tuwape moyoo kuelekea autonomy and self determination kwani hivyo ndivyo na Tanganyika itapatikana na kupelekea uwepo wa muungano unaoendeshwa kwa ushindani and with less waste of resources tofauti na mfumo mbovu wa ccm na serikali zake mbili zisizo na tija.
Wazanzibari should be inspired by the likes of Mauritious, tusiwakatishe tamaa, tusiwatishe. Isitoshe, wakiamua kufungua kesi ya madai ya uchakachuaji wa mali na akiba zake nilizojadili, ndani ya serikali ya ccm hapatatosha.
Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.
Mtanganyika,
Bongolander,
MwanaDiwani,
ZeMarcopolo,
zomba,
Nape Nnauye,
Mwigulu Nchemba
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums