Uongozi wa nchi hauna majaribio. Hata vile, kwa maneno na matendo ya viongozi wa upinzani, ni dhahiri hawajawa tayari kuongoza nchi. Japo wanaongoza katika baadhi ya Halmashauri na Majimbo ya uchaguzi, hawajaonesha utofauti wa mabadiliko, zaidi ya hali kuendelea kuwa mbaya.