Mtazamo: Kuhusu MCC kusitisha msaada wa MCC 2 na shughuli zake Tanzania

Naishauri serikali iwe strong na isonge mbele najua kisaikojia na kiuchumi vitatusumbua lakin hutuwez anguka,pia serikali iwatazame vizuri wapinzani huwa katika nchi nyingi za kiafrika zilizo ingia migogoro na wahisan chanzo ni hawa watu kwahiyo ubandidu ni muhimu mm nawaona hata humu mitandaoni serikali inatengeza mikakati mahususi wao wanahangaika na wazungu,wazungu hupitia kwa vibaraka ambao kwa sasa ni hawa watu muwaangalie.uroho wa madaraka utafikiriki wakiwa madarakan wanaweza fanya lolote kumbe ni ubinafs umewajaa.
 
Na hivi leo nimemsikia Polepole akiongea chanel ten asubuhi hii na kuniharibia siku.
Eti vyombo vya habari vimemnukuu katibu mkuu wa hazina na kupotosha umma. Na anasema alimpigia na kumuuliza. Pia mabalozi wa nchi 10 wanaodaiwa kuinyima misaada Tanzania yeye kazipigia balozi 2 na kumwambia hawajajitoa. Yeye kageuka kuwa msemaji wa mabalozi? Ni kwanini hao mabalozi wasiitishe press conference wajisemee au kukanusha? Polepole tambua, watanzania wa leo siyo wale wa 2015 uliowageuka na kuanza kuwapopoa mawe ya katiba mpya. Eti wewe mwananchi unayekerwa, utakuwa mwananchi zaidi ya rais wako? Usiutafute ukuu wa wilaya kwenye media na tupunguziane kupotoshana na kujifanya msemaji wa taasisi na balozi.
 

Unajikanganya. Kama Tz ilipingana na UK kuhusu UDI kule Rhodesia (salsa Zimbabwe) ni sawa na Zanzibar kujitungia katiba yake 2010 halafu kufuta uchaguzi 2015 Wana demokrasia wengine wasiseme kuhusu unafiki wa TZ bara wa kukumbatia ubakaji huu wa demokrasia?
 
Serikali ya ccm itawajuwa watu wa marekani ni kina Nani.

Ujumbe huu umeletwa kwa hisani ya watu wa Tanzania.
 
Ahsante kwa andiko hili kuntu bwana polepole. Mimi nakukubaligi wewe polepole ingawa wengine hawakukubali.
Wewe ni mfano wa mzalendo kamili.
viva polepole
Sikushangai, ni kawaida yetu kushabikia tune ya mwimbo ulioimbwa kwa lugha usioielewa.
Humphrey Polepole ana tumbo kama alivyo mwanadamu yeyote. Hili za sizitaki mbichi hizi ndio la kumfanya aandike maandishi meeengi namna hii jukwaani?
Mbona haya hayakusemwa awali wakati tukipokea fedha? Leo hii Wachina wanasema uchaguzi wa Zanzibar safi, hutasikia kauli yao ikijadiliwa na Polepole sbb imeenda alongside na ahadi ya kuendelea kuisaidia Tanzania.

My friend, siasa ni siasa, hakuna Marekani wala China, tusichopaswa kufanya ni kuwa wanafiki.

Critics wa kweli hawamchagui wa kumkosoa.
 
Hivi China ilishawahi kufanya uchaguzi? Maana ukisifiwa na kichaa umependeza inabidi ujitafakari, leo hii North Korea waisifie Tanzania kwa demokrasia inahitaji akili ya maiti au ya Jecha kuwaelewa.
 
Polepole kila kitu ni expert. Makala yako hai-reflect kilichotukosesha package ile.
 
Kama huhitaji msaada wa wamarekani, na kama unaona haina tija kwa nchi kwa nini useme mcc haitaondoa uhusiano wetu uliopo kati yetu na marekani? kama wanatuingilia na hatuwahitaji sema moja kwa moja hata wamarekani wakivunja uhusiano wetu haina tatizo, sio kupiga miguu wakati unataka kutembea.
 
what the hell..Kwani ninyi na mmarekani nani anamuhitaji mwingine zaidi?

CCM itaendelea kuigharimu nchi hii...tena sana

Huu ni mwanzo tu....

Ila namshukuru Mungu kwa sababu mwisho wa siku utawala huu ndio utakaowaonyesha watanzania kuwa CCM haifai......ni kiini cha matatizo ya nchi hii......

