Mtizamo wangu pia nikuwa, Tanzania siyo kisiwa, kiasi cha kujifanya tunaweza kujitegemea. Tuwe wakweli juu ya hili. Tusidhani ni hili tu bali litakwenda kutuharibia hata mahusiano yetu mengine. Mimi ninaamini Tanzania tukiingia wenyewe mkataba huo na sasa tumeshindwa masharti hivyo tunastahiki kufanyiwa hivyo wala yusijifari kwa kunakili maneno ya mwakimu ili kutupa public support. Miradi mingi itasimama na sisi hatuna ujanja wa kuiendeleza. Mimi ninamuomba Mh. Rais Magufuli asidanganyike na washauri wasioitakia mema nchi hii . Ajitajihidi kushughulkia suala hili kwa hekima kwakuwa ninajuaana hekima hiyo. Fedha hizo za MCC tunazihitaji sana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote ule, ukizingatia chama chetu kimeahidi mambo mengi kuwafanyia wananchi. Mwalimu pamoja na kauli zake lakini aliizita nchi hizi ni giant kama hatutashikana nazo sisi wadogo tuta umia. Hivyo huo ndy wito wangu. Tuache kupotosha ukwelu