Uchambuzi wa MCC kesho Times FM
Kesho tarehe 31 Machi 2016, saa 1 Asubuhi nimealikwa na Times 100.5 FM. Huko nitafafanua sintofahamu na taharuki ya kusitishwa kwa awamu ya pili ya Msaada wa MCC. Nitaelezea historia ya MCC, historia yake na Tanzania, MCC Awamu ya Kwanza, na aina ya miradi iliyotekelezwa nchini na Awamu ya Pili ambayo imesitishwa (hakuna mradi uliotekelezwa). Nitaeleza tofauti ya MCC 1 and ambayo iliyokuwa inakuja kuwa MCC 2.
Kubwa ni kwamba Maisha lazima yaendelee katika Tanzania na hasa tukiendelea kuheshimu uhuru wetu na uwezo wetu wa ndani kufanya maamuzi yetu pasina kuingiliwa na mtu au Taifa lolote.
Watu wengi wanapotoshwa juu ya nini MCC 2 ilikuwa inakuja kufanya Tanzania, nitafafanua kwa kina kesho.
Kujitegemea na kujenga uwezo wa ndani kujitegemea na kupeana morali huu ni zaidi sana kuliko kulia lia na Msaada ambao haujaja.
Huu ni wakati wa kuwa Mtanzania Kwanza.
Usikose, Mjulishe na Mwingine, Please SHARE