DidYouKnow
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,229
- 1,950
Nikiri kwamba andiko hili limepata nguvu kutokana na mauaji yaliyofanyika katika Bar ya Lemax, Sinza, kama yalivyoletwa na Tusker Bariiiidi. Kupitia taarifa ya ITV, ukichunguza kwa umakini utagundua kuna mhanga wa hili tukio, mwili wake umelala kwenye kiti, ingawa polisi wapo wakirandaranda kila kona, hakuna tukio lolote kubwa linalofanyika la kiuchunguzi zaidi ya kuchukua maelezo ya mashahidi na (labda kupiga picha), na hatimaye wataondoka na miili ya marehemu.
Video iko hapa
www.jamiiforums.com
Hii imekuwa ni kama kawaida ya jeshi la Polisi Tanzania inapofanya uchunguzi wa kifo. Tukio kubwa wanalokuja kulifanya ni kubeba miili ya marehemu tu. Huwa hawako serious. Ndio maana baadhi ya kesi huwasumbua sana mahakamani wakikutana na wakili mzuri kwani baadhi ya evidence wanakuwa waliziacha kwenye eneo la tukio la uhalifu (crime scene).
Ukiangalia namna Polisi Tanzania wanavyo treat crime scene utajua hawana mafunzo ya kutosha ya kufanya uchunguzi wa makosa ya jinai. Na kama kuna mafunzo wanayapata huko vyuoni kwao, basi ni bora hayo mafunzo yafutwe tu kwani hayana tija. Polisi Tanzania wanapofanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu, wanafanana na kijana wa mtaani anayetafuta mgoni wake, lakini tofauti ni kwamba wao Polisi wana access ya kupata taarifa maeneo mengi kama TCRA, NIDA, Bank na sehemu nyingine ambazo raia wa kawaida hana.
Ukiangalia video za matukio yote ya mauaji hapa Tanzania utashangaa kuna uchunguzi gani unafanyika zaidi ya wao kwenda kwa spidi kukusanya mwili au miili ya wahanga.
Hakuna video ambayo waweza ona hata kamba tu ya kutenga eneo la tukio la mauaji ili kutolichafua imewekwa. Huoni hata alama za utambulisho (identification markers) kama stendi za plastiki zenye namba, au bendera inayoonesha alama za ushahidi katika eneo la tukio la uhalifu. Polisi naamini wanajua kwamba vitu vidogo kama hizo identification markers husaidia kufunua, kurahisisha, kupanga na kubaini vitu vingi vya ushahidi unaopatikana kwenye eneo la matukio la uhalifu. Inapotumiwa vizuri inawaruhusu hata wengine kuelewa kwa urahisi tukio zima.
Wito kwa Polisi Tanzania na Vyuo Vikuu vya Tanzania, kujenga ushirikiano na vyuo vikuu vya kigeni ili kuanzisha kozi ambazo mwisho wa siku zitawafanya Polisi Tanzania wawe wameiva katika usindikaji na ufungaji wa ushahidi, mbinu za uchunguzi wa eneo la uhalifu, kusimamia na kufanikiwa kumaliza uchunguzi wa mauajib, mbinu za upigaji picha za uchunguzit, stadi za mahojiano na kuandaa taarifa n.k
Hapa ndipo tunapohitaji kuwa na vijana wenye ufaulu mzuri kutoka kidato cha 6 wanaopaswa kujiunga Polisi Tanzania kwa ajili ya mafunzo kama haya. Na mafunzo haya yanapaswa kutolewa kwa mamia ya Polisi nchini Tanzania, na si kupeleka mtu mmoja au wawili nje ya nchi halafu anaishia kuhamishiwa makao makuu ya Polisi Tanzania.
Chini nimeweka video ya Sinza na picha ndogo za mfano wa jinsi Polisi Kenya wanavyofanya uchunguzi wa eneo la tukio la uhalifu kwa kupitia tukio la karibuni la Polisi Caroline Kangogo anayesadikika kujiua (wengine wanaamini kauawa) baada ya kuua watu wawili.
Video iko hapa
Dar: Mauaji Lemax Bar Sinza kwa Remmy. Kabla ya kujiua, Alex Korosso alimpiga risasi Gift Mushi
Watu wawili wamefariki Dunia jioni hii Saa 11...baada ya Jamaa anayejishughulisha na Biashara ya Madawa ya Binadamu Alex Koroso kumpiga risasi Jamaa ambaye jina lake halijajulikana lakini anasadikika ni Mziba Pancha wa Maeneo hayo na kisha yeye kujiua kwa kujipiga Risasi kwenye shingo na...