Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

tufike sehemu tujikubali,,ipo siku watatuonea wivu,,ndipo misaada yao haitakuwa na mashart makali,,mcc safar njema natambua ipo siku mtarud kwa jina lingine namsipe nafas kirahis kama mlivyo ingia.

Tujadili hoja ya kwa nini tumenyimwa msaada wa MCC. Kama marekani walikuwa wanatulazimisha ndoa za jinsia moja, hapo tungeungana kuukataa msaada, lakini ccm imefanya uhuni Zanzibar halafu mnataka watu na akili zao wawapongeze? Yeyote anayeitakia amani nchi hii na mzalendo wa kweli lazima alaani upuuzi uliofanyika Zanzibar. Ku quote maneno ya Nyerere juu ya ubeberu hakuna uhusiano na yaliyofanywa na marekani kutaka kauli ya wananchi iheshimiwe. Je Nyerere angekuwa hai leo angeshabikia ubakaji wa demokrasia uliofanyika Zanzibar? Bw. Polepole, huna hoja zaidi ya kuunga mkono waliokununua.
 
Huyu Polepole hajui asemalo
 
Kwanza mambo Vipi Bro? Hivi Aggrey yuko wapi sikuhizi? Vipi bado Ni kipanga Ktk Sector anayodeal nayo Kwa Sasa! Mwambie ndugu yako mlikuaga wote Enzi Za primary MPS pale anakusalimia sana!

Tukija kwenye Mada; umeongea point mno Ila swali Ni hili " kwanini hukuzungumza yote haya from day one?

Lingine; Uko tayari kuvunja uhusiano Na MCC Kwa maslahi ya Chama?
 
Mafisadi hawataki kukosolewa,wantk waendelee na ubabe wao kwa kisingizio cha kutotaka kuendeshwa na mabeberu
 
Polepole hujipambanua kama kijana lakini sura yake inakanusha hilo.... Midomo yake anapoongea huchezacheza kufurahisha tumbo lake...macho yake hupeleka picha tofauti katika ubongo wake hivyo macho huona kingine lakini ubongo hutafsiri picha nyingine.... samahani lakini sikusoma aliyoyaandika maana hakawii kuyapinga tena....
 
Mimi ninachokataa ni kuweka UWINGI kwa kitu kinachofanywa na watu wachache! Kati ya Watanzania milioni 45 ni wangapi wamechangia katika hayo magazeti? Sana sana hawazidi hata laki moja ukijumlisha CUF na UKAWA Bara!

Jaji Warioba alisema nini kuhisu marudio ya uchaguzi visiwani?
Dr Salim Ahmed Salim alisema nini kuhusu marudio ya uchaguzi?
Bernard Membe alisema nini kuhusu marudio ya Uchaguzi?
Fatma Karume alisema nini?
Mzee Butiku alisema nini kuhusu marudio ya uchaguzi ?

Je hawa wote ni ukawa?Au umeamua tu kubisha?
Jaribu kufanya uchunguzi kwanza kuhusu hili.
Kuna vitu unaweza kujumlisha moja na moja ukapata jibu.Kwa mfano ukifatilia vyanzo vya habari utagundua Rais magufuli anakubalika hata kwa wapinzani.Hivyo hivyo ukifatulia vyanzo vya habari utagundua wengi wanalaani uchaguzi wa Jecha.
 

Kwanza, Polepole hakuwa na sababu ya kuandika text ndefu kama hii. anarudia yanayofahamika miaka yote na kwa wengi ndani ya JF.

Tatizo langu kwako Polepole, unaandika kama mwanasiasa wa miaka ile ya elimu ya kujitegemea. Nahisi unajadili mambo ambayo ni zaidi ya uwezo wako. Amini hilo! Unapozungumzia Egypt inakupa faraja gani wakati uhusiano huo una sababu tofauti. Hii ni dunia ya mashindano na urafiki sasa wewe unapotaka misaada na wakati huo unadai uwe huru kuajili makampuni ya kichina, huo ni uzembe. Hayo yanajulikana miaka yote. Huwezi ukapewa pesa za British council ukasome chines language. Hii ni miaka ya Obama kuingia Cuba. Ni miaka ya globalisation. Hii ni nchi yenye negative forex income tofauti na zile tunazopeleka nje. Tz inahitaji forex kuliko jeuri ya kisiasa ambayo haina faida kwa waTZ wote bali kwa hao wanaofaidika na ikulu.

Ushauri wangu kwako ni jinsi gani utaweza kulinda uwezo wa kufikiri. Ulipewa sifa wakati wa Tume ya Warioba, tatizo ukaharibu baada ya kuonekana kwamba hukuwa unazungumza akili yako. Sasa ndugu yangu ni vigumu sana kupata heshima au kusikilizwa kwa kutegemea reasoning yako tuu! Sit down and assume those glory days are gone!
 