Muda ni judge mzuri sana
 
Naelewa spirit ya watu wanaotamani nchi yetu ijitegemee lakini nachelea kusema ni uwandawazimu kudhani spirit pekee inaweza kuondoa ukweli kwamba pamoja na juhudi zote za serikali ya awamu ya tano kuminya mianya ya ukwepaji wa kodi bado ni tegemezi iwe ni kwa nchi za magharibi au japan na uchina there is no lesser evil wote wapo kwenye kulinda maslahi yao lakini swala la kua na demokrasia ya kweli nadhani ni la maslahi makubwa ya watanzania kuliko ilivyo kwao hivyo hatuwezi kusema kilio cha wazanzibar kuhusu uchaguzi wa mwezi October kilichagizwa na nchi wahisani kila mtanzania asiyesukumwa na unazi wa uchama " he was smelling something fishy" kuhusu uamuzi wa jecha. Nadhani bwana polepole hizo nukuu za mwl. nyerere hazisadii kujenga hoja yako bali zinazidi kuidhoofisha naamini tasfiri sahihi ya nchi kuamua mambo yake si watawala bali wananchi hivyo naamini kama ilivyo batili marekani au nchi nyingine kuingilia mambo yetu ya ndani (yaliyoamuliwa na wananchi) ni kwa kiasi hichohicho (labda zaidi) sio sahihi kwa kikundi kidogo cha watu wanajiita watawala au chama cha siasa kudhani wanaweza kuamua jambo zito kinyume na matakwa ya wananchi na pale zinapokuja athari kubwa kwa nchi nzima kudhani they will win public sympathy kwa kujificha kwenye kichaka cha uzalendo!
 
Ahsante kwa andiko hili kuntu bwana polepole. Mimi nakukubaligi wewe polepole ingawa wengine hawakukubali.
Wewe ni mfano wa mzalendo kamili.
viva polepole
Kama unamkubali huyo Polepole ucpate tabu katoe Posa umpeleke kwako chama chao kishazoea mombasa hana shida kijana

Sent from my TECNO M6 using JamiiForums mobile app
 
Tuweni tu wakweli, wana ccm mlio wengi kwenu nyie chama chenu ni muhimu zaidi kuliko Tanzania. Mpo tayari kuona Tanzania inaangamia lakini sio ccm; tukubali tukatae, iwe ndio sababu ya kukosa pesa au isiwe sababu, Zanzibar ccm imecheza faulo. Tukumbuke maneno ya Nape Nnauye aliposema hata kwa GOLI la MKONO ccm itashinda. Leo eti Polepole unasema watu waende mahakamani au bungeni kubadiri sharia? Kweli? Tanzania hi hi au nyingine? Kwani wewe umaarufu wako ulianzia wapi kama sio kwenye tume ya KATIBA? Bunge la katiba kwa kupitia jingo hilo hilo ndio walikufanya wewe na kina mzee Warioba either kua maarufu au kukutweza, halafu wewe huyo unashauri eti BUNGE lijadiri sharia lililotunga lenyewe; wonders shall never end! Hivi nani asiyejua kua sharia inasema kilicho tangazwa na tume hakuna mahakama yoyote yenye uwezo wa kutangua?
Napendekeza hivi; kama mnavyo tutaka tuanze kua wazalendo kwenye nchi yetu, na nyie ccm ondoeni mawazo haya, "ccm ndio Tanzania na Tanzania ndio ccm" oneni kwamba Tanzania inao uwezo wa kuendelea hata zaidi sana bila uwepo wa ccm, ccm inaihitaji sana Tanzania lakini Tanzania haina uhitaji wa kitu kinacho itwa ccm. Tukifika hapo wala hivi viji mawazo vya kutwambia tuwe wazalendo havitakua na sababu yoyote.
 
Kwanza naomba nitangulie kwa kusema kwamba ni ujinga uliotopea kuamini kwamba kila anayelaumu au kwenda tofauti na dhana hii ya MCC basi ni mwanaccm.

Hoja yangu ni kwamba nani anaeweza kuleta ushahidi wa moja kwa moja kwamba CCM imevuruga matokeo au CCM imejitwalia madaraka kwa nguvu?

Kati ya CCM ya Shein na CUF ya Seif nani aliyekiuka kanuni za uchaguzi wakati wa uchaguzi October 25 mwaka jana?

CCM ya Shein na CUF ya Seif ni ipi iliokimbia meza ya mazungumzo?
CCM chini ya M/kiti Dr. Jakaya imesikitishwa na kufutwa uchaguzi Zanzibar, maneno haya ameyatamka siku ya maadhimisho ya chama pale singida.

Kwa nini akina Msigwa hawajadili zile sababu 8 zilizopelekea kufutwa uchaguzi Zanzibar na badala yake wanaimbisha kasuku wimbo wa CCM?

Na kama Cyber crime hilo suala limepitia bungeni pamoja na sheria ya Takwimu, sasa yeye na wenzie walitakiwa waifanye hiyo kazi wakiwa bungeni lawama haisaidii.
 
Tanzania tuliona mbali, heri Trump kaja.
 
Pole Pole mbona huandiki tena maandiko kama haya??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…