Mtazamo upoje kuhusu ajira?

Reagan Carima

Member
Joined
May 20, 2015
Posts
44
Reaction score
194
Sijui kama nawaza sawa au lah. Mimi naona kuwa mikataba au kipindi kilichowekwa mtu kufanya kazi mpaka kustaafu ni adhabu ikiwa hutaweza kujipa tafsiri binafsi.

Nilibahatika kupata ajira yangu ya kwanza katika kampuni moja nikiwa na miaka 23. Ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu sana hasa ikizingatiwa nimetoka katika familia ya chini tena kijijini.

Nilifanya kazi mwaka wangu wa kwanza na niliutumia katika kujifanyia tathmini zaidi kuhusu. Malipo, thamani ya muda wangu, thamani ya kile ninachokifanya, malengo ya kampuni kwangu na malengo yangu binafsi.

Nikagundua kuwa kampuni iliniajiri ili inilishe, inivishe na inilaze na si vinginevyo. Nikatambua kuwa thamani ya muda wangu ilikuwa ghali×10 ya mshahara niliokuwa naupata.

Kwanza niligundua kampuni imemjengea mfanyakazi mazingira ya kutobanwa sana ili usiichoke kazi kirahisi, ikizingatia pale niliwakuta watu ambao wametumikia kwa miaka zaidi ya 10 ila kiukweli sikuona cha zaidi kati yao.

Niliamua kuketi chini na kujitafakari zaidi. Katika maisha yangu nina kawaida ya kufanya maamuzi magumu hivyo kama kawaida nilifikia maamuzi magumu.

Niliweka mpango mkakati wa kuendelea kutumika pale kwa miaka mitatu kisha nisitishe mkataba.

Kwakuwa nilikuwa na malengo basi nilikuwa naangalia sana target na time rate maana nilipanga kuwa baada ya pale nikafanye biashara na nisiajiriwe tena. Ilinibidi kusimamia mambo yangu vyema kwakuwa ilitakiwa ndani ya muda ule niwe nimeshapata mtaji.

Kweli Mungu ni mwema muda ukifika na nikapanga kuacha kazi mwezi mmoja mbele. Unajua nini? Ajabu ni kuwa niliongezewa majukumu (Nilipandishwa ngazi) Haikuwa wakati mrahisi kwangu kwani kama unavyojua kila mmoja anapenda kupanda cheo. But trust me sikupokea ile offer ile siku naletewa barua nilipoisoma tu nikamaliza niliandika barua yangu yakurisign.

Nilifanya vile kwakuwa ingekuwa aibu kwangu kushindwa kusimamia mipango ambayo nimeiweka mwenyewe kisha nifuate mipango ya kampuni.

Basi bhana kweli niliacha kazi nikaendelea na maisha yangu. Kwa kipindi kile tayari nilikuwa nimeanzisha biashara yangu hivyo nikahamishia huko nguvu zangu zote.

Namshukuru Mungu kwani nilichokiona nimekipata. Kwa sasa napata pesa yangu hata kama sio nyingi ila ni ya amani na haina majungu na hata ikitokea nikawa sipo kazini basi familia yangu inaweza kusimamia biashara na pesa ya kula ikapatikana.

Ninachowaza zaidi ni kuhusu mzee wa miaka 65 anapostaafu na kupewa ile pension yake huwa ni kwa malengo gani hasa kwa sisi ambao mshahara wote huwa tunalia maandazi ya sukari??

Kumpa mzee Milioni 100 ni kumsukumiza kaburini tu afe kabla ya mida wake.

Niishie tu hapa kwa leo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lengo lako lilikua nini? Kuacha kazi ili uongeze kipato zaidi kwa kujiajiri au kuwa huru kufanya kazi bila usimamizi wowote? Ulianza vizuri lakini mwishoni umenichanganya.
 
Nilipenda nione How Your Plan More Economic, ila nimeona More Freedom.
Of course plan yangu ni kukuza kipato changu zaidi ila more advantage ni kwamba kwa sasa i have my own freedom.

Mfano kwa sasa naweza kupanga mipango yangu zaidi bila kuingiliwa na maamuzi ya mtu mwingine. Hata kama biashara yangu itanihitaji kusafiri au nataka kufanya survey kuhusu biashara yangu. Am free. Huo ndio uhuru niliomaanisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lengo lako lilikua nini? Kuacha kazi ili uongeze kipato zaidi kwa kujiajiri au kuwa huru kufanya kazi bila usimamizi wowote? Ulianza vizuri lakini mwishoni umenichanganya.
Kupata uhuru ambao utaniruhusu kuutumia kwa manufaa zaidi uwanja wa mawazo yangu.

Baada ya kutimiza hili basi matokeo ya uhuru huu ni kukuza kipato changu. Na pia sikupendelea zaidi pesa ambayo nitalipwa mwisho wa mwezi kwakuwa binafsi matatizo yangu huwa hayana muda maalum hivyo nilipenda niweze kuyatatua muda wowote yatakaponikabili na sio mpaka iwe mwisho wa mwezi
 
Na hili ndo linawatesa sana vijana wengi sasa hivi, kutaka kuwa na freedom, freedom ya nini kama huingizi hela? Kuna mmoja aliacha kazi yenye mshahara mkubwa kama 2M akataka kuwa free.

