Reagan Carima
Member
- May 20, 2015
- 44
- 194
Sijui kama nawaza sawa au lah. Mimi naona kuwa mikataba au kipindi kilichowekwa mtu kufanya kazi mpaka kustaafu ni adhabu ikiwa hutaweza kujipa tafsiri binafsi.
Nilibahatika kupata ajira yangu ya kwanza katika kampuni moja nikiwa na miaka 23. Ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu sana hasa ikizingatiwa nimetoka katika familia ya chini tena kijijini.
Nilifanya kazi mwaka wangu wa kwanza na niliutumia katika kujifanyia tathmini zaidi kuhusu. Malipo, thamani ya muda wangu, thamani ya kile ninachokifanya, malengo ya kampuni kwangu na malengo yangu binafsi.
Nikagundua kuwa kampuni iliniajiri ili inilishe, inivishe na inilaze na si vinginevyo. Nikatambua kuwa thamani ya muda wangu ilikuwa ghali×10 ya mshahara niliokuwa naupata.
Kwanza niligundua kampuni imemjengea mfanyakazi mazingira ya kutobanwa sana ili usiichoke kazi kirahisi, ikizingatia pale niliwakuta watu ambao wametumikia kwa miaka zaidi ya 10 ila kiukweli sikuona cha zaidi kati yao.
Niliamua kuketi chini na kujitafakari zaidi. Katika maisha yangu nina kawaida ya kufanya maamuzi magumu hivyo kama kawaida nilifikia maamuzi magumu.
Niliweka mpango mkakati wa kuendelea kutumika pale kwa miaka mitatu kisha nisitishe mkataba.
Kwakuwa nilikuwa na malengo basi nilikuwa naangalia sana target na time rate maana nilipanga kuwa baada ya pale nikafanye biashara na nisiajiriwe tena. Ilinibidi kusimamia mambo yangu vyema kwakuwa ilitakiwa ndani ya muda ule niwe nimeshapata mtaji.
Kweli Mungu ni mwema muda ukifika na nikapanga kuacha kazi mwezi mmoja mbele. Unajua nini? Ajabu ni kuwa niliongezewa majukumu (Nilipandishwa ngazi) Haikuwa wakati mrahisi kwangu kwani kama unavyojua kila mmoja anapenda kupanda cheo. But trust me sikupokea ile offer ile siku naletewa barua nilipoisoma tu nikamaliza niliandika barua yangu yakurisign.
Nilifanya vile kwakuwa ingekuwa aibu kwangu kushindwa kusimamia mipango ambayo nimeiweka mwenyewe kisha nifuate mipango ya kampuni.
Basi bhana kweli niliacha kazi nikaendelea na maisha yangu. Kwa kipindi kile tayari nilikuwa nimeanzisha biashara yangu hivyo nikahamishia huko nguvu zangu zote.
Namshukuru Mungu kwani nilichokiona nimekipata. Kwa sasa napata pesa yangu hata kama sio nyingi ila ni ya amani na haina majungu na hata ikitokea nikawa sipo kazini basi familia yangu inaweza kusimamia biashara na pesa ya kula ikapatikana.
Ninachowaza zaidi ni kuhusu mzee wa miaka 65 anapostaafu na kupewa ile pension yake huwa ni kwa malengo gani hasa kwa sisi ambao mshahara wote huwa tunalia maandazi ya sukari??
Kumpa mzee Milioni 100 ni kumsukumiza kaburini tu afe kabla ya mida wake.
Niishie tu hapa kwa leo
Sent using Jamii Forums mobile app