tindo,
Sawa wewe mkubwa unataka nikupe shikamoo? au tuzungumze hoja yetu hapa?
Unanishambulia kwa udogo wangu kutaka kunipoteza confidence, unaweka kuwa nimeandika mahaba kitu ambacho sijaandika hivyo pia unataka kuniaminisha nilichokiandika sicho wakati nimeandika mwenyewe. Huwezi kuzungumzia uwezo wa akili yangu ikiwa tu husomi na you put words on my mouth. Hahaha mie sijasema wala usije sema nime edit post yoyote bado husomi unajibu na unaona kitu amabcho akili yako inataka kuona. .
Sijasema mheshimia Tundu Lisu kakumbatia mashoga, nimeona anahojiwa kwenye taarifa ya habari BBC anakubali kwa kusupport ushoga kwa kauli yake mwenyewe Tundu Lisu kwa hilo sijaona mimi tu wengi wameona ila wewe hujaona. .
Ila siwezi kuendeleza mjadala na wewe hauko kunifundisha kwa madai ya ukubwa wako na unayoyazungumza ni yale yale, unajikita kwenye maneno ya fedheha na matusi kitu ambacho si siasa kwangu. Nina haki ya kusema sitaki upinzani huu, wewe una chama mimi sina chama ni haki yangu, sijakutukana au kukuponda kwa kufata siasa za upinzani ni haki yako. Unaniletea Uditekta kwenye huu uzi, alafu unadai Magufuli ni ditekta wakati wewe mwenyewe ni ditekta. Kwa kuwa una umri basi sisi wadogo hatuwezi kuwa na mawazo chanya tusihi unavyotaka wewe. .
Tatizo mtu yeyote anayeandika kuhusu raisi Magufuli basi anamnyenyekea kitu ambacho si kweli. Magufuli sio Mungu siwezi mnyenyekea, na yeye kama binadamu wote ana mapungufu mengi hata kwenye uongozi wake hajakamilika sio malaika yeye kwa hiyo sishangai akikosea. Ila mie nimeandika mtazamo wangu tu kama wewe umeona kunishambulia kuwa ni mtazamo mbovu sawa, siwezi kushambulia wa kwako na siwezi kukubaliana nao pia ni mawazo yako, sitokuvunjia heshima just because you lose mine which matters nothing for me, nikikujibu vibaya I will lose mine on respect which is worth everything to me. .