Akajiingiza kwenye kilimo sasa hivi anajificha kama kindege haonekani mtaani wala haijulikani analala wapi, mambo yamemvurugikia kabisa, fanyeni kazi ufree utawaponza vijana!
 
Hivi mnatafsiri vipi mtu anavyosema Freedom?

Unaachaje kazi ikiwa haujaweka misingi mbadala ya kipato zaidi ya kile ulichokuwa unalipwa?

By the way suala la kuajiriwa kila mtu alitafsiri kadiri ya upeo wake utakavyomruhusu.

Kwa upande wangu nipo tofauti sana.

Unasema mtu ameacha kazi ya 2M
Kwa hesabu zangu mimi 2M sio pesa nyingi maana nikipiga hesabu ya siku ni kama kuingiza around 67,000 per day.

Means kama mtu ataweza kuacha kazi hii basi lazima anao mradi ambao upo tayari kumpa kuanzi 70,000 kuendelea na si chini ya hapo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah lakini kama una uwezo wa kutengeneza zaidi ya hiyo kwanini usifanye hivyo?

Maana calculate kodi, usafiri, malazi, dharura utakuta unasave kiasi kidogo sana au husave kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitaacha kazi nikiwa na uwezo wa kuzalisha faida mara mbili ya mshahara wangu wa sasa, kinyume na hapo acha mwajiri aendelee kuninyonya!
 
Tatizo wanaponzwa na motivational speakers bila mtu kujitathmini yupo kwenye level gani.

Watu wenye akili huwa wanaanzisha biashara wakati bado yuko kwenye ajira.
Halafu badae biashara ikishasimama na ikawa inanuingizia pesa mara 5 ya mshahara wake hapo ndipo hufanya maamuzi ya kuacha kazi.

Sasa vijana wa siku hizi wanafuata mkumbo kuacha kazi eti ukimuuliza kwa nini ameacha atakwambia amefungua kiduka cha kuuza maharage na sukari.
 
Msimcheke sababu safari yake haijafika mwisho Wala hujui anafanya Nini huku aliko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
More economic inaanza na freedom.
watu wanapenda kuambiwa tyr nishafanikiw'
tyr nin majumba'
magari.
lkn ktk hatua mhim zaid kama hizi matomaso ni wengi sana'
hata hivyo jambo la kufanikiw ktk maish bado tafsri yake ni tata sana.
mtoa mada hadi hapo ushafanikiw sn kw ujasiri wa kutimiza malengo yako ya kusimama wew kama ww badal y kusubir kuongozw kam mbuzi'
nayo ni mafanikio makubwa hata usipotoboa ww leo'
kesho nayo ni siku kwa kizaz chako kitabeb ujasiri na uwezo wako'
watatusua tu. kikubw n kuacha alama.
kutumikia kaz moja had miaka 60+
ni adhabu kubw san asikwambie mtu'
hasa hizi kaz za ualim' askari nk.
kuna watu wameshapat magonjw yasiyoambukiz'
magonjw ya akili'
sbb y mazingira y hizo kazi
bravo mtoa mada.
 

Ishu sio pesa mzee, tunacho angalia ni TIME VALUE.

Na usimkejer mtu ambae alifer kufanya jambo fulani, tunajifunza baada ya kufer, sasa mtu kafer kwenye kilimo unamuona kama mpumbavu hivi, je angefanikiwa ungesemaje???
 
Ishu sio pesa mzee, tunacho angalia ni TIME VALUE.

Na usimkejer mtu ambae alifer kufanya jambo fulani, tunajifunza baada ya kufer, sasa mtu kafer kwenye kilimo unamuona kama mpumbavu hivi, je angefanikiwa ungesemaje???
Sawa mkuu!
 
Mtoa mada ni mbinafsi inaonekana hawawazi hata watoto wake. mm nimejifunza sana sometimes mama mzazi wa mtu anaweza akawa hata muuza genge. Lakini kupitia lilile genge watoto wakijifunza biashara na watakapo kuwa wa kubwa wata fanya zaidi. Sasa wewe kenua mdomo wako hivyohivyo usijue kama kuna wanaokufuata ndipo hapohapo watoto wako wataona maisha bila ajira haya wezekani na utawaweka nyumbani mwako.

Kwa mm ninavyoona ni Bora kujiajiri hata Kama ni pesa ndogo kisia gani mungu atakubariki hata yesu alilisha maelfu kwa kidogo. Tafsida halisi ya kuajiriwa nimtumwa wa mwenye akili. Ila sio ndo kuingiza hela nyingi na kuwa salama.

Kwa mm nilivyo experience huko nyuma Kama ajira za private fanya ili upate kutengeneza msingi ila sio za kutegemea kabisa. Mara utasikia hawajapata miashara miezi minne Sasa hapa mtu. Unakuwa umefungwa vyote akili, muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…