ndolelejiUduhe
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,381
- 4,588
Inafikirisha Kwakweli !Kutokana na mwenendo wa mambo, kila siku nimekuwa nikiwaza hivi kwasababu kuna maamuzi yakifanyika, ni lazima kwanza kuwe na justification ili dunia ielewe ni kwanini watu fulani walifchukua maamuzi hayo magumu.
Kanisa moja kubwa sana hapa nchini, wanajenga picha fulani, na kule Mahabusu yule Simba wa Yuda kashusha waraka wa kimkakati huku yule Askofu machachari nae akitema nyongo bila kusahau Nondo za Bwana Slow Slow.
Kwa kifupi, kuna jambo liinatengenezwa au linajitengeneza, ila kwa ulevi wa madaraka, wahusika ama hawaoni au wanaona ila wanapuuza kwa ulevi tu wa madaraka.
Kote wanakofanyaga maamuzi magumu, huwa kuna sababu, japo Jumuiya za kimataifa na kikanda, huwa zinajitokeza kupinga na kulaani. Hata hivyo, sometimes hufanya hivyo kuzuga tu ikitokea watawala walikuwa wamejisahau sana kwa kutenda maovu dhidi ya ubinadamu bila kusahau watawala kujihusisha na wizi na ufisadi wa kupitilza katika nchi.
Hivyo, kwa mtazamo wangu, naamini jamaa wanaangalia tu kabla hawajasema sasa basi.
Tambueni hata ule waraka wa kamanda kutoka jela, unahitaji akili kubwa sana kujua ujumbe wake unawalenga kina nani hasa. Wengi wanafikiri na sisi wabongo wa kawaida huku mitaani, kumbe umelenge wale wanaoweza kuchukua hatua kututoa hapa tulipo.
Pia, bado najiuliza ni nani alishauri wafanye lile tukilo la kukusanya manoti kutoka kwa madoni huku wengine wakiwa na rekodi chafu kabisa. Mimi naona alieshauri alikuwa ni special agent akitimiza majukumu yake.
Sijuii mmenielewa?
Kama hamjanielewa, basi muda utawasaidia kuelewa.
Muda utaongea 😳🤷🏾♂️ !