Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Mbaya zaidi, Humphrey anasemaJecha alikuwa
sahihi kisheria na kikatiba kufuta uchaguzi. Ansahau kuwa mpaka sasa Jecha hajasema alitumia sheria ipi na kifungu kipi cha sheria, wala hattaji chapter y a katiba aliyotumia.

Polepole is a nincompoop, period
 
Hizo dola bil 3 kwa Egypt & billion 6 kwa Israel ni za mfuko wa MCC? Acha kuchanganya mambo na kujivua ufahamu. Mmeshawapora waZNZ haki yao ..endeleeni tu kusheherekea na kupeana nyadhifa
Hatuangalii ni mfuko gani kwani huko misri anatoa pesa hizo mburundi,au wakenya na mcc zinatoka burundi au japani
 
Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

I
Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Kwa uwandishi huu TRUMP hajakutukana itakuwa kakusifia, Naona sasa unakula na Watawala kelele zote kwisha, hay Kutesa kwa zamu.Leo CCM imekuwa nzuri.

Hivi kwa wewe uliyejipambanua kama mtetezi wa katiba ya wanyonge leo UMEKENGEUKA NAMNA HII ?
 
Sikuhizi ni shida ana kujadili na watu humu, hivi kwanini hamfikir kabisa?

Mmarekani natoa Hela Misri kubariki Ubakaji wa Demokrasia na ni kw amslahi yake OVU na Kuilinda Israel.

Je ulitaka na Tanzania-CCM wapewe hela pia kwa kubaka demokrasia Huko znz na huku bara?

Embu tufikiri kwanza kabla ya kuandika.
 
Mtaisoma namba na hapo bado hadi wahisani wote wapige pini misaada yao yote na bajeti yenu ndio inahitaji 40% ya fedha za kigeni ( wafadhili )sijui mtaishi vipi,kisa sheni?
Waziri wa fedha keshasema walikuwa hawakuzihesabia fedha za MCC, baada ya kuonyesha ugeugeu tangu November mwaka jana.
hata hivyo ifikie hatua hatutaitaji misaada , tunachapa kazi na kujitegemea wenyewe.
 
KUHUSU MCC KUSITISHA MSAADA WA MCC 2 NA SHUGHULI ZAKE TANZANIA: MTIZAMO

Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi. Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

Watanzania tuna ugonjwa sana wa kulilia misaada. Kenya walinyimwa misaada miaka kadhaa iliyopita, lakini bado walijiendesha wenyewe tena kwa ufanishi hadi watoa misaada hao wakafukuzana kurudi kwa aibu. Tujifunze kujitegemea, halafu misaada iwe ni nyongeza tu, siyo tuwe tunaishi kwa misaada miaka yote.
Kwahiyo mkuu unataka kuiweka Tanzania na Kenya kwenye uzani mmoja?
 
Sipo tayari kuvaa koti la uzalendo wa kipuuzi linalotangazwa na CCM! MCC haiuzi uhuru wa Tanzania bali inapambana na uhuni wa CCM na watu wake! Mimi simo kwa wana CCM wanaoungana kujifariji na matokeo ya uhuni wao kule Zanzibar! Hilo ni la wana CCM na kamwe msihusishe watanzania wengine!
Wehu....kweli wameshavulugavuluga ss leo wanataka watuveshe koti la uzalendo kama kawaida yao........siku zote viongoz wa nchi hii hawajawah kuwa wazalendo ila wanatakaga wananchi wabebe uzalendo...wao wanatumbua tuuu....mara escrow....mara epa afu baada ya hapo wanatuimbisha ss wimbo wa uzalendo.....
 
Kama hautokuwa tayari kuwa mzalendo ndani ya nchi yako hupaswi kujivunia kuitwa mtanzania....mtu yotote mzalendo huwa tayari kuzungumza kutetea maslahi ya taifa lake ndiyo maana mzalendo kama kafulilila alikuwa tayari kuzungumza ili taifa lisongembele na siyo wachache wafaidike
 
We pole pole acha kujichetua akili na kutuletea propaganda zako hapa za si zitak mbichi hizi....hiv munatuona watanzania ss ni mazezeta na mliosoma ni ninyi tu mnaokesha kwenye vyombo vya habar munatoka povuu.....jua kwamba huwa tunawachora kupima level zenu za ujinga.....ili kujua munazidiana ujinga kwa kias gan......unaleta porojo nyingiii unazan ss hutujui hizo historia.....unazani hatujui kilichotokea Zanzibar? Na unazani hatujui kipi kimetufanya tukose hyo pesa? Na unazan hatujui kipi serikali yetu piga ua galagaza haiwezi kukifanya bila msaada kama huo wa mcc? Unazan hatujui pato la nchi yetu? Ss acha kabsa kutufanya ss watanzania mijinga......tunaelewa....na tunajua kazi ya propaganda kama hyo unayotuletea hapa
 
Mbaya zaidi, Humphrey anasemaJecha alikuwa
sahihi kisheria na kikatiba kufuta uchaguzi. Ansahau kuwa mpaka sasa Jecha hajasema alitumia sheria ipi na kifungu kipi cha sheria, wala hattaji chapter y a katiba aliyotumia.
Mkuu muda mwingine unaweza kupata ukakasi hata kujadili na watu kama Polepole maana jamaa kujipendekeza kumezidi hadi akili imemmuishia kabisa.
 
We pole pole acha kujichetua akili na kutuletea propaganda zako hapa za si zitak mbichi hizi....hiv munatuona watanzania ss ni mazezeta na mliosoma ni ninyi tu mnaokesha kwenye vyombo vya habar munatoka povuu.....jua kwamba huwa tunawachora kupima level zenu za ujinga.....ili kujua munazidiana ujinga kwa kias gan......unaleta porojo nyingiii unazan ss hutujui hizo historia.....unazani hatujui kilichotokea Zanzibar? Na unazani hatujui kipi kimetufanya tukose hyo pesa? Na unazan hatujui kipi serikali yetu piga ua galagaza haiwezi kukifanya bila msaada kama huo wa mcc? Unazan hatujui pato la nchi yetu? Ss acha kabsa kutufanya ss watanzania mijinga......tunaelewa....na tunajua kazi ya propaganda kama hyo unayotuletea hapa
Mcc imeanza 2008 kabla ya hapo tuliishije jiulize
 
Mkuu muda mwingine unaweza kupata ukakasi hata kujadili na watu kama Polepole maana jamaa kujipendekeza kumezidi hadi akili imemmuishia kabisa.
Ukweli haupendwi na waongo sisi tunapenda ukweli ongera polepole
 
Pole pole wakati mwingine uchague kukaa kimya hasa mambo yanapoborongwa na chama chako!
Heshima yako inaporomoka kwa kasi ya ajabu!
 
Tatizo ni pale mtu anapoangalia hii suala kama la kupandikizwa kutoka nje bila ku address habari za uhuni uliofanyika katika uchaguzi wa Zanzibar na sharia Draconian za kuvunja uhuru wa habari.

Mtu mzima anatetea Jecha alivyofanya uhuni usiofuata sharia wala katiba Zanzibar?
 
Pole pole wakati mwingine uchague kukaa kimya hasa mambo yanapoborongwa na chama chako!
Heshima yako inaporomoka kwa kasi ya ajabu!
Pole pole mzalendo kwenye ukweli anaongea awali mlimsifia sana kwa sababu tu alikuwa awaseminyinyi sasa hivi mnamuona mbaya kwa kuwa mnataka awaunge nyinyi....jamani kama mtakuwa hivyo upinzani hii nchi muisahau
 
Back
Top Bottom