Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,788
- 2,690
Habarini!
Moja ya mambo ambayo ni telezi basi bila Shaka ni asili ya binadamu. Zipo nadharia nyingi kama mchanga wa bahari zinazoelezea asili ya kiumbe huyu ambaye ni mtawala wa hii dunia.
Moja ya nadharia kuhusu asili ya binadamu ni pamoja na nadharia ya kidini/kiimani ambayo imegawanyika katika makundi mbalimbali.
Wapo wanaodai mwanadamu aliumbwa na Mungu. Wapo pia wanaosema mwanadamu hakuumbwa na Mungu Bali ni matokeo ya Mabadiliko ya kikemikali yaliyochukua miaka zaidi ya bilioni moja iliyopitia.
Hakuna mwenye ushahidi hilo ndilo linafanya kila kundi kujiamini katika upande wake.
MTAZAMO WANGU.
Bila Shaka mwanadamu hakutokea katika ombwe Bali ni matokeo ya akili Fulani iliyojuu yake maradufu.
Huenda mwanadamu hakuumbwa na Mungu kama watu wanavyodhani. Hii pia ni nadharia.
Wazo hili linaibuka katika akili yangu kutokana maandiko ya Bibilia na QUruan.
Katika kitabu cha Mwanza moja. Kinasema Natuumbe mtu Kwa mfano wetu wakatawale samaki wa baharini, wanyama na ndege wa angani.
Kauli hiyo inadhihirisha moja Kwa moja aliyekuwa akiongea alikuwa Mungu ambaye hakuwa peke Yale bali alikuwa na jopo la wahusika ambao hawakutajwa.
Kauli hii ni fikirishi mno. Hii ni kutokana na muandishi wa kitabu hicho kushindwa kudokeza wahusika waliokuwa na Mungu katika Uumbaji.
Kwa mtazamo wangu; naona mwanadamu aliumbwa na moja ya viumbe wakubwa wenye mamlaka za juu. Na kuumbwa kwake ni kutokana na amri ya mwenyezi Mungu. Na huyu/ hawa waliomuumba Mwanadamu walikuwa moja wa Malaika au mfano wa Malaika.
Sikatai Mwanadamu hafanani Kwa chochote na Mungu bali hufanana na wale viumbe waliomuumba Kwa mfano wao yaani moja wa Malaika wakubwa wenye uwezo.
Kwa nini Mwanadamu aliumbwa?
Kwa mtazamo wangu;
Kuumbwa Kwa mwanadamu ni matokeo ya muendelezo wa mamlaka ya Mungu katika jeshi lake lote la angani. Ikumbukwe dunia ni moja ya jeshi la angani.
Zipo nyota mabilioni Kwa mabilioni. Hivyo katika kila nyota na sayari zake yupo kiumbe na mamlaka inayoongoza nyota hiyo. Katika kurahisisha mamlaka huenda Malaika huyo mwenye uweza mkubwa aliopewa na Mungu ndipo alipomuumba mwanadamu Kwa ajili ya kutawala dunia.
Hivyo mwanadamu aliumbwa Kwa ajili ya kuitawala dunia yaani kuwa muwakilishi wa Mungu japokuwa hafanani na Mungu hata chembe.
Kama vile Wanadamu walivyo na akili na maarifa ya kutengeneza vyombo kama ndege, magari, simu n.k Kwa ajili ya kuwarahisishia mambo yao ndivyo na wao walivyotengenezwa/ kuumbwa kwaajili ya kuweza kurahisisha mambo katika mamlaka za rohoni ambazo ndio hao malaika wakubwa. Ikumbukwe pia kama ilivyo Kwa binadamu kuwa si wote wenye maarifa ya kuunda vitu vya kisayansi halikadhalika si Malaika wote wenye uwezo wa kumuumba mwanadamu.
Mwanadamu ni akili Fulani ambayo ilibuniwa na Malaika Fulani wakubwa ambao walipewa akili na mwenyezi Mungu. Na Mungu ndiye aliyetoa ruhusa ya Mwanadamu kuumbwa japo huenda hakuhusika moja Kwa moja.
Kama mwanadamu angeumbwa na Mungu moja Kwa moja basi angekuwa mkamilifu asilimia Mia moja. Asingekuwa na mapungufu kama aliyonayo sasa. Ndio maana kuna wazo huwa linakujaga akilini mwangu kuwa huenda mwanadamu si kazi ya mikono ya Mungu.
Karibuni