SoC02 Mtazamo wa msamaha

SoC02 Mtazamo wa msamaha

Stories of Change - 2022 Competition

Gmak developer

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Habari watanzania na wadau wote kwa ujumla.

Katika chapisho hili nalenga kukutazamisha angalau kwa sehemu kuhusu msamaha, ninauhakika utakapomaliza kulisoma kwa utulivu utabadili au kuboresha mtazamo wako kuhusu msamaha.

Katika chapisho la kiingereza liitwalo safari ya mahusiano binafsi (journal personal relationship) toleo la mwaka 2011 kila wanandoa katika ndoa 68 walikubaliana kuwa na dakika nane kuongelea kuhusiana na namna yoyote ambayo mwenza mmoja wapo alivunja taratibu za ndoa hiyo.

Kisha baadae wakahojiwa na watafiti ili kujua ni wangapi wameweza kusameheana alafu walienda kupimwa msukumo wa damu na kukuta wale walio weza kuwasamehe wenza wao pamoja na waliosamehewa msukumo wa damu katika miili yao ulishuka. Hii inadhihirisha kuwa msamaha unafaida kwa watu wote kwa kuleta afya ya akili pia na faida kiafya.

Kuna madaraja manne katika kusamehe kama ifwatavyo:

Sifuri, hii ni pale ambapo mtu hataki kusamehe kwa namna yoyote ile, na anawaza hata njia ya kulipa kisasi.

Kigezo, hili ni daraja la pili la kusamehe ambapo mtu anajisemea "nitamsamehe ila mpaka aniombe msamaha" mwingine anasema "nitamsamehe ila mpaka ahaidi kutokurudia tena".

Afadhali, hili ni daraja la tatu la msamaha ambapo mtu anasamehe bila kujali kigezo chochote hata asipoombwa msamaha.

Takatifu, hili ni daraja la msamaha ambalo mara nyingi mzazi anakuwa nalo kwa mtoto wake. Ninamaanisha mtu anakuwa alishajiandaa kusamehe kosa lolote kabla hata halijatokea na bila kujali ukubwa wake.

Hivyo basi ninashauri daraja la msamaha la kwako liwe angalau kwenye afadhali. Ni ngumu kujua kwa nini fulani amekukosea na pia tambua watu wametofautiana malezi na fikra, tambua wewe siyo mkamilifu na wala usitarajie mwenzako ni mkamilifu. Pia jua waliodumisha uhusiano siyo kwasababu ni wakamilifu ila kwa sababu hata wakikosea wanawahi kusameheana.

Ni hitimishe kwa kusema usiwe mgumu kusamehe na usione taabu kuomba msamaha.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom