MTAZAMO: Mwanadamu hakuumbwa na Mungu.

Unapokuwa hai ndipo unapoandaa maisha utakayoishi baada ya kifo.
Sasa subiria Ukifa ndipo utayajua haya uyasemayo na nadharia zote utazikuta huko.

Yeah mkuu!!

Huenda upo kwenye mawazo ya mtu Fulani bila wewe kujua sema wewe unajiona unaishi halisi. Utakuwa huru siku huyu mwenye kuwaza atakapokoma kufikiria habari zako.

Be blessed
 
Yeah naafikiana na wewe juu ya hilo la kutomuona Mungu ila nimejaribu kueleza msimamo wangu juu ya uwepo wake na malipo yake kwa waja wake
 
Inawezekana.maana binadamu ndo kiumbe wa mwisho kuumbwa.mungu alishaumba vitu vyoote.wanyama,mimea,majini,miti,n.k.
Na wakati mungu anamuumba adam kwa udongo.ibilisi alikuwa anamuona adam akiwa amelala.akawa anamchezea kama mdoli.alipopuliziwa adam roho na kuwa kiumbe kamili.mungu akawaambia malaika na viumbe vilivyopo mbinguni wamtukuze adam.ibilisi akakataa.ndipo akalaanika.
 
Yeah naafikiana na wewe juu ya hilo la kutomuona Mungu ila nimejaribu kueleza msimamo wangu juu ya uwepo wake na malipo yake kwa waja wake
Kweli mkuu.
Mungu yupo na kuelezea uwezo wake ni kukufuru Kwa maana haulinganishwi na chochote.

Na ndio maana wakati mwingine naamini hata Shetani hamjui Mungu na hajawahi kumuona japo nahisi aliwahi kusikia sauti yake
 
Zote ni nadharia mkuu.

Hakuna hata mmoja mwenye uthibitisho wa kile anachokisimulia. Ndio maana inaitwa imani yaani kuwa na uhakika ya mambo yatarijiwayo
 
Hiviii ulipasoma na pale palipoandikwa akachukuwa ubavu wa mwanaume akamuumba mwanamke kwa udongo.

Ulielewa ile sehemu anasema "akampulizia pumzi yake ya uhai akawa hai"???

Unajua ni siku ya ngapi Mungu alimuumba mwanadamu?

Someni bwanaaaaaa msituchoshe na mitazamo isiyokamilika.
 
Viumbe gani wenye akili na utashi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…