Mr pole pole siku hiz umekuwa mchumia tumbo hakuna anaekusikiliza hata walokuahid ukuu wa wilaya wamekutosa kwa miaka zaid ya 50 nchi hii imeongozwa na chama chako hamkujua kuwa tunaweza kujitegemea? Rais wenu kla cku alkuwa anasafir kwann hamkumshaur kuna misitu asiende kuomba? Tatzo lako ubongo umejaa funza huwez kugundua now madhara yke hebu jarbu kuwa kijana wa wakat ule usiwe kijana wa kuolewa mombasa utapotea..
 
Povu linawatoka , fedha za watu, mtaambiwa muwe mashoga sijui mtakubali. Tulieni fanyeni kazi mlipe kodi. Mnapenda kula vya bure eheeeeee,haya.Leo wanakuja na utawala bora ,kesho watakuja na hilo gumu ,sasa wazungusha mikono kazi mnayo.
 
Mimi nadhani tungejikita kwenye sababu za kusitisha hiyo misaada. Kwanini CUF wamepokwa ushindi wao Zanzibar?
 
Ongeza juhudi wakati wowote jina lako litawekwa kwenye orodha ya ma DC wapya!
 
nani aliomba?
Usihemke japo humpendi Polepole lakini hoja yake ni nzito kuliko za kina Kabwe ambao wapo bungeni na walipiga kura kupitisha moja ya hayo mapoungufu

Jakaya Mrisho wa CCM na Rais wa awamu ya nne kwa niaba yetu sote watanzania, ndiye alikuwa karibu nusu ya siku za kila mwaka yuko angani hata tukamwita Mr FastJet akitembeza bakuli!

No, mimi sijasema simpendi Mr Humphrey Polepole......wewe ndiyo unanitafsiri hivyo. Labda tofauti yangu na huyu jamaa ni kutofautiana naye kimitizamo katika baadhi ya mambo.

Hii haiwezi kuwa kutompenda mtu!!
 
Pole pole alishajitoa ufahamu, anachotuaminisha ndicho sicho, mimi huyu bwana namfananisha na Samwel Saba, pia namfananisha na yule wa Zenj aliyefuta matokeo, hana lolote huyo!
 
Pumba tupu
 
Pole pole alishajitoa ufahamu, anachotuaminisha ndicho sicho, mimi huyu bwana namfananisha na Samwel Saba, pia namfananisha na yule wa Zenj aliyefuta matokeo, hana lolote huyo!

watu wanaitoa sadaka Nchi na Wana wa Nchi wake kwa ajili ya chama cha siasa na wanachama wake!!!!!

hivi nchi hii imeanza kuwepo lini na hii ccm imeanza kuwepo lini?
Si kwamba Nchi ni ya milele mpaka hapo ulimwengu utakapokoma? Je chama cha siasa nacho ni cha milele?

Kila ninapomsikiliza Mhe Maguful kwa kauli na matendo yake napata imani kuwa ndani kabisa ya moyo na ubongo wake Mhe Rais Magufuli haamini katika ubabe uliofanyika Zanzibar na hapendi matokeo yake haya yanayotokea. Ni wahafidhina tu wa CCM wanamlazimisha kufanya mambo yanayoigharimu nchi pasipo maana wala ulazima wowote.

Mhe Rais Maguful chukua maamuzi magumu ya Kimalawi kama ikibidi. Chama hakiwezi kuwa kikubwa kuliko Nchi..hiyo haiwezekani.
 
Eewa mantiki ya argument, si kwamba we have nothing to lose we will lose obviously.
Lakini mtu akitaka kukuchukulia mkeo kwa vile anakufadhili, siiku nyingine hata heshima ya kutetea utu wako unakuwa huna!!
Ndy maana nimesema sijamuelewa mtoa mda!!!
Mpaka ukubali kufadhiliwa ni kuwa una tatizo,unahitaji msaada kwahiyo kama mkeo ndiyo collateral ya huo ufadhili ukubali tu
 
Watanzania tuna ugonjwa sana wa kulilia misaada. Kenya walinyimwa misaada miaka kadhaa iliyopita, lakini bado walijiendesha wenyewe tena kwa ufanishi hadi watoa misaada hao wakafukuzana kurudi kwa aibu. Tujifunze kujitegemea, halafu misaada iwe ni nyongeza tu, siyo tuwe tunaishi kwa misaada miaka yote.
 
Mbaya zaidi, Humphrey anasemaJecha alikuwa
sahihi kisheria na kikatiba kufuta uchaguzi. Ansahau kuwa mpaka sasa Jecha hajasema alitumia sheria ipi na kifungu kipi cha sheria, wala hattaji chapter y a katiba aliyotumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…