aise
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 5,175
- 16,488
Kuna mtazamo potofu wanao watu wa dini, wanaamini mtu ambaye haamini uwepo wa Mungu basi ni mtenda maovu, hana maadili n.k
Mtazamo huu ni potofu.
Maadili ya mtu hayaamuliwi na imani yake ya kidini, bali misingi yake ya utu, malezi na jamii inayomzunguka.
Kuna sehemu tulikuwa tunafanya kazi, kukawa na baadhi ya watu (wakristo na waislamu) wanabishana kwamba Yesu hawezi kuwa Mungu, wengine wakisema Yesu ni Mungu, Wengine wakidai Yesu ni mtoto wa Mungu.
Baada ya kuwasikia wote kwa muda mrefu, mimi nikawaambia Mungu Hayupo,
Basi baada ya kusikia nimesema hivyo, wale wenye imani ya Uislam wakaongea maneno ya kiarabu huku wengine wakisema huu ni msiba mzito.
Wengine wakasema kama nimekataa uwepo wa Mungu, basi mimi nastahili kufa / kuuwawa.
Wakidai kwamba kama nimesema Mungu hayupo, basi mimi nitakuwa mtu muovu, ambaye sitakiwi kwenye jamii.
Lakini hiyo siyo kweli, maadili hayategemei Dini pekee.
Historia na Jamii zinaonyesha kuwa kuna waumini wa dini waliofanya maovu, kama vile Ufisadi, Vita, au Ubaguzi.
Lakini pia kukiwa na Atheist Waadilifu, Waaminifu, na wenye kusaidia wengine.
Kwahiyo Uadilifu unatokana na uelewa wa mtu kuhusu mema na mabaya, si imani ya kidini pekee.
Watu wengi wanao amini Mungu hujitahidi kuishi maisha yenye maadili mazuri kwa sababu wanaogopa kupewa adhabu na Mungu, na wakiamini kwamba watapewa zawadi na Mungu huko mbinguni.
Wapo wanao amini kwamba watapewa Uzima wa milele, wapo wanao amini kwamba wataenda kuishi maisha ya anasa Mbinguni kwa kunywa Pombe, au kuogelea kwenye mito yenye maziwa na asali huku wakiwa na Mabinti mabikira.
Lakini kwa upande wa watu wasio amini uwepo wa Mungu, wanaishi kwa misingi ya Uaminifu, Uadilifu Huruma na Haki sawa kwa wote.
Si kwa sababu ya matarajio ya zawadi baada ya kifo, bali kwa sababu wanatambua umuhimu wa mshikamano wa Kijamii na haki kwa wote.
Yaani kwa ufupi Atheist tunaishi kwa maadili si kwa sababu ya hofu ya kupewa adhabu na Mungu, au kwamba kwa sababu tunahitaji mabikira huko Peponi, bali kwa sababu tunaelewa athari za matendo yetu kwa wengine.
Watu wa dini wanatakiwa watambue kwamba,
Mtu anapochagua kuwa Atheist, mara nyingi hiyo ni matokeo ya Safari ya kuuliza maswali, kuchunguza kwa kina Imani mbalimbali na kuamua kufuata njia ya Hoja na Ushahidi,
Badala ya kufuata mafundisho fulani kwa sababu tu yamerithishwa.
Kwahiyo ni vyema kuhukumu kwa tabia za mtu badala ya kuhukumu kwa kungalia imani ya mtu.
Eneo Hatari, ndiyo eneo Salama