Simba hawapo vibaya sana na ni kweli wakicheza kimataifa huwa wanabadilika sana sijui hata ni kwanini. Lakini kitu ambacho naona kitakwenda kuwaangusha Simba ni kuwa haina washambuliaji wa uhakika wanaokupa matokeo. Ukiangalia washambuliaji waliondoka Phiri na Baleke na hao walioletwas Jobe na Koulban hakuna tofauti yoyote kubwa kati yao.. Hakukuwa na sababu ya kuwaacha Baleke na Phiri ilihali unakwenda sokoni kuleta watu wanaolingana nao kiuwezo.
Na mbaya zaidi pale mbele akipangwa mkalimani ndio basi tena. Watu tumepiga kelele sana kuhusu mkalimani kuikaba timu wapi sio viongozi wa Simba wala benchi la ufundi wanaona au kusikia badala yake anapangwa mechi zote mwanzo mwisho. Ngoja tuone kesho labda watabadilika.