Mtazamo wa raia wa nchi za Afrika wanaoishi Ulaya na Marekani juu ya Hayati Rais Magufuli

Huo ndo ukweli kabisa hayati Magufuli atabaki kuwa best President
 
mmh jamaa kasema Samia watamu win na imekuwa hivyo. naona Samia hana uwezo
 
Kuna baadhi tu ya Mambo sikukubaliana na Magufuri, but moyoni nilim support!

Kuna rafiki yangu anaishi Free state South Africa, siku wameenda kumzika Raia wa Congo aliyefia huko huko, Sasa Kuna Mcongo mmoja akawa akawa anamsifia Sana Magufuri, akielezea Yale akifanya kwa muda mfupi kwamba hakuna Rais hapa Africa amefanya....

Jamaa akasema anatamani Marais Africa wangekua Wakuu wa Majimbo na Magufuri angekua Rais wa Africa yote ..

Yule Mtanzania akawa anamwambia jamaa kuhusu Mapungufu ya Magufuri, kuhusu Demokrasia, Uhuru wa kutoa Naomi n.k...

Mcongo akawa anasema huwezi kupata Rais Aina ya Magufuri akawa laini laini, wapo wachache wataumia kwa faida ya wengi....

Ukaibuka mzozo mkubwa wakiwa Makaburini yule Mcongo akashikwa na hasira akamchunja Shari yule rafiki yangu Mtanzania, akimwambia unawezaje kusema maneno mabaya kuhusu Magufuri, Rais ambaye wao Wacongo wanatamani angekua Rais wao!? Wakawa wanarushiana maneno huku yule Mcongo bado kamkunja Rafiki yangu........ That time ndo Kuna fununu Magufuri Mgojwa! Rafiki akamropokea yule Mcongo "Hivi wewe Mcongo unamjua vizuri Magufuri kuliko Mimi Mtanzania? Sasa kwa taarifa yako Magufuri mwenyewe hivi ninavyoongea Kafariki!" (Magufuri alikua bado mzima)

Yule Mcongo akamwachia rafiki yangu akaanza kulia, Watanzania wengine wanaanza kumbembeleza wakimwambia yule Mcongo kuwa rafiki yangu anadanganya Magufuri ni Mzima..,..

Baada ya week Kama taarifa rasmi inatoka kuwa Magufuri Kafariki, nikawa MTU wa kwanza kunwambia rafiki yangu, na yeye akatoka kwenda Town Center kutafuta Mcongo ampe taarifa za msiba wa Magufuri...,. Akakutana nae, akampa taarifa za msiba, anamwambia Mcongo alilia Kama mtoto mdogo, akimtuhumu Mungu kuwa amekosea..,.

So binafsi nakubariana na wewe kuwa nje ya Tanzania wanamwelezea vizuri Sana Magufuri..
 
Naona wazee wa legacy mko busy Sana wiki hii na nyuzi uchwara..

Awamu yote hamkuwahi kukanyaga Ulaya na US sasa roho inawauma mkiona mama anachanja mbugha..Ulaya anaenda na Kazi zinasonga..

Huyo jamaa yako kwa nini hakuja japo kufanya Kazi Bongo aone moto wa Dhalimu Jiwe? Au mwambie aende Rwanda alafu aje kusimulia upumbavu wenu hapa.

Jitu liliharibu uchumi,lilikuza deni la Taifa hatari tupu na lilikuwa katili,liongo na jizi afu unasemaje?
 
Nchi huwa inabadilishwa na mtu mmoja na mkimmis itachukua muda Sana labda angekaa miaka kumi nchi hii ingeweza kuwa na mwendelezo wa Rais mwenye mwona Kama yy lakin sasa itachukua muda Sana maana tutaenda na kikwete system kwa miongo kadhaa labda itokee maajabu Sana hiki kizaz Cha kikwete kiishe
Itatuchukua muda kumpata mtu kama magufuli

USSR
 
One thing is for sure, Watanzania tutamkumbuka Magufuli kwa mema mengi aliyotufanyia.

He was the president of his own calibre.

He had the guts and could get things done.

He was a true son of Africa.
Bila wewe utamkumbuka,binafsi never..nilimpinga since ni Waziri hadi keshokutwa..

Kwangu namchukulia kama Rais ambae alikuwa hatumii akili ..Mingi ya miradi yake ni hasara kubwa kwa Nchi,tusubirie sgr ikamilike mtapata majibu
 
Kwangu this is the best system,ule upumbavu wa kuabudu na kujiamulia miradi isiyo na maana kwako ndio kitu?

Kwanza kwa uongozi wake maskini waliongezeka , wawekezaji walikimbia ,madeni ya nchi yaliongezeka ,kilimo kilokufa ..
 
Tuwekee hapa izo propaganda nasisi tuzijue mkuu
Kudanganya kwamba uchumi unakua kwa 7% kumbe uongo,kudanganya kwamba tunajenga kwa pesa zetu kumbe mikopo ya Kibiashara, kudanganya kwamba Rushwa imeisha kumbe watu wake walikuwa wala rushwa wakubwa ,kufukuza watu waliotoa uozo serikali yake kama Assad nk..

Kudanganya watu kwamba tiba asili na miujiza inatibu uviko kumbe uongo,kutukana na kudhalilisha wenzie,,kuharibu zao la korosho,mbaazi,ufuta,mahindi ,sukari,..

Watoto kurundikana madarasani na marufuku kuibua kwenye habari,kutosha watu,ofisini watu walikuwa wanaogopana hapo waliokuwa wanaogopwa kutumia fursa hiyo kuiba na kufuja ..

Orodha ni ndefu sana
 
Utakuwa ni punguani Kama unahitaji jirani kukuelezea tabia za baba yako.
Wewe ndiye unayeishi nae unamjua nje ndani kwamba akirudi amelewa huwa anavua nguo mbele yenu, mnamfunika Kwa mito ya makochi, akiingia kulala huwa anajisaidia haja zote kitandani.
Jirani Hawezi kujua hayo.

Huyo pimbi unayesema ana PhD ulimuambia kwamba Jiwe alikuwa anapora hela za Watu hasa wafanyibiashara Kwenye akaunti zao?Ni theory gani ya uchumi hiyo?

Ama ni theory gani ya uwekezaji wa kiuchumi iliyomtuma kujenga chato airport Wakati hata kunguru tu hawatui hapo?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Alikuwa mjinga wa mwisho,watu wa hivyo jibu langu kwao ni kwamba wangekuja kufanya maisha Tzn waache kusimuliwa mambo ya mapapai kuwa na korona
 
Mwisho wa siku Mwenyezi Mungu, Mola Wetu Mlezi, anatujua sisi wanadamu vizuri kuliko tunavyojijua sisi. Akaamua kumchukua Mh Rais.
 
Unfortunately mapunguani ndio wengi,watu wenye akili ndogo
 
Mwisho wa siku Mwenyezi Mungu, Mola Wetu Mlezi, anatujua sisi wanadamu vizuri kuliko tunavyojijua sisi. Akaamua kumchukua Mh Rais.
Tunamshukuru Sana kwa kazi nzuri na iliyotukuka kututolea katili yule.
 
Kwa mara ya kwanza nakuona umepevuka. Kongole